Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Kweli kabisa Ndugu Isaya,Nchi hii ni ya kwetu sote kwani hata sisi wamakonde nao tupo,ingawaji ktk mkoa mzima wa Mtwara kuna shule za Advanced Level zisizo zidi 5,sasa sijui tutafika lini huko,ila najipa moyo naamini tutafika angalau kuwa karibu na makabila mengine
 
Najua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali

Je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya Wachagga,Wanyakyusa na wahaya?

mimi nilikuwa siamini mpaka pale NILIPO ambiwa kuwa kuna UKABILA wa hali ya juuu kule Ikulu NA vile vile namba mbili kwa UKABILA ni TRA je kuna ukweli katika haya?

Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?




-JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY

Ni kweli hata mimi nilikuwa siamini ila nilikuwa nikisikia ,kama wtu ni wafuatiliaji tujaribu kwa wizara ya ujenzi hususani kitengo cha TANROAD. Kuanzia ngazi ya juu mpaka mikoani ni kabila la wahaya tu na ukiwa mwigine wa tofaut utahamishwa.
Watanzania tujitahidi tuwe tunaajiri watu ambao ni TECHNICALLY KNOW HOW na si TECHNICALLY KNOW WHO.
AKSANTE.
 
Huo si ukabila ila ni nimna ya utawala wa kitemi wa kurthishana madaraka,maana urishanaji wa madaraka unatoke kwa jamii zilizo endelea sana kielimu au zilizokuwa nyuma sana kielimu.
Je,tanzania iko wapi.
 
Ni kwamba wao wako wengi maofisini wanao elewana Lugha kwa hiyo akisema jamani hii ni ya nyumbani si kumoja Basi wanafanya kama wanasaidiana ila ndo kuila serekali kiaina
 
Ni kweli hata mimi nilikuwa siamini ila nilikuwa nikisikia ,kama wtu ni wafuatiliaji tujaribu kwa wizara ya ujenzi hususani kitengo cha TANROAD. Kuanzia ngazi ya juu mpaka mikoani ni kabila la wahaya tu na ukiwa mwigine wa tofaut utahamishwa.
Watanzania tujitahidi tuwe tunaajiri watu ambao ni TECHNICALLY KNOW HOW na si TECHNICALLY KNOW WHO.
AKSANTE.

Uzoefu wangu unanionyesha kuwa ukabila kwenye taasisi na mashirika ya umma huwa ni wa muda tu. Unakuwepo wakati aliyeuleta anapoendelea kushika madaraka ya juu kwenye Taasisi/Shirika husika.Mifano ipo mingi tu na hapa nitataja michache tu:
1.Bima ya Mwaikambo sio hii ya leo;
2.Kuna bwana mmoja wa Kichagga alikuwa relwe kabla ya Mboma alipoondoka mambo yalibadilika haraka;
3.Jeshi sasa hivi sio la Wakurya;
4.Dawasco ya sasa sio kama Dawasa ya Mutalemwa (1991-2003).
Tuwe makini tu na zile ofisi kuu tatu za Nchi yetu. Hili CCM wameliweza sana.
 
..vipi kuhusu mahakama ya rufaa.

..majaji wanawake wako 4 na 3 kati yao wanatoka kabila moja.

..kuna Jaji Ausebia Munuo, Nathalia Kimaro, Engera Kileo.
 
Ni kweli hata mimi nilikuwa siamini ila nilikuwa nikisikia ,kama wtu ni wafuatiliaji tujaribu kwa wizara ya ujenzi hususani kitengo cha TANROAD. Kuanzia ngazi ya juu mpaka mikoani ni kabila la wahaya tu na ukiwa mwigine wa tofaut utahamishwa.
Watanzania tujitahidi tuwe tunaajiri watu ambao ni TECHNICALLY KNOW HOW na si TECHNICALLY KNOW WHO.
AKSANTE.

