Ujuzi wa chama cha mapinduzi {CCM} kwenye ukingo wa siasa

Ujuzi wa chama cha mapinduzi {CCM} kwenye ukingo wa siasa

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Ni jambo la kawaida sana wanasiasa haswa wa hapa kwetu Tanzania kuhama chama A kwenda B na kadhalika.

Lakini jambo la kujiuliza ni nyakati na namna muhusika anavyoenda kwenye chama husika.
Yapo maswali ya kujiuliza kuhusu aina ya wanasiasa hawa na namna watanzania tunavyopumbazwa na watu wachache kwa kujifanya hawaelewani kumbe wapo vizuri tu.

Je, Mchungaji Msigwa kuhama chama ambako aliaminika kama mwandamizi kunatoa taswira gani kwa maelfu ya watu waliomwamini?

Je,Msigwa alishindwa kwenda chama kingine tofauti na CCM?

Je,ni mbinu za CCM kuwakeep busy watanzania kulingana na yanayoendelea nchini,suala la Bashe na sukari au Mpina na Bunge na mengine mengi?

Kama Amos Makala alivyouita usajili,na usajili huu umefanyika dakika za mwishoni kabisa,je tutegemee nini kwenye upinzani ambapo chama kikubwa kabisa kimetikisika vilivyo huku CCM ikilamba dume.

Ingawaje sijawahi kuukubali upinzani lakini angalau walikuwa wanaikumbusha serikali mambo mengi.

Achaneni na propaganda za kusema Msigwa kashindwa uchaguzi hivyo akahama chama kwa hasira.bali ni mkakati wa muda mrefu ambao settings zake ndiyo kwanza zinaanza kufanya kazi ,na tutashuhudia mengi .

Loading..........49%....
 
Ni jambo la kawaida sana wanasiasa haswa wa hapa kwetu Tanzania kuhama chama A kwenda B na kadhalika.

Lakini jambo la kujiuliza ni nyakati na namna muhusika anavyoenda kwenye chama husika.
Yapo maswali ya kujiuliza kuhusu aina ya wanasiasa hawa na namna watanzania tunavyopumbazwa na watu wachache kwa kujifanya hawaelewani kumbe wapo vizuri tu.

Je, Mchungaji Msigwa kuhama chama ambako aliaminika kama mwandamizi kunatoa taswira gani kwa maelfu ya watu waliomwamini?

Je,Msigwa alishindwa kwenda chama kingine tofauti na CCM?

Je,ni mbinu za CCM kuwakeep busy watanzania kulingana na yanayoendelea nchini,suala la Bashe na sukari au Mpina na Bunge na mengine mengi?

Kama Amos Makala alivyouita usajili,na usajili huu umefanyika dakika za mwishoni kabisa,je tutegemee nini kwenye upinzani ambapo chama kikubwa kabisa kimetikisika vilivyo huku CCM ikilamba dume.

Ingawaje sijawahi kuukubali upinzani lakini angalau walikuwa wanaikumbusha serikali mambo mengi.

Achaneni na propaganda za kusema Msigwa kashindwa uchaguzi hivyo akahama chama kwa hasira.bali ni mkakati wa muda mrefu ambao settings zake ndiyo kwanza zinaanza kufanya kazi ,na tutashuhudia mengi.Mods hapo juu neno ukingo nilimaanisha Ulingo.

Loading..........49%....
Sidhani kama CCM wamelamba Dume zaidi ya ng'anda au galasa
 
Hizi dalili za viongozi wa chama tawala kuanza kujitokeza hadharani ni kujisifia mbinu chafu na za kihaini wanazozitumia kwenye uchaguzi ni dalili mbaya kabisa. Hayo maneno Dalili hizi ambazo vyombo vya ulinzi na usalama hazisemi kama zinatishia uvunjifu wa amani, mwisho wa siku zitalitumbukiza Taifa kwenye umwagikaji mkubwa wa Damu. Tunaona kama masih'ara lakini itajenga mazoea Raia tutaanza kuuawa hadharani kama kuku kwa kisingizio cha kutaka kusababisha taharuki kwenye jamii.
Polisi kamata yeyote bila kujali chama anayetoa matamshi ya kujinadi yeye alisaidia chama chake kuingia madarakani kwa njia haramu! Tulinde AMANI ya Tanzania Kwanza.
 
Back
Top Bottom