Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Chonde Waziri Mkuu,
Liambie taifa ukweli wote kuhusu Meremeta zote mbili na kwanini ilikuwa ni lazima kuitengeneza kampuni hiyo. Liambie taifa juu ya wahusika wake na jinsi gani walitajirika kwa kupitia kampuni hiyo; liambie taifa kwanini Jeshi lilijiingiza kwenye biashara ya kuchimba madini kama front ya kile "kingine" walichotaka kufanya; liambie taifa ukweli wote.
Ndiyo, taifa linaweza kutikisika na wengine wanaweza kuishia kutiwa pingu na hasa wale ambao ni makada wenu wazuri wa CCM na maafande wenye nyota. Liambieni taifa ukweli kwani linastahili hivyo kutoka kwa watawala wake. Msipinde maneno sana na msiwatishe watu kwa kusema "usalama wa taifa".
Kama ni suala la usalama wa taifa basi waambieni wenye taifa hilo ni jinsi gani kuchimba madini kwa hasara ya mabilioni kulilinda taifa hilo. Waambieni ni jinsi gani kurithishana hisa za kampuni ya serikali kwenye familia ni kulinda usalama wa taifa; waambieni ni jinsi gani kupeana misamaha ya kodi ya magurudumu n.k kwa Meremeta kulilinda usalama wa taifa; waambieni wenye nchi yao ni kwanini MEREMETA NI SEHEMU YA USALAMA WA TAIFA!
Ndiyo, hata kama hamuwezi kufanya hivyo "hadharani" basi waambieni wawakilishi wa wananchi hao, msiwafiche!
Si mnakumbuka Iranian-Contra? Si mnakumbuka hadi aliyekuwa Waziri wa Ulinzi alikutwa na hatia na wengine 13 maafisa wa serikali ya Marekani kwa kufanya mambo "kwa nia njema" lakini kwa kulificha Bunge la nchi hiyo?
Hicho ndicho serikali imefanya na wabunge ovyo wamekubali ulaghai huo (namaanisha wabunge ovyo ovyo). Wabunge wamekubali serikali iwafiche mambo yanayohusu taifa hili na katika upotofu wa mawazo yao wanampiga mkwara mbunge mwingine yeyote yule kulileta jambo hili bungeni. Hawa ndiio maadui wa usalama wa taifa letu.
Hivyo.. liambieni taifa ukweli mapema. Kama huwezi (kwa kuogopa kusulubiwa) mwache Rais Kikwete alizungumzie kwa uwazi na ukweli..
vinginevyo... vinginevyo... Litaanza kufunuliwa na magazeti mengine na Cheche litachukua msimamo mkali siku ya Ijumaa. Natafuta watu Dodoma ambao wataweza kuchapa nakala hizo za Cheche na kugawa bure kwa Wabunge.
Tunatoka kulalamika, tunaelekea kuhamasika. Kama hawataki kulijadili hadharani, watalijadili vyumbani mwao! Msitulazimishe kwa maamuizi yenu kuwa na misimamo mikali (do not force us by your horrible decisions to become radicalized!).
Hivyo mkuu chonde sana liambieni taifa ukweli, vinginevyo wengine watafanya!