Lugwa...Naomba utupe Uthibitisho...mie nilikutana na Rafiki yangu mmoja tumemaliza nae UDSM, nikamwambia kwanini haombi kazi TANROADs...wakati wao wanazo projects nyingi...akasema huko wamejaaa Wakaskazini...na hata Sub-contracts wanapewa wao..Hapo MZee Lugwa umetaja Wahaya...kidogo nahitaji ufafanuzi...Wahusika Serikalini ni vema Mkaanza kuboresha pia hali hii...
Utashangaa kuwaona vijana waliomaliza Civil wamekaa wanafundisha Matuition Mchikichini, Magomeni..au Mikoani kutafuta pesa za Kujikimu..wakati Jamaa zetu wamejazana Tanroads...wakijipangia per deim $300
 
Lugwa...Naomba utupe Uthibitisho...mie nilikutana na Rafiki yangu mmoja tumemaliza nae UDSM, nikamwambia kwanini haombi kazi TANROADs...wakati wao wanazo projects nyingi...akasema huko wamejaaa Wakaskazini...na hata Sub-contracts wanapewa wao..Hapo MZee Lugwa umetaja Wahaya...kidogo nahitaji ufafanuzi...Wahusika Serikalini ni vema Mkaanza kuboresha pia hali hii...
Utashangaa kuwaona vijana waliomaliza Civil wamekaa wanafundisha Matuition Mchikichini, Magomeni..au Mikoani kutafuta pesa za Kujikimu..wakati Jamaa zetu wamejazana Tanroads...wakijipangia per deim $300

Hilo la ukabila nakubaliana na wewe kwa kweli suala hili lisipoangaliwa upya nhi hii wanaonufaika nayo ni watu wa kaskazini wale tunaotoka mikoa iliyobaki tumebaki kuwa ni wasindikizaji tu
 
..vipi kuhusu mahakama ya rufaa.

..majaji wanawake wako 4 na 3 kati yao wanatoka kabila moja.

..kuna Jaji Ausebia Munuo, Nathalia Kimaro, Engera Kileo.

Hawa waheshimiwa majaji nawafahamu, wawili ni kabila la WAURU na mmoja MACHAME (msiseme wachaga, kabila hilo halipo nimeishi Kilimanjaro na kuyasoma makabila haya kiundani). Mmojawao mwanae alikuwa mwanafunzi wangu katika darasa langu la kwanza la A-level nililofundisha, sijui yuko wapi siku hizi lakini alifaulu vizuri sana form 6. Je hawa kinamama wameteuliwa ujaji kwa sababu ya kabila lao? Kuna Jaji Mkuu au Rais au mamlaka ya uteuzi kutoka kabila lao? Nani mwenye ushahidi au angalau tetesi tu kuwa uteuzi wa hawa kinamama unatokana na ukabila?

Mimi napinga sana ukabila na ubaguzi wa aina yoyote, lakini nashauri tusianze kusingizia kila kitu ukabila, mwishowe vitaanza kuturudisha nyuma. Hivi inapotokea hitaji la kuwa na majaji wapya na ikatokea wenye sifa hizo ni hao kinamama basi wasiteuliwe kwa kuwa ni Wauru? Na kule Kilimanjaro wauru hutengwa na kudharauliwa na wanaojiita "wachaga wenzao", sasa maskini ya Mungu sijui hawa kinamama walipata wapi "mkabila" mwenzao wa kuwapigia debe! Hebu watu chapeni kazi acheni uzandiki, jaribuni kutofautisha kati ya wanaopata sifa kwa kustahiki na wanaopendelewa, sio basi kila anayepata uteuzi fulani kwa kuwa na wenzie wa kabila hilo wamepata basi kuna ukabila! Wapo kinamama wenye uwezo wa hali ya juu wa kiutendaji na wasio na masikhara katika kazi zao, tuwaache wapate nafasi wanazostahili bila kuwazushia viwingu vya ukabila kutokana na wivu tu wa kijinga! Wapo pia wanaume wenye uwezo, uzalendo, bidii katika kazi zao, tuwaache wapate haki yao ya kupanda cheo na kupata teuzi mbalimbali. Na kama kuna pahala penye ushahidi au hata mashaka ya dhahiri ya ukabila, viwekwe dhahiri vijadiliwe, lakini sio kusingizia kila anayefanikiwa.

Hii ya kuwasema hawa waheshimiwa kinamama majaji, japokuwa wametajwa tu, imeniudhi kabisa, maana naona haiingii hata kidogo kwenye classification ya ukabila. Acheni wivu wa kijinga!
 
Kithuku,

..asante kwa majibu yako hapo juu. posting yangu ilikuwa na nia ya kuchokoza mjadala. kama utachunguza michango yangu ktk thread hii basi utaelewa kwamba it is not my belief kwamba Majaji wale wa Mahakama ya Rufaa wamefikia ngazi hiyo kwa kutumia ukabila.

..nafikiri kuendelea kulalamikia ukabila muda wote huu ni dalili ya uvivu. labda nitoe mifano kidogo: timu yetu ya taifa ya riadha imejaa Wabarabaig na Wambulu; JWTZ kumejaa wenyeji wa Musoma; kuna Wapemba wengi ktk biashara ya maduka.

..swali la kujiuliza ni kama mazingira niliyoyaelezea hapo juu yamesabibishwa na ukabila peke yake, au kuna mambo mengine ya msingi yamejificha.
 
Kithuku,

..asante kwa majibu yako hapo juu. posting yangu ilikuwa na nia ya kuchokoza mjadala. kama utachunguza michango yangu ktk thread hii basi utaelewa kwamba it is not my belief kwamba Majaji wale wa Mahakama ya Rufaa wamefikia ngazi hiyo kwa kutumia ukabila.

..nafikiri kuendelea kulalamikia ukabila muda wote huu ni dalili ya uvivu. labda nitoe mifano kidogo: timu yetu ya taifa ya riadha imejaa Wabarabaig na Wambulu; JWTZ kumejaa wenyeji wa Musoma; kuna Wapemba wengi ktk biashara ya maduka.

..swali la kujiuliza ni kama mazingira niliyoyaelezea hapo juu yamesabibishwa na ukabila peke yake, au kuna mambo mengine ya msingi yamejificha.

Nimekuelewa mkuu, nakushukuru tuko pamoja.
 
Ni ukweli usiopingika kwamba aina yoyote ya ubaguzi haikubaliki.
Pia ni ubaguzi kumyima mtu nafasi eti sababu dini au kabila lake wapo wengi katika hiyo idara.
ILA kinachofanyika ni hao wenye dini au makabila husika kupigiana "pande" na taarifa ya hizo nafasi kupeana kwenye vikao vyao. hivyo hata huo uzoefu wasio kwenye system hawaupati.
Hivyo basi, mchakato mzima lazima uwe wazi kwa watu wote.
Hakuna makali yasiyo na ncha, lazima ifikie mwisho ila tuombe Mungu uwe mwisho usio wa chuki na vita.
 
Lakini tusilalamike sana kuhusu hawa wachaga kwani Mungu kawajalia vipaji vingi sana.
Kwanza utafikiri hii inayoitwa pesa amezaliwa nayo, Pili huwa wanatreak nyingi sana za kusaka pesa. Lakini pia hata madarasani wanajitahidi sana pamoja na kwamba wote waume na wakike wakikaa hata ikulu wanafanya biashara.
Tukumbuke hapa dar wamejazanaaa utafikiri wao ndo wazaramo.Kwanini wasipewe hizo sector nyeti za fweeeza kama TRA,IKULU,MAMBO YA NJE YA NCHI,NA MIPAMGO NA UCHUMI?? BADO MALI ASILI NA UTALII< ndiyo tutawajua akina masawe na bwashe.
 
Ni kweli kabisa wala si uongo, lakini hiyo inatokana na serikali yenyewe kuyafumbia macho mambo haya,wao wanachokijua ni kutafuta pesa na kuwaibia wananchi tu
 
