Ukaguzi wa CAG usiozingatiwa ni wa nini?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Demokrasia inahusu wengi kupewa. Hata hivyo ni busara zaidi walio sahihi kupewa:


Kaguzi za CAG zinazofanyika miaka nenda rudi bila hatua zozote za maana kuchukuliwa ni za nini?

Your browser is not able to display this video.

Ya nini kupoteza pesa kwenye kuibiwa na kwenye kaguzi zisizozingatiwa?

Kwa mwendo huu wanaoona ofisi ya CAG ifutwe, wana hoja.

Wasikilizwe!
 
Ingekuwa Kenya raila angeitisha maandamano ya kutaka mamlaka za uwajibishaji hapa kwetu uteuzi zichukue hatua dhidi ya wezi wa kodi za wananchi.

Bahati mbaya kwa sasa hatuna mpinzani wa kuweza kufanya ya Raila. Hivi ni nini mbadala wa upinzani hapa kwetu kinachoweza kuchukua nafasi ya upinzani kushinikiza serikali kuçhuku hatua?
 
Fuatilieni kwa makini bungeni, hao wawakilishi wenu ndio wenye jukumu la kufanyia kazi ripoti ya CAG na kuipa maazimio serikali. Msiwalaumu wasiohusika.
 
Kumbe na wewe iko moyoni? Tuko pamoja. Siasa siyo uadui.
Bwashee wanaogeuza Siasa Kuwa Uadui ndio wanatucheleweshea maendeleo

Binafsi huwa napenda kumpa changