Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

..huyo jamaa aliyetoa hilo tangazo hajui maana ya alichokisema "tanzanian of asian origin",bora hiyo wangeifanya katika ku-short list na si wazi hivyo!

..kesho hiyo duka ikipigwa mawe na kuvunjwa vioo watamlaumu nani?

..wamejiweka naked for racial hatred!
 
..huyo jamaa aliyetoa hilo tangazo hajui maana ya alichokisema "tanzanian of asian origin",bora hiyo wangeifanya katika ku-short list na si wazi hivyo!

..kesho hiyo duka ikipigwa mawe na kuvunjwa vioo watamlaumu nani?

..wamejiweka naked for racial hatred!

Sasa mpaka hapo ndio ujue kwamba Watanzania wanapolalamika kwamba Wahindi wana matatizo ya ubaguzi tuelewe somo!
Hapo wameonyesha wazi kabisa jinsi walivyo!
True colour.
 
Unajua kuna mtu kaanzisha thread ya kuwabagua watanzania wenye asili ya kiasia
Halafu kuna watu wanamzungumzia Mghufuri kama mkabila vile vile

sijui ukweli uko wapi
 
Hoja ya ukabila ni nzito ni nzito na inavuta hisia kali katika jamii,ni vizuri ikajadiliwa bila hiyana.
Tuwe wakweli, kinachotokea leo kwa majirani zetu ni funzo kwetu.Tusijidanganye hii ni Afrika,matatizo ya umaskini kila mara ktk Afrika hutafutiwa mchawi,na siku zote mchawi ni ni kabila fulani.
Tusimsingizie Mwalimu,aliliona hilo.Mazingira yaliyokuwwepo wakati ule siyo ya leo,makabila yaliyokuwa hayakusoma leo yamesoma.
Mfano mzuri tuchukuwe TRA wakati fulani kulifanyika kozi Bagamoyo ktk jumla ya wafanyakazi 45 waliohudhuria kozi hiyo 35 wakikuwa kabila moja,siyo makabila matatu bali moja!!Tuelewe kwamba ktk nchi hii jumla ya wasomi wote wa makabila mengine ni ndogo kuliko kabila hilo?!Au tuseme nini, je si kwamba watu walikosa haya na sensitivity?
Kwenye miaka hiyo inayotolewa mifano na kisingizio kwamba MWL aliliona na kwamba haliepukiki MWL kwa makusudi kabisa alitenga
nafasi kwa makabila yaliyokuwa nyuma kielimu hata marks za ushindi ktk mikoa fulani zilikuwa chini kuliko mikoa fulani mingine.Tuseme MWL alianzisha ubaguzi?
Leo hii kabila fulani ktk nchi fulani lilipewa nafasi za kazi, nafasi za kiuchumi na utawala dhidi ya makabila mengine.Wananchi walipoamua kubadili serikali yao kwa nia njema kabisa,hasa kwa sababu za kiuchumi zaidi kabila hilo liliona ni ubaguzi kama mnavyouita nyinyi.Kila mkoa wafanya biashara,wafanyakazi,wakulima ni wao matokeo yake tunayasikia.Wananchi wanapokataa serikali yao imefika mahali inaonekana wanalikataa kabila fulani.Tusiende huko kwa visingizio vya ubaguziTufanye jitihada za makusudi kurekebisha kasoro hii mbaya ktk Taifa."Kufichaficha maradhi kilio kitatuumbua"
Ktk awamu ya tatu ya uongozi mawaziri karibu 10 walitokea mkoa fulani je hiyo ilikuwa fair?
Tuache kucheza na moto wa ukabila.Siku ukiwaka tusisingizie ubaguzi bali tuwe wakweli tutakuwa tulikosa hekima.
 
Masuala ya ukabila yalikuwepo NBC enzi za Amon sekela ilikuwa watu wa Nyanda za juu kusini wanakula kwa ulaini sana.
na Posta na simu nako kuliingia ukabila wakati fulani.
 
Masuala ya ukabila yalikuwepo NBC enzi za Amon sekela ilikuwa watu wa Nyanda za juu kusini wanakula kwa ulaini sana.
na Posta na simu nako kuliingia ukabila wakati fulani.
Amon Nsekela nasiyo Sekela.
 
Nafurahi sana kujiunga na JF, kisa cha kujiunga hiki hivi hawa wazungu pori(Makaburu) kwa nini wanatunyanyasa wakati hata elimu tumewashinda, acheni hiyo ya ukabila ikulu. chekini na hizi za UDHUNGU kwenye makampuni
 
Kwenye ufisadi mikubwa yote inayoibuliwa hivi sasa, wahusika wengi wanatokea mikoa ya Kagera, Mara - in short, Kanda ya Ziwa.

Hii inaashiria nini:
a) Ni wasanii wazuri kwa mambo ya kugushi;
b) Wana ulinzi mahsusi kutoka vyombo vya usalama - wengi kutokana na ukabila wamo humo;
c) Well-connected in high Govt. offices;
d) U-homeboy syndrome.
 
samvulechole... hakuna hoja ambayo ni ngeni hapa.. madai ya makabila hayo kupendelewa hayakuanza leo! tangu mara tu baada ya uhuru kulikuwa na tuhuma hizo hizo.. so.. there is nothing there..! Hata hivyo hatari unayoweza kuleta siyo ukabila bali ubaguzi, kuwa kama mtu anatoka kwenye makabila hayo basi asipewe nafasi fulani kwa vile watu fulani wanadhani kuna ukabila! Nitakupa mfano, kuna wanasheria watatu wote ni maprofesa... kuna Prof. Mwakalindile (Sheria, uzoefu miaka 30), Prof. Mtimba (mmakua, uzoefu miaka 10, sheria), na Prof. Chanda (Mzigua, sheria uzoefu miaka 5). Assuming maeneo ya fani zao ni sawa, ceteris paribus Rais anataka kumteua mshauri wa kisheria.. nani apewe kwa haki? Wengi watasema prof. Mwakalindile! Sasa kwa kufanya hivyo hata hivyo kuna wanyakyusa wawili tayari hapo ikulu ambao wameshapata nafasi zao, je tumnyime Mwakalindile kwa vile itaonesha ukabila?

Kabla hatujafikia hapo pa kudai ukabila tujiulize: "Kwanini inaonekana kuna wasomi wengi wa makabila hayo matatu Wachaga, Wahaya, na Wanyakyusa"? Je, tupunguze wanafunzi wanaotoka kwenye makabila hayo na kuwapa nafasi watu wa makabila mengine ili kuleta uwiano (parity)? Je tukiamua kufanya hivyo hatutakuwa tunaanza ubaguzi wa kikabila?

Tarehe 9 Disemba 1968 Nyerere alitumia siku ya Jamhuri kuzungumzia "Vitu ambavyo ni lazima Tuvisahihishe", vitu ambavyo baada ya uhuru havikwenda vilivyotarajiwa. Alizungumzia ukabila; kwanza alisema hivi:

"the man who talks about tribalism being practised without having any evidence for his statement is often a man who wants to stir up tribalism. Even if that is not his purpose, the result can be just the same. People will begin to think that there is tribalism, and, once people begin to think in these terms, then tribalism has begun to enter tinto our society"

Kuhusu Wahaya, Wanyakyusa, na Wachaga kupata nafasi nyingi katika serikali, Mwalimu alisema hivi miaka karibu 30 iliyopita:

"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes".

Akaongeza pia,

"Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs which require higher education, the answer is very obvious. They were the ones who received higher education during colonial times. I'd say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the Parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and at the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren't any, or there are one or two. This is the truth"

kwa umahiri wake wa maneno JKN akatoboa ukweli huu

"Anyone who refuses to accept a very obvious truth like this, and says that the reason is tribalism, must provide us with the evidence for his statement. If he cannot provide any evidence, we must conclude either that he is a fool, or that he is strirring up tribalism deliberately. He is the sort of (a) person who begs work on a tribal basis, and when he is refused because he does not have the capabilities, he pretends he was refused on tribal grounds."

Akasema pia ni jukumu la serikali kusaidia sehemu ambazo bado ziko nyuma kielimu. Na alimaliza kwa kusema:

".. if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusayoung man were refused work simply because of his tribe - when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualifications - then we would be practising a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid ANYTHING WHICH COULD BRING OUR COUNTRY INTO THIS KIND OF DISGRACE" (emphasis mine)
(From: Uhuru na Maendeleo pp 76,77)

so what say you?
baba upo juuu usipimer maana lazima tukubali shule ndiyo inakuweka madarakani. nelson mandela wakati amechukua madaraka africa kusini aliwambia hivi wanachi wake, Elimu yako ndiyo itakayo mtoa mzungu madarakani na ndiyo maana weusi huko sauzi wanasoma na tunaona wazungu wanaachia ngazi. papa umenigusa sana mwanakijiji
 
Ukabila Tanzania upo at a latent position yaani huwezi kuuona waziwazi. Mtu anaweza kujiwekea mazingira hayo pindi anapokuwa na madaraka makubwa na huweza kutengeneza vijinafasi ambavyo vitawawezesha nduguze angalau kupata kajiugali. Kwa hiyo mtu kwa kutumia madaraka yake aweza kuhalalisha visivyo halali. Au hukumbuki ya Richmond. Na ukabila huu ndio mbaya zaidi afadhali ya Kenya wanajuana kabisaa yule mkikuyu ,mluhya,mluo au mkamba hapa Tanzania tunayo makabila mengi sana kwa hiyo inakuwa ngumu lakini ukabila upo. Jiulize mbona chuo kikuu kuna vyama vya ukabila tena kweny wasomi waliobobea ambao wangeipigia kelele hii ishu. Na ukiangalia msingi wake ni kuwekeana mazingira na watu waliopo kwenye system ,Channel za ajira na vitu kama hivyo.
 
