Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

yeah..ni mtu asiyekua na upeo mkubwa wa kufikiri ama ni uvivu tu wa kufikiri utamfanya mtu aache mambo ya msingi yanayolitafuna taifa hili na kurudi nyuma kuangalia mambo ya ukabila..haina mantiki kumwacha mtu mwenye sifa na kumpachika asiyekidhi simply kwa kua unataka kuwaridhisha watu fulani fulani kua huna ukabila..
 
tanzania no ukabila
ubaguzi uko kwenye elimu.
hujasoma unategemea kuwa ikulu?
miji yote iliyoendelea ina maduka ya wachaga.
fanya utafiti
 
MMM, I like the way you put your arguments!
Lets not talk of ethnicity while we know the obvious reasons for the cause! The cause is history and we learn from history and create a different future by creating enbaling strategies to the less opportunities groups so that they can also be accommodated in the systems as time come and go!
 

Mbaya zaidi ni kwamba hayo makabila unayosema yana upendeleo ., pia ndo wanapenda kuzaa kwelili kweli. Sasa wanaoa mpaka mikoa ya huko kwenu, na punde wataleta majina yao huko. Je wakizaliwa Wanyakyusa, Wachaga, na Wahaya kwa dada wa Kizigua, Kizaramo au Kimbulu, halafu wakasoma bado uatasema ni ukabila?
Kazana mzee, elimu bila werevu pia sio merit ya kazi! Tuna wanasheria wengi tu waliograduate , lakini tunasikia majina machache tu...Lamwai, Marando, Mawalla nk..... hivyo on top of education, comes merits, experience and ability to execute! Achana na maneno ya ukabila hapa.....
 
Kwa kweli mimi sina shaka na ukweli kwamba hayo makabila yanaongoza kwa kuwa na idadi kubwa hasa wachaga kwenye maeneo yaliyotajwa. Lakini nina maswali madogo tu kwamba inakuwaje watu hawajajiuliza idadi ya wachaga ambao wana baa karibu nchi nzima.....hawajauliza wanaofanya umachinga wachaga ni wangapi? ....madereva wa daladala wachaga ni wangapi?....Wanaochoma mbuzi, mishikaki, wachaga wako wangapi? ...wezi wa magari wachaga ni wangapi? ... wanaomiliki nyumba za kulala wageni wachaga ni wangapi? wenye maduka wachaga ni wangapi? na mengine mengi ....Ukimaliza hapo utajua suala la hawa watu si historia ya elimu tu bali kuna kitu zaidi ya hapo.....aggressive....
 
Mwanakijiji
hongera sana n big up!
huo ndiyo ukweli wenyewe!!!!!
 
Sipendi,
umezungumza ukweli kuhusu aggressve!
but mtu kuwa hivyo ni lazima upate elimu ya kupenda kujaribu kufanya kitu na kuto kata tamaa ya kupata mafanikio!
hiyo elimu ya kuwa na tabia ya kupenda kujaribu na kutokata tamaa ni elimu ambayo mtu huipata kupitia malezi katika familia zao, marafiki, shule n.k
hakuna kulala mpaka kieleweke!!
 
Ninahisi hapa mnaimply kuwa mwenye kigoda anaachia mambo ya ukabila. Ndugu zangu think back kwenye seventies na eighties ikulu, jeshini,nbc, nic na sehemu nyingine nyeti . ilifikia kipindi ukiingia NIC lugha ya taifa haikuwa kiingereza wala kiswahili. Hata vyeo NBC na NIC vingi vilikuwa kwa watu wa kabila fulani. Mambo haya yalikuwa yakitendeka wakati mzee yu hai na mwenye afya.
 
Tukipita kila ofisi serikalini,binafsi,uwiiiii
wachaga tena wako post za juu jamani
inatia moyo lakini ndugu zetu tuwaachie na wengine naona watu wameanza kukasirika najua tofauti za shule ndio sababu basi msisome sana wengine tuingie huko.....wasije wakawalalia bagamoyo dunia mbaya hii..
Wakwe mmenisikia lakini
 
Hii naitazama kwa jicho la 3, ina maana kubwa zaidi ya hivyo uionavyo!
OK..na tuijadili!
 
huu ni ubaguzi wa wazi kabisa haya ndo nyerere alokuwa akipinga usiku na mchana matabaka yasiwepo ya ukabila na udini leo hii tunayaanzisha kidogo kidogo mkuu niwie radhi kama nimekukosea ila sijaona jb au neno sahihi la kujib zaidi ya kusema ni ubaguzi na ninakanusha kauli yako kwamba si kweli wachaga wamejazana kwenye maofisi
 
hapo kwenye RED umeniacha Hoi lol!
 
utafiti wako umetumia kigezo gani?......si kweli kuwa wachagga ni wengi....rudia tena huo utafiti
 
Tupeleke watoto zetu shule jamani. wezetu kule uchagani walipeleka sana watoto wao shule na sasa matunda yanaonekana. Kule Songea shule nyingi zilikuwa seminari, wangoni wengi wameishia kuwa mapadri. Hata Mbeya wamekwenda shule sana ukifika maofisini utakuta akina MWA MWA kibao. Na miaka ya themanini watu wengi sana walipeleka watoto shule za Mbeya kule Lutengano, na nyinginezo, so hata hawa viongozi wetu nao wanachangia sana kuna watu wapo siriaz kusaidia jamii zao lkn, wengine wakija Dar wakipata Nyadhifa baaaasi wanaongeza nyumba ndogo hata kwao hawarudi.
 
Sasa unataka wenzako wasisome wakusubiri wewe uende shule? Hizo si ndizo sera za awamu ya kwanza za kuweka average marks za kupasi kwenda Form ! kwa Wachagga kuwa kubwa kuliko Mikoa mengine. Matokeo yake wale ndio wakawa wana akili zaidi na kupasi zaidi kwenda Form V na hatimae Chuo Kikuu.

Walipobaniwa na Serikali kutokuingia government schools, Wachagga vile vile walijitahidi kujenga private schools ili wale walioachwa wapate fursa ya kwenda Sekondari. Mimi sio Mchaga lakini niliwahi kusikia wakati nilipokuwa Chuo Kikuu mwalimu mmoja akielezea huo mkasa.

Cha msingi ni hayo makabila mengine kujitahidi ili nao wapasi zaidi na kupata fursa zaidi za kwenda Chuo Kikuu.
 
lakini kama wanasoma waacheni wapate ajira ......tatizo hakuna kama makabila mengine tunahitaji mabadiriko basi tuingie darasani na tusome kwa bidii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…