Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ndg yangu na wamasai wasemeje wamechoka kulinda?
Kumbuka tulipata waziri mkuu mmasai....
cha maana kisomo ndio mkombozi.
Bila kisomo kaz za oficn coishu ila ishu ni kaz gan utafanya(responsibilities)
kuna wanapata kaz za ofcn lkn kaz yake ni kufungulia mlango wageni tu..Hapo niaje?
Nenda B.O.T wamakonde wapo...kisomo ndugu,kisomo..Sema ni vizuri unavyo wapigania ilia waelimishe wapunguze ngoma na mimba za utotoni.
 
Cha msingi tukubali kwamba katika kila jamii matabaka yapo hata kwa hao wahaya,wachaga n.k..
Pili kila jamii ina character zake...mfanoa pitia Majeshi yetu utaona watu wa asili flani ni wengi zaidi,Mabenki,Vyama vya michezo, Hata watawala wetu wa local gvnts,VEO's,WEO's n.k Madaktari na wengineo..hata wenye magengeni kule sokoni.
Hii haimaanishi ukabila but ukiweka ukabila wewe ndo utakua mkabila namba 1,kwasababu hiyo hali haikuwapo kabisa bali ninyi wachache mlio na lack of comfidence mnarise hoja hiy
 
Tafiti imefanyika kuwa watanzania 75% wanaoishi England nia kutoka TZ-zanzibar...sio hivyo tu 62% ya watanzania wanaoishi USA ni wa jamii za kihaya na wachaga.
JE MAAFISA WA BALOZI ZA US NA UK NI TRIBALIST?
 
Mtized one,

Kwani kukaa USA ndio unakuwa msomi, kwa sababu hoja ni usomi? Kuna scholarships huwa zinakuja kupitia serikalini au mashirika/taasisis fulani, sasa ikiwa ndugu yangu atanipendekeza/atanipa mimi nipewe hiyo nafasi, na yeye anahusika na mchakato wa kuchuja wanaotakiwa wapewe hiyo scholarship nitashindwa kuipata? Swali lingine, unajua ni watoto wangapi wa wakubwa wanaosoma nje ya nchi, na wanatumia aidha fedha za serikali au za wahisani lakini hawana sifa kupata hizo hela badala yake hizo scholarships walitakiwa wapewe watu wengine wenye sifa zaidi kuliko zao? Nilishawahi kushudia UDSM, kuna Lecturer fulani alipewa scholarships za watu 20 wakasome Sweeden, badala yake alitafuta watu wachache, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na wengine, wale watu walikuwa aidha ni ndugu au watu wa karibu yake, akawaambia wazungu sijaweza kupata watu wenye sifa, nimepata hawa tu wachache wakati kulikuwa na lundo la watu wenye sifa na walikuwa na nia ya kusoma! Kazi ya ubalozi ni kutoa visa baada ya kuwa wameambiwa huyo mtu wanayempa visa anaenda huko kwa ajili ya jambo fulani, usiwahusishe na ukabila, upendeleo, wala ubaguzi, kwanza hata makabila ya Tz hawayajui, ukabila unaweza kufanyika kabla mtu hajaenda kuomba visa au kabla hajafika USA!
 
Uko sawa MM unajua hata wakoloni waliwekeza hasa shule na vinginevyo maeneo hayo ie mbeya,klm na kagera kwa sababu ya resources za maeneo hayo hali kadhalika hali ya hewa pia
Kinyume chake maeneo mengine yakawa inhabited na waarabu ie Lindi,Mtwara.Pwani etc ambao kwao Elimu ni sawa na mmasai na chupi
Naona kama wako wengi maeneo fulani hayo makabila ni kwa kuwa yanadeserve ingawa kuna case chache za apa na pale
 
Uliona wapi mwanao ana njaa ya kufa mtu,umepata chips dume moja kuna mtoto jirani,je utampa wako au wa jirani?
 
asante kwa nukuu hizo hata asiyelewa akisoma nukuu za mwalimu zinajitosheleza. Tukisema enzi za mwalimu haaaaaaaaaa haziishi.

Maskini mwanakijiji!


Maskini mwanakijiji!! Kumbe kweli moto huzaa majivu.Moto wako wa kuchambua issues umekwenda wapi?Mbona sasa umepotea kinachotoka ni majivu tupu tena hata joto hamna. Maskini, kumbe kisu kimegusa mfupa!We should be objective in order to tacle this evil malaise.Mimi siangalii kabila langu ninapokumbana na issue hii ya ukabila.Ukabila upo. Hata Mwalimu katika siku za mwisho za uhai wake alilizungumza alipokaribishwa na mama MONGELA alipokuwa Washington.Sidhani wewe unaelewa kuhusu maswala na hali za ukabila kuliko mwasisi wa Taifa hili.Ili tushinde vita tutambue ukabila upo.Tusiwe kama kisa cha mbuni. Tusiwe wadau wa ukabila.Mahali ambapo hata lugha inayozungumzwa toka reception mpaka ofisi ya CEO ni ya kabila fulani,wote hao wameingia humo kwa bahatitu?!.You are too naive or too alienated.
 
