Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali


Mwongo peupe wewe usifurahishe baraza wakati wanaume wanafikiri,ofisi gani hiyo kama wewe ni mkweli uiseme hapa tukafanye utafiti,maana ndio kazi yetu wana JF.
 
kaka kweli nimekukubali.umeipangia vizuri sana.tunatakiwa tushukuru MUNGU walau hawa ndugu zetu walibaatika kwenda shule.sasa huyu aliyetoa mada atupe facts ya hii thread yake laa sivyo huyu ni mpuuzi tuu.
 
Umeliona hilo ni vema .Tushauri tufanye nini tuondokane na hiyo hali.
Angalizo; Ushauri wako usituhamishe kutoka hao unaodai na kwenda kundi lingine kwa kisingizio waliachwa nyuma. Tusije wapa hao unaowafikiria tukaishia kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi. Kwa vile wataanza na kasi ya ajabu ili wafikie kilele ktk muda mfupi.
 

Kama we ni A student basi hamna haja yakusoma ili kupata A duh kwahiyo ni wazi kuwa wewe ulikuwa mtu wakudesa na kuingia na nondo kwenye exams kama unasema eti kusaidia ni vizuri kwenye paper.
Pili ni vizuri kusoma maelezo ya mtu vizuri,jamaa hakumanisha kwamba siyo vizuri kusaidiana bali anasema wakati wa examz yaani in examination. Hii inanipa mashaka na hizo A7,A3..and G.P.A kubwa kama kweli ni halali..!?
 
People mnapoteza muda kuongea kuhusu ukabila kwenye ajira in being a dog! or slavery, ajira ni utumwa......
kwanini usijiajiri mwenyewe......! learn to be a master and not a dog. Fanya utafiti mtaani kwako ni kabila gani asilimia kubwa wengi wao wamejiajiri wenyewe kisha utapata jibu ni kabila gani linabaguliwa zaidi kwenye ajira. we uko ukwereni/ uzaramoni lakini maduka mengi mtaani ni ya wachagga au wapemba .....? acheni upuuzi kazi yenu kucheza bao alafu mnataka mpewe ajira serikalini........kwanini msiseme wachagga, wapemba na wakinga wanapendelewa kwenye kumiliki biashara ya mduka kariakoo na kumiliki biashara tz....NAZANI ALIYE ANDIKA MAADA ANGEMAANISHA
WACHAGGA, WAPEMBA NA WAKINGA WANAPENDELEWA KWENYE KUMILIKI MADUKA NA BIASHARA TANZANIA.
walaau angeonyesha kuwa ni mpenda maendeleo na mzalendo wa kweli.
 

Who the hell is "Robert Kiyosaki"?

Kama unasema kuiba na kuibia mitihani ni team work sasa nimeelewa unavyofikiria, halafu umesema umefundishwa kukariri na sio kuelewa, nimekuelewa pia na endelea kukariri, na nashindwa kupata picha uhusiano uliopo kati ya A zako point 7 na 3. Ningekuwa nina nafasi na kama ungekuwa tayari tuonane, ningefurahi sana kuona unavyofanya kazi zako.

Narudia tena, niliyoyaongea ni ukweli, kama hujanielewa endelea kusoma tena na tena mwisho utaelewa naamanisha nini.
 

Nimependa point yako ya kujiajiri na kuajiri wengine. Ni hilo tu.
 

Alexism, you got it! Amenipa wasiwasi jamaa kama hata chuo amefika na hata kama hizo A, 3, na 7 anazo, kwa sababu nahofia hata kuibia angeweza kukosea, labda kama alikopi, maana hawezi kutofautisha kati ya team work, kuiba na kuibia.

Ukabila upo, na sio kwamba ni kwa makabila hayo matatu tu! Mtu anaweza kufanya ukabila hata kama anatoka kabila dogo. Watu wakisema kuna ukabila hawamaanishi kila Mhaya, Mchagga na Mnyakyusa ni mkabila, ila wanaashiria ni kwa kiasi kikubwa, kwani wapo amabao sio wakabila pia.

Hapa siongelei swala la qualifications, naongelea hili: mtu aidha hana vigezo, au au vigezo vyake ni vya chini kuliko vya wengine lakini anapewa nafasi.

Kama wewe, mkeo, watoto wako, mjomba, babu yako, bibi yako, shemeji yako, mkeo mdogo, shangazi, hawara yako, mjomba wako mnafanya kazi ofisi moja lakini mna vigezo vyote vinavyotakiwa na mmepitia hatua zinazotakiwa kupata hizo kazi, mimi wala sina shida na hilo, na wala sitasema nyie ni wakabila.

Ndani ya Tz kila aina ya uchafu unawezekana, wizi, ukabila, ufisadi, unyang'anyi, uporaji, rushwa, utapeli........ and the list goes.
 