Mimi kama mmoja wa hayo makabila, nasikitika sana sijafaidi na huo ukabila wenyewe, nimeshaomba kazi sehemu zote hizo, na wanaochukuliwa ni wa makabila mengine kabisa, sababu kubwa ni kuwa wazazi wao au ndugu zao wako "well connected" hapa 'know who' ndio inaangaliwa siyo kabila.

Kinachowasumbua kenya ni umasikini. Matajiri wanazidi kutajirika na masikini wanazidi kufilisika, vizazi hadi vizazi wakirithishana.
sie ndio tunaenda huko, kuanzia kwny siasa hadi kwny ajira za kitaalamu.
inasikitisha sana, lakini ndio hivyo.
Kwa maoni yangu ni kuwa kuna ubaguzi wa kila namna, kifedha, kikabila, kidini, kijinsia, kirangi, kiumri, kimaumbile, kisura, kisiasa, kielimu nk.
ukibahatika kimojawapo kikakusukuma mbele unafurahi, kikikukwamisha unajisikia vibaya sana.
Solution is to make a deliberate effort that the resulting feeling does not sweep you. You may feel hate, jelous, on top of the world, or anything else.
i do not have the solution to the world, but for myself, I make sure my decisions are based on the issue at hand, if there are to choices left, then i choose the more vulnerable one.
Lakini katika kujadili hoja hii niliwahi kusikia kuwa watu wanachagua mtu wanaemjua au mwenyekujulikana kwani na jamaa zake kwani watanzania siku hizi hatuaminiki. Bora mtoto wa mjomba atakuogopa au mtoto wa rafiki yako. Kwa upande mmoja pia naafiki uchaguzi wa aina hii.
Niliwahi pia kuulizwa, "kama kuna vijana wawili wote wako qualified mmoja ni ndugu yako mwingine humjui ila CV na interview wote poa tu, utamchukua yupi?"
Mimi nitamchukua ambae nina background yake
 
Kwenye ufisadi mikubwa yote inayoibuliwa hivi sasa, wahusika wengi wanatokea mikoa ya Kagera, Mara - in short, Kanda ya Ziwa.

Hii inaashiria nini:
a) Ni wasanii wazuri kwa mambo ya kugushi;
b) Wana ulinzi mahsusi kutoka vyombo vya usalama - wengi kutokana na ukabila wamo humo;
c) Well-connected in high Govt. offices;
d) U-homeboy syndrome.



Huu ukabila kabila umeenea kila mahali, usishangae hata hapa JF ukabila ukawa unanyemelea, lets see kwani ukweli haufichiki.
 
Kuna na huyu mtoto wa Rais mstaafu, aliekuwa hataki kusoma, ghafla kasoma sheria ya kimarekani lakini kaajiriwa TZ, Hii ni ukabila au??
 
Kuna na huyu mtoto wa Rais mstaafu, aliekuwa hataki kusoma, ghafla kasoma sheria ya kimarekani lakini kaajiriwa TZ, Hii ni ukabila au??

Mwenzangu, mtoto wa Mr clean au Mzee Ruksa? mtaje tu openly na wengine tujue anaitwa na na kaajiriwa wapi
 
Kuna na huyu mtoto wa Rais mstaafu, aliekuwa hataki kusoma, ghafla kasoma sheria ya kimarekani lakini kaajiriwa TZ, Hii ni ukabila au??

At JF We dare talk openly, weka wazi jina la kijana huyo.
 
bado hujawa wazi Haika. Nico Toto Tundu ni cartoon character au?
 
bado hujawa wazi Haika. Nico Toto Tundu ni cartoon character au?

Nilisoma sehemu wanamtaja kuwa Nicholaus Mkapa, sasa ameajiriwa ofisi ya DPP. Huyu Nico Mkapa amemwoa Mtoto wa Joseph Mbuna. Joseph Mbuna ni wakili wa Chenge. Joseph Mbuna, Mkapa, Yona na Chenge wote wana share Kiwira Mining...hapo chachaa
 
Daa!! kama huku kwetu wala hatutajwi kabisa japo mwl katoka huku, ninashindwa kuelewa hebu ni kwa nini mwl hakuyajenga mashule mengi huku kwetu? Mkoa mzima miaka ya 70-80 shule za sec zimekuwa tatu tu jamani, Sina haja ya kumlaumu Mwl kwa sasa, ila na ninyi (wahaya, wanyakyusa na wachaga) basi msibebane huko maofisini kwani siku tukitaka kubanana tusijetukaonana wabaya.Taifa hili ni letu sote hivyo twende sawa,
 
Back
Top Bottom