PostGE2025 Ujumbe wa SADC: Waangalizi wetu walinyanyaswa nchini Tanzania na kulazimishwa kufuta picha

PostGE2025 Ujumbe wa SADC: Waangalizi wetu walinyanyaswa nchini Tanzania na kulazimishwa kufuta picha

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Licha ya kubeba vitambulisho vyao vya uangalizi, waangalizi wetu waliokuwa Mjini Tanga walikabiliwa na mahojiano makali kutoka kwa vyombo vya usalama, nyaraka zao rasmi zikiwemo pasipoti, zilichukuliwa (ingawa baadaye zilirudishwa), na walilazimishwa kufuta picha zinazohusiana na kazi ya uangalizi kutoka kwenye vifaa vyao rasmi.

Pia soma > GE2025 - Waangalizi SADC: Uchaguzi Mkuu wa Tanzania haukuwa HURU wala wa HAKI

SADC.jpg
 
Spika mstaafu wa bunge la Malawi, Richard Msowoya sasa anafunguka sawsawa baada ya siku za mwanzo kudanganywa na vyombo vya dola vya serikali tapeli dhalimu ya chama dola kongwe

.Toka maktaba:

Mjumbe wa SADC: Tangu nimefika Tanzania sijapewa mlinzi, Kwangu hicho ni kiashiria kwamba kuelekea Uchaguzi Mkuu kuna amani​

Si kwamba hakuna amani ipo lakini kuna uvunjifu mkubwa sana wa haki na hivi sasa kumetawala sana hofu kwa wananchi.

Najua watakuhendo vizuri kwa sababu ni mgeni lakini tulio ndani tunajua kinachoelendelea. Ila nikupashe habari kwamba hata hiyo siku ya uchaguzi kutafanyika maandamano makubwa sana ya kuikomboa nchi yetu!
=============
Hali ya ulinzi na usalama nchini inaridhisha licha ya kwamba zimebaki siku chache kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 21 na Spika Mstaafu wa Malawi, Richard Msowoya ambaye anaongoza Ujumbe wa Uangalizi wa Uchaguzi wa SADC katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania (SEOM) wakati wa ufunguzi wa ujumbe huo jijini Dar es Salaam.

“Unapoingia nchi husika kama Mkuu wa Ujumbe wa Uchaguzi na ukapewa walinzi ishirini suala hilo huashiria mambo hayako sawa. Lakini tangu nimefika Tanzania sijapewa mlinzi yeyote na hakuna aliyetamka neno lolote baya, wala sijasukumwa wala hakuna aliyenizuia kwenda popote. Kwangu hicho ni kiashiria kwamba kuelekea Uchaguzi Mkuu kuna amani nchini humu,” amesema
Soma zaidi :

GE2025 - Mjumbe wa SADC: Tangu nimefika Tanzania sijapewa mlinzi, Kwangu hicho ni kiashiria kwamba kuelekea Uchaguzi Mkuu kuna amani
 
Back
Top Bottom