Kwa hiyo wewe unaamini makabila mengine hawajasoma kabisa isipokuwa yale matatu tu? Halafu unaamini kwamba kwingine hakuna shule isipokuwa ni mikoa mitatu tu? Halafu unaamini nyie tu ndio mliosomesha ndugu zenu? Halafu unaamini ni makabila mengine ndio yanayooa wake wengi tu na sio lako, halafu unamaanisha pia makabila yote isipokuwa yale matatu? Halafu unawaambia watu wanabonyeza kibodi hujua mafanikio yao, hujui wamefanya mangapi tena labda kukupita wewe! kwa sababu hata kama wana uwezo hawawezi kusomesha jamii nzima! Halafu hujui kwamba watu wengi toka makabila madogo kama mnavyoyaita wana qualifications za kufanya kazi sio tu BOT na TRA, bali hata kwenye mashirika/makampuni makubwa duniani kama UN, NASA, Google, IMF, World Bank, nk na hizo ajira hawajapata kwa njia za longolongo? Halafu unaamini kila mtu toka makabila hayo matatu amesoma?

Halafu jiulize huo usomi wanautumiaje, kuiendeleza nchi au kuiibia na kuidhulumu?

Kwa mfano Andrew Chenge alisoma Havard (sisemi anatoka hayo makabila), among the most respected universities in the world! Kama scandal zake zile ni za kweli, usomi wake utakuwa unaisadia nchi? Sasa weka wengine wenye scandals toka makabila hayo matatu au kabila lako, namaanisha scandal za wizi, rushwa, ufisadi, uuaji, umalaya nk halafu tuambie jinsi usomi wao unavyochangia kwenye maendeleo ya nchi.
 

Sio wewe pekee unayetoka kabila dogo ndio umesoma , yapo maelfu ya watu na huenda wanakuzidi kila kitu, kuanzia elimu, utendaji, uwajibikaji na hata mafanikio mengine, lakini hiyo hoja yako haimaanishi kwamba hakuna ukabila!

Ndani ya Tz kila kitu kinawezekana.
 
Samvulachole zingatia usemi wa akina Mao Tse Tung an wenzake kuwa "NO RESEARCH NO RIGHT TO TALK". Wachaga; Wahaya na Wanyakyusa wamesoma sana tu ndiyo maana kila mahali wamepata ajira kuliko makabila mengine. Yaani we acha tu. Hata shoe shiners wengi ni wachaga bila kuwasahau mafundi saa pia. Kutembeza bidhaa mkononi wanaongoza wasiosoma yaani chingas, waha etc. Tafadhali chukua tahadhari kubwa sana kabla ya kukurupuka na masuala ya ukabila usije aibika buree ndugu yangu uliyetoka kimasomaso kama msomi kwenye kabila lako.
 
jamani tusome na tuweze kutetea taalumu zetu pia tusaidie ndg zetu wasome kwa wng.si kulalama tu huku unachangia harusi na umaarufu baa na ndg yako wanakosa elimu
 

Umesahauu sio ukabila pia kuna

  • UJINSIA waajiriwa wengi ni wanaume
  • UDINI- Probably labda wakiristu ni wengi huko
  • UUMRI- wengi wenye vyeo ni walio above 50
Trabist, genidst, ageist, religionist..... .. endleeeni na ist nyingine


So hope hapo utapata jibu Lisllo la kisiasa. maana ukisema ukabila tu unaweza ukaja na nadharia na longolongo amabyo haitakusaidia kukupta jibu zuri la tatizo hilo kwma wako ni tatuzo. Ukiangali issue issue kwa upana wake nutajua ukweli na nini kifanyike au nini wengine wanatakiwa kufanya.

 
Jamani kuhusu ukabila upo sana kuna IDARA kama MAHAKAMA kuna ukabila sana hapa watu wanaothaminiwa ni WAHAYA,sisi wengine ni Third Class human being,ubaguzi si wakificho tumechoka,na waziri wa sheria na katiba analijua hilo
 
Na sisg wangoni tumejaa idara gani wajameni..? Naomba mnijuze mwenzenu hata sijui.?
 
Jamani kuhusu ukabila upo sana kuna IDARA kama MAHAKAMA kuna ukabila sana hapa watu wanaothaminiwa ni WAHAYA,sisi wengine ni Third Class human being,ubaguzi si wakificho tumechoka,na waziri wa sheria na katiba analijua hilo

poleni sana kuhusu ukabila hapo mahakama,kuna jamaa yangu kanieleza kuwa kuna ukweli,nasikia chief accountant mr Tiibuza anawapendelea WAHAYA tu,pia ni mdhaifu sana kwa wadada
 
Pamoja na kukubaliana na mwanakijiji naomba niongezee hapohapo, kwamba hata sasa katika madarasa tunayoyasoma utakuta makabila hayo ndo yaliyo na uchungu na shule, kama we ni mwanafunzi au hata uliwahi kupita shule ushindani wa kitaaluma utakuta ni katika makabila yanayotoka kanda ya ziwa, kasikazini na mbeya. Hawa wenzetu wengine, wao cha muhimu ni kumaliza shule suala la (scintillation perffomance) au GPA kubwa kwao ni ya nini? Nimalizie kwa kusema akhsante saana MM kwa kutuka flashback ya "ukabila".
 
Kumbe mswahili was wrong on this...
Mswahili said:
Mama Mkapa alipokuwa Ikulu alifanya kila linalowezekana kuhakikisha anaingiza wachagga kila kona, na hata deal za rada na ndege ni wafanyabiashara wa kichagga wana mikono yao.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…