Ujumbe wa shukran kwa WanaJamiiForums

Makox

Senior Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
125
Reaction score
163
HABARI WAKUU WANGU WA JAMII FORUM!

Awali ya yote natumia fursa hii KUWASHUKURU sana kwa maoni yenu mliyokuwa mkinipatia tangu nilipoweka post ya kutengenezewa zengwe na mkuu wa shule na mzazi wa mwanafunzi mpaka nikafukuzwa kazi hivyo kuwaomba ushauri wa namna yoyote ile.

Kwa post hii ya Leo NINAWASHUKURU SANA NYOTE Hasa Kwa mawazo na ushauri mlionipa humu na kwa kunipigia Simu kwani baada ya kurejeshwa kazini kesi ilianzishwa upya kama ilivyoagizwa na TSC makao makuu na NILISHAPEWA BARUA YA UMAMUZI WA TUHUMA YANGU ambapo SIKUPATIKANA NA HATIA YOYOTE.

Aidha ninawaombeni muendelee kunipa ushauri wa Nini kifanyike baada ya kushinda kesi
pamoja na kuendelea kuwashauri watu wengine wanaopatwa na changamoto kama yangu na nyingine zote.

Hakika Sina Cha kuwalipa Zaidi ya kuwaombea kwa Mungu wetu aendelee kuwasimamia katika Majukumu yenu ya kila siku.

AMA KWELI JAMII FORUM NI ZAIDI YA FAMILIA YA WAPENDANAO UKIITUMIA VYEMA.

MUNGU AWABARIKI SANA🙏🙏
 
Mshkuru Mungu na ikiwezekana mtolee sadaka kama sehemu ya shukrani zako kwa kuondokana na hiyo changamoto !! Kingine hama hapo maana unaweza tengenezewa tatizo jingine .
 
Mshkuru Mungu na ikiwezekana mtolee sadaka kama sehemu ya shukrani zako kwa kuondokana na hiyo changamoto !! Kingine hama hapo maana unaweza tengenezewa tatizo jingine .
Shukran sana mkuu
 
Ashukuliwe pia Maxence Melo kwa kuanzisha JF na kuruhusu ushauri na watu kubadilishana mawazo na kutatua changamoto.

big up JF all members , muendelee hivi wapendwa.
 
Ashukuliwe pia Maxence Melo kwa kuanzisha JF na kuruhusu ushauri na watu kubadilishana mawazo na kutatua changamoto.

big up JF all members , muendelee hivi wapendwa.
Kweli Wabarikuwe sana, waliwaza kitu kisichoweza kupoteza ubora kamwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…