 
 
Nafikiri issue ya ukabila huwa inachanganywa sana watu wanapoizungumzia. Ukabila unatokea pale ambapo mtu asiye na sifa au mwenye sifa anapopatiwa nafasi, kazi kwa kupitia mlango wa nyuma, yaani upendeleo au bila kuwepo na open forum kwa watu wote kuiomba hiyo nafasi. Lakini kama mzee Kimei pale CRDB anatangaza nafasi za kazi na watu wengi wanaomba lakini anaona kuna mchagga ame-qualify zaidi ya waombaji wengine wote. sidhani kama katika hali hiyo CRDB itakuwa imemwajiri huyo jamaa kwa sababu ya kabila lake bali ni kwa sababu ya sifa zake. Ila kuna baadhi ya nafasi zimekuwa zinatolewa kwa watu kwa sababu za kishikaji.. ukabila au hata ubia wa biashara. Kwa namna yeyote ile katika hali hiyo mambo hayaendi sawa na inabidi yarekebishwe. Kama ukiende mlimani ukakuta darasa lina wanafuzi 20 na kati ya hao 12 ni wahaya, au ni wachagga ina maana hao jamaa watapata kazi kwa wingi huo huo na hapo hatuwezi kusema ni ukabila bali ni juhudi yao!!
 
Mi si kati ya hayo makabila yeneye akili Tanzania ila nawaambia hivi wale ambao mmeishiwa confidence kuwa hata mkipata nafasi ya kuwa viongozi watu wenu hamuwajali. Fanyeni uchunguzi hivi mkoa wako una shule ngapi za sekondari kijiji chenu kina wasomi wangapi kijiji chenu kina vipaumbele gani juu ya elimu. Leo hii wanafunzi wa kata yako wanasoma au wanaoana tu na kuvuta bangi. Msilalamike wakati elimu mpaka leo hii mnaipiga teke. Hamuwezi kushindana na hao watu ambao hata leo hii mkipewa pamoja shilingi milioni moja baada ya miaka mitano wewe utakuwa na wake watano na watoto ishirini na mwenzako atakuwa na nyumba tano na magari kibao. U deserve kunyanyapaliwa unless mubadilike. hatuwezi kuwa na jamii amabazo zimeparanganyika hazina misingi ya maendeleo na upendo zinabaki kulalamika kwenye key board. Anayebisha aniambie amesomesha ndugu zake wangapi mpaka anabonyeza kibodi amabo siku moja wataomba kazi huko TRA BOT nk na watapata kwa merit za Competence?
 
Siamini kama uko justified kutoa conclusions zako kuhusu makabila haya kwa kutumia hiyo experience yako ndogo ya kuhisi (labda na kusikia) na ulipokuwa chuo. Kwanza si kwamba kama ulikuwa A student basi utaweza ku deliver kazini. Elimu yetu yatufunza "kukariri". Huwezi fanya kazi kwa kutumia elimu "uliyokariri", hivyo usitegemee A student wajae ikulu au TRA na kwingineko, maana kule hatukariri hesabu, jiografia n.k. ila tunafanya kazi. Kule hawaangalii kama ulipata A, hizo A nenda nazo chuo kafundishie watu kukariri. Robert Kiyosaki anazungumzia kuhusu kusaidiana katika masomo ambapo wewe wasema ni cheating, lakini ukienda kwenye ajira hutakuwa ukifanya kazi bila ushirikiano na wenzako. Ndio maana A student wengi huwa hawawezi kuwa na team work maana kwao ushirikiano ni cheating, na hii huwafanya dellivery zao kuwa poor. I was an A student, A ya point 7 na point 3, na GPA kubwa chuoni, ila naamini sana katika ushirikiano darasani.
 
Kaka upo sahihi kabisa! c ukabila na udin umejaa hapo! Me huwa nakasirika sana pale Kanisani tulipotakiwa kuleta vyeti kwa ajili ya ajira ktk sekta ya serikali! na kuna wa2 walikimbiilia kuforge vyeti na yule jamaa hakavichukua na sasa wanaajira! Tatizo ni kwamba wanatutia aibu ktk utendaji kazi wao! hili me linanichukiza sana wadau
 

Bigup.............................
 
Jamani tusome,hakuna njia za mkato kwenye ajira za kisasa. Mi nipo kabila dogo tu lakini namshukuru Mungu kwamba kichwa changu na vyeti vyangu ndio huwa vinanisaidia kupata ajira sehemu ninazotaka. Sijawahi kuulizwa kabila kwenye interview,huwa sijuani na mkubwa yeyote na kazi huwa napata. Makabila hayo matatu mliyoyataja kweli yapo serious kufuatilia elimu za watoto wao,niliwahi kufanya kazi Mbeya,nilikuwa mpangaji wa mzee mmoja anaitwa Kibona,kuna wakati alikosa ada ya mtoto wake aliekuwa chuo. Aliuza sehemu ya shamba lake ili mtoto akalipe ada!. Kuna makabila kwenye hali hiyo huwa wanamwambia mtoto rudi nyumbani fungua biashara kisha oa mke muanze maisha! Tusiwe waongeaji sana wa tanzania. Jitahdi u meet qualification for the job,the rest will be taken care.
 
Tukatae tusikatae ukabila upo sana na sidhani kama unaweza kuisha kilahisi kwa sababu unafanyika katika sekta kibao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…