Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama hakuna sababu za msingi kwa nini yacheleweshwe jamani watu wanataka kuona uhesabuji wa kura ulio makini na siyo uchakachuaji
Eti viongozi wa tume? mbona sasa hii kadhia nyingine inataka kuzuka ina maana wamezidiwa na usingizi wameenda kulala ili asubuhi waje kuendelea na zoezi ama?ndio nini hiki....
Kuna uwezekano mkubwa kuwa CORD wameshashindwa huu uchaguzi. Hili tamko lao linaloendelea sasa hivi wanaongea kama chama cha upinzani tayari. Same stories tulizozoe kuzisikia bongo.
Kiujumla ni kwamba cord kama wameshayakataa matokeo.
wanaomba explanation wanasema "otherwise results of this election will be in serious doubt". Na kuna sehemu kura zinaendleea kupingwa wakati ni after midnight.
Inaonekana CORD walimchukulia poa Uhuru, wanakuja kushituka tayari kura zilishapigwa, kuna dalili ya CORD kushindwa maana gap linazidi kuongezeka, sa hivi kuna gap la karibia laki 3.
Mbona watangazaji wanasifia kwamba turnout ilikuwa overwhelming? mimi nikajua itakuwa ni zaidi ya 95%Halau turnout siyo kubwa kama ilivyotegemewa. Kuna sehemu turnout ni only 4% nyingine 0%. Kwahiyo hapa inaonekana kura zote hazitazidi milion 5, inagwa waliojiandikisha ni mil. 14.
Inaonekana CORD walimchukulia poa Uhuru, wanakuja kushituka tayari kura zilishapigwa, kuna dalili ya CORD kushindwa maana gap linazidi kuongezeka, sa hivi kuna gap la karibia laki 3.
Mbona watangazaji wanasifia kwamba turnout ilikuwa overwhelming? mimi nikajua itakuwa ni zaidi ya 95%
Kwa ujumla, uchaguzi wa Kenya umegubikwa na ukabila na hili si la kumtupia lawama mgombea mmoja tu. Odinga naye yumo humo, katika mkumbo huo huo. Anagombea si tu kwa sababu anadhani anaweza kuiongoza Kenya, bali pia kwa sababu anadhani ni wakati wa Wajaluo kuongoza. Bado huo ni ukabila na huo ndio pia unaomfanya naye asipate kura.
Chama chake kimetoa tamko baya sana muda mchache uliopita. Japokuwa mambo waliyoyaongea mengine yana mashiko, nadhani kwa ajili ya amani na usalama usingekuwa wakati wa kutoa tamko kama lile. Lile tamko laweza kuwachochea watu wakaanza machafuko.
Siasa za ukabila zinaletwa sana Tanzania na Serikali ya CCM. Ngoja waendelee kuupalilia nchini kwetu tuone nasi watatufikisha wapi. Tumwombe Mungu, siasa za sasa zimekuwa chai ya moto, ukinywa lazima upulize. Zinachoma
40mins kuhakiki tu, hata kama ningekuwa mimi ningeweza kuondoka, ila kwa jinsi Raila alivyokuwa anajiamini nadhan alikuwa hajajiandaa kushindwa, kama matokeo yakiendelea hivi kuna hatari ya machafuko kutokea tena, inabidi hapa wakenya wawe watulivu na wavumilivu kupita kiasi la sivyo watachichanjana tena.Matokeo yanaonyesha tofauti. Sehemu zenye turn out kubwa zilikuwa ni around 25%. Mtu mmoja kumverify kupiga kura ilikuwa inachukua mpaka masaa mawili. Yule aliyetumia 40min ndiye aliyetumia muda mfupi, so watu wengi wameondoka bila kupiga kura.
Kwa ujumla, uchaguzi wa Kenya umegubikwa na ukabila na hili si la kumtupia lawama mgombea mmoja tu. Odinga naye yumo humo, katika mkumbo huo huo. Anagombea si tu kwa sababu anadhani anaweza kuiongoza Kenya, bali pia kwa sababu anadhani ni wakati wa Wajaluo kuongoza. Bado huo ni ukabila na huo ndio pia unaomfanya naye asipate kura.
Chama chake kimetoa tamko baya sana muda mchache uliopita. Japokuwa mambo waliyoyaongea mengine yana mashiko, nadhani kwa ajili ya amani na usalama usingekuwa wakati wa kutoa tamko kama lile. Lile tamko laweza kuwachochea watu wakaanza machafuko.
40mins kuhakiki tu, hata kama ningekuwa mimi ningeweza kuondoka, ila kwa jinsi Raila alivyokuwa anajiamini nadhan alikuwa hajajiandaa kushindwa, kama matokeo yakiendelea hivi kuna hatari ya machafuko kutokea tena, inabidi hapa wakenya wawe watulivu na wavumilivu kupita kiasi la sivyo watachichanjana tena.
Nimejiuliza hivi baada ya lile tamko iwapo cord watashinda uchaguzi watakuwa tayari kuyakubali matokeo maana yatari wameshaonyesha kutokuwa tayari kuyakubali!!!
In my view nadhani cord wameshapata taarifa kuwa wameshindwa na wanaanza kutengeneza mazingira ya kupatiwa nafasi kwenye government...
Uko sahihi kamanda. Lile tamko linaonyesha ni kwa sababu wanaonekana kushindwa. Japokuwa sikubaliani na utaratibu wa kurusha matokeo, ikiwa kuna maeneo bado kura zinapigwa, sikubaliani na namna ambavyo CORD wametoa malalamiko yao kwa kuonyesha kama wamehujumiwa. Ikiwa mpaka sasa wameshakufa watu zaidi ya 22, kuna uwezekano kuwa tamko lile linaweza kuwachochea wapuuzi wachache na kuanza kupigana mapanga tena