Wewe ni Mzungu? Mbona umeumia kihivyo mkuu? Nisamehe kwa bure ila ukweli unabaki kuwa sasa hivi hamna jeuri tena Vi-China vimewashika pabaya!!!Kama hawana nguvu kwa nini unawaruhusu wakuamulie? chuki hiyo ni ya nini wamekufanya nini wewe? Usianze kutukana mvua eti ndiyo maana hukuvuna wakati hukulima!
Pamoja na kufanya uchaguzi kwa amani lakini dosari kubwa ktk uchaguzi wa Kenya ni ukabila. wananchi wengi wamepiga kura kwa kuangalia makabila yao badala ya sera za wagombea. Uhuru Kenyatta anaongoza kwa kura hadi sasa kwa kuwa tu anatoka kabila la Wakikuyu ambao ni wengi kuliko kabila jingine.
Raila Odinga kabila lake la Wajaluo si kubwa kuweza kumuunga mkono na kushinda. Mzee Jommo Kenyatta ambaye anadaiwa kupalilia ukabila nchini humo kwa kuwabeba Wakikuyu aliwahi kunukuliwa akisema "Jaluo Jinga Jeusi haiwezi ongoza Kenya". Na hicho ndicho kinachomcost Odinga. KILA LA HERI KENYA.
JK ni nani/nini?
kwa lipi labda ?
Mkuu nimesalimu amri! Ukiona kimya ujue ninaomboleza he he hee! Lakini haikuwa kazi rahisi, kwani hiyo 50.03% ilikuwa ni Mungu wake tu, bila kura 4,100 za Uhuru uchaguzi ungerudiwa. Hongera zake na zenu!Mkuu mbona umesepa jumla wala hutaki tena kuchungulia chungulia humu? Uliahidi utanitafuta!!!
Tunaendelea kumkandamiza uncle wako ile mbaya. Sasa hivi kapigwa gap la kama kura laki 7 hivi sijui atazikomboaje hizo?
UHURU ATOSHA!!
Mkuu nimesalimu amri! Ukiona kimya ujue ninaomboleza he he hee! Lakini haikuwa kazi rahisi, kwani hiyo 50.03% ilikuwa ni Mungu wake tu, bila kura 4,100 za Uhuru uchaguzi ungerudiwa. Hongera zake na zenu!
..Pamoja na kufanya uchaguzi kwa amani lakini dosari kubwa ktk uchaguzi wa Kenya ni ukabila. wananchi wengi wamepiga kura kwa kuangalia makabila yao badala ya sera za wagombea.
Uhuru Kenyatta anaongoza kwa kura hadi sasa kwa kuwa tu anatoka kabila la Wakikuyu ambao ni wengi kuliko kabila jingine. Raila Odinga kabila lake la Wajaluo si kubwa kuweza kumuunga mkono na kushinda.
Mzee Jommo Kenyatta ambaye anadaiwa kupalilia ukabila nchini humo kwa kuwabeba Wakikuyu aliwahi kunukuliwa akisema "Jaluo Jinga Jeusi haiwezi ongoza Kenya"
Na hicho ndicho kinachomcost Odinga. KILA LA HERI KENYA.
Kama ni ivo ukwelikitugani, Magufuli afuata nini Kenya kwenye uzinduzi wa kampeni za Raila?Mshabihiano upo ndugu Sigma. Hapa Tanzania we are fighting against the Status Quo (and of course,this is what is killing our country) under CCM. Likewise for Kenyans, the CORD is against the Kikuyu Status Quo..! So to say, CCM = KIKUYU (wanadhani wanahaki miliki ya kutawala,ikibidi kufanya umafioso ,
CDM = CORD, Fighting for change.!!
Magufuri na Agwambo ni Comrades. Hata Magufuri alipofiwa Baba yake Mzazi, Agwambo alikuja Kule Chato na Mawaziri wenzake toka Kenya kwenye Msiba..so u can imagine.!!Kama ni ivo ukwelikitugani, Magufuli afuata nini Kenya kwenye uzinduzi wa kampeni za Raila?
kama kawa kama dawa. Odinga lazima awe rais. marafiki washajumlisha kura na kukuta kashinda kwa asilimia 62.
Unathibitisha vp kuwa Odinga hakubebwa na suala la ukabila?
Wewe ni Mzungu? Mbona umeumia kihivyo mkuu? Nisamehe kwa bure ila ukweli unabaki kuwa sasa hivi hamna jeuri tena Vi-China vimewashika pabaya!!!
Ureno sasa hivi vijana wanakimbilia Msumbiji na Angola, hiyo taarifa unayo? Uchumi uko hoi bin taaban!!
hakika hata odinga kabebwa na kura za waluo na kabila la kalonzo kama vile kenyatta alivyobebwa na kura za wakikuyu, wakalenjini, wameru na kabila za aina hiyo zikiwa topped up na za hapa na pale. inaelekea pia waliompigia kura kenyatta walijitokeza kwa wingi sana kuliko wale wa kina odinga. kinachosikitisha kwa baadhi ya makabila kenya KUJIAPIZA kutawala daima na kamwe kutoruhusu kabila lingine kutawala hata iwe kwa kuzusha mapigano - kiapo cha msituni.
kama kenya ilikuwa na wakati mzuri wa kuachana na sera ya UKABILA ilikuwa wakati mzee Kenyatta akikaribia kung'atuka na kumwachia mwanasiasa machachari na mwenye akili sana TOM MBOYA ambaye alithubutu kuwa mbunge ndani ya wakikuyu enzi zile za giza kabisa za ukabila. lakini Tom aliuwawa (assassinated) mchana kweupe jumamosi moja ya 1969. na wakati huo gumzo lilikuwa huyu Tom alikuwa dangerous kwani angeteka nyoyo za wakenya akawa rais - cheo ambacho ni "teule" kwa kabila fulani - na tetesi ambazo sio rasmi ni mauwaji yaliongozwa na mzee mwenyewe akipata ushauri wa karibuu toka kwa mzungu mweusi Charles.
Kenyata Jnr, rais mteule kama kenya imo moyoni mwake ana wakati mzuri wa kuileta kenya pamoja na ambayo itaendelea kuuvunja ukabila maana kizazi kijacho cha kenya sio lazima kuwa kitakuwa na mambo ya kipuuzi haya ya ukabila. ni rahisi kwa kenyata kuanza kuuondosha ukabila kama vile nyerere akiwa mkristo aliweza taifisha shule za wakristo ili kuleta utaifa ambapo rais mwislamu ingemuia vigumu kudiriki kufanya kitu kama hicho.