Alichosema JK Nyerere kiko sahihi mpaka leo. Hicho ni kuhusu ukabila na usomi. Nakumbuka wakati nakwenda kidato cha tano SHYCOM waka 1980, tulikuwa wanfunzi 120tuliochaguliwa nchi nzima kuingia hapo. Lakini wanafunzi 60 (yaani nusu ya hao) walikuwa wenyeji wa Kilimajaro. Hivi leo tunapiga kelele kuhusu sekondari za kata. Kwa Kilimajaro hiyo ni historia kwao kwa kuwa kila kata ilikuwa na shule zaidi ya moja. Sisi tunachunga ng'ombe, halafu tunalalamikia upendeleo. Mtanzania yeyote aliyesoma vema ana nafasi nzuri tu ya kuwa mkuu mahali. Hata hapo TRA panapolalamikiwa, sio kweli wengi ni Wachaga. Haya ni majungu tu ya watu kutotaka kwenda shule. Sisi tusiokuwa Wachaga tusome kwa bidii na tujitahidi kuwapeleka watoto wetu shule. Pia tujitahidi kuleta wale watoto wa ndugu zetu kutoka vijijini pasipo na elimu bora ama kwa kuwasaidia hukohuko walipo au kutoa mawazo kwa ndugu zetu kuhusu umuhimu wa elimu bora.
Je, tunakumbuka habari kuwa kuna wafugaji waliokuwa na ng'ombe zaidi ya 5000 bonde la Ihefu lakini hawawapeleki watoto wao shule??? Kalaga baho.
 
samvulechole... hakuna hoja ambayo ni ngeni hapa.. madai ya makabila hayo kupendelewa hayakuanza leo! tangu mara tu baada ya uhuru kulikuwa na tuhuma hizo hizo.. so.. there is nothing there..! Hata hivyo hatari unayoweza kuleta siyo ukabila bali ubaguzi, kuwa kama mtu anatoka kwenye makabila hayo basi asipewe nafasi fulani kwa vile watu fulani wanadhani kuna ukabila! Nitakupa mfano, kuna wanasheria watatu wote ni maprofesa... kuna Prof. Mwakalindile (Sheria, uzoefu miaka 30), Prof. Mtimba (mmakua, uzoefu miaka 10, sheria), na Prof. Chanda (Mzigua, sheria uzoefu miaka 5). Assuming maeneo ya fani zao ni sawa, ceteris paribus Rais anataka kumteua mshauri wa kisheria.. nani apewe kwa haki? Wengi watasema prof. Mwakalindile! Sasa kwa kufanya hivyo hata hivyo kuna wanyakyusa wawili tayari hapo ikulu ambao wameshapata nafasi zao, je tumnyime Mwakalindile kwa vile itaonesha ukabila?

Kabla hatujafikia hapo pa kudai ukabila tujiulize: "Kwanini inaonekana kuna wasomi wengi wa makabila hayo matatu Wachaga, Wahaya, na Wanyakyusa"? Je, tupunguze wanafunzi wanaotoka kwenye makabila hayo na kuwapa nafasi watu wa makabila mengine ili kuleta uwiano (parity)? Je tukiamua kufanya hivyo hatutakuwa tunaanza ubaguzi wa kikabila?

Tarehe 9 Disemba 1968 Nyerere alitumia siku ya Jamhuri kuzungumzia "Vitu ambavyo ni lazima Tuvisahihishe", vitu ambavyo baada ya uhuru havikwenda vilivyotarajiwa. Alizungumzia ukabila; kwanza alisema hivi:

"the man who talks about tribalism being practised without having any evidence for his statement is often a man who wants to stir up tribalism. Even if that is not his purpose, the result can be just the same. People will begin to think that there is tribalism, and, once people begin to think in these terms, then tribalism has begun to enter tinto our society"

Kuhusu Wahaya, Wanyakyusa, na Wachaga kupata nafasi nyingi katika serikali, Mwalimu alisema hivi miaka karibu 30 iliyopita:

"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes".

Akaongeza pia,

"Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs which require higher education, the answer is very obvious. They were the ones who received higher education during colonial times. I'd say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the Parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and at the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren't any, or there are one or two. This is the truth"

kwa umahiri wake wa maneno JKN akatoboa ukweli huu

"Anyone who refuses to accept a very obvious truth like this, and says that the reason is tribalism, must provide us with the evidence for his statement. If he cannot provide any evidence, we must conclude either that he is a fool, or that he is strirring up tribalism deliberately. He is the sort of (a) person who begs work on a tribal basis, and when he is refused because he does not have the capabilities, he pretends he was refused on tribal grounds."

Akasema pia ni jukumu la serikali kusaidia sehemu ambazo bado ziko nyuma kielimu. Na alimaliza kwa kusema:

".. if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusayoung man were refused work simply because of his tribe - when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualifications - then we would be practising a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid ANYTHING WHICH COULD BRING OUR COUNTRY INTO THIS KIND OF DISGRACE" (emphasis mine)
(From: Uhuru na Maendeleo pp 76,77)

so what say you?
Mwanakijiji,

Nakuheshimu sana kwa utoaji wa hoja nzito nzito. Pamoja na ufafanuzi wako mzuri kuhusu ukabila na mfano, ambao nao pia ni mzuri sana, nadhani bado kuna haja ya kupigana vita ya kuondoa ukabila kwenye masuala ya ajira. It's true kwamba ukianza kuzungumzia ukabila pasipo kujua unaweza ukawa unauibua na kuuchochea. Lakini nadhani ni vizuri uongozi wa juu ukaanza kufuatilia kwa usiri sana maeneo nyeti yanayolalamikiwa. Lengo likiwa ni kujaribu kuangalia kwa nini kabila fulani lime-dominate kwenye eneo fulani. Kama watumishi wengi waliajiriwa kwa merrits zao basi, utizamwe mfumo mzima wa ajira tangu kutangazwa hadi usaili. Suala la kusema wanyakyusa, wachanga, wahaya wamesoma sana lina mantiki lakini lisigeuzwe kuwa kichaka cha "wakubwa" wenye ugonjwa wa kupendelea ndugu na jamaa wa kabila zao. Mbona uteuzi wa baraza la mawazili lina-consider kauwiano fulani ka mikoa??????? Isitoshe, as time goes, makabila yote including wafugaji yatasheheni wasomi tu.

Best regards,

Goodluck
 
Hii Mada Nzuri Sana Na Ni Nzuri Kwa Sababu Tunaijadili Sasa Hivi. Ila Mimi Naona Kadiri Siku Zinavyoenda Mambo Yatabadilika Na Hili Suala La Ukabila Litapungua Tuu, Kwa Sababu Watu Wanaoa Na Kuolewa Na Makabila Tofauti, Kwa Mfano Kaka Yangu Kaoa Mchaga, Mimi Nimeoa Muhaya Na Kaka Yangu Ninayemfuata Ana Mpango Wa Kuoa Mtu Wa Kanda Ya Ziwa, Kwa Hiyo Watoto Wetu Watakuwa Tofauti Kidogo Na Ndio Maana Siku Hizi Hatuulizani Makabila Tukikutana, Labda Wengine Wanaweza Kujulikana Kwa Majina Yao. Ila Suala La Ukabila Sio Kwamba Halipo Kabisaa Hata Kama Tunachukulia Kwamba Makabila Fulani Yamesoma Kwa Mfano Wakati Mzee Mwaikambo (rip) Alivyokuwa Bima Wanyakyusa Walikuwa Wako Wengi Sana. Na Pia Kuna Wakati Ma-top Wa Tra Wengi Walikuwa Wachaga, Sasa Sijui Hapo Ilikuwa Ni Kwa Sababu Wamesoma (hayo Makabila) Au Ni Kwa Sababu Ya Ukabila ? Ila Kaka Mwanakijiji Shikamoo! Respect Bro!
 
Lusajo,Goodluck,Congo,

..huo mfano aliotoa Congo unaweza kujibu baadhi ya maswali yanayotutatiza.

..yeye anadai in the 80s, asilimia 50% ya wanafunzi wa shycom walikuwa toka kilimanjaro.

..kama ni hivyo inawezekana kabisa uwiano huohuo ukajitokeza kwa wanafunzi wanaosomea B.Com, na zaidi ktk kada nzima ya wahasibu/wachumi nchini.

..hata bila kuwa na kiongozi anayeendekeza ukabila, inawezekana kabisa idadi kubwa ya wahasibu ktk mashirika mbalimbali ikawa toka Kilimanjaro.

..idadi ya wasomi toka makabila mengine inapaswa kuongezeka. nafasi za kazi za maana nazo zinapaswa kuongeza. bila hivyo tutaendelea kulalamikia suala hili.

NB:

..vipi kuhusu kujuana?

..schoolmate wangu amenisaidia kumpatia ajira bwana mdogo wangu. huyo mate wangu hatutoki kabila moja.

..naamini kwa sasa hivi kazi nyingi zinapatikana kwa kujuana kuliko ukabila.
 
Back
Top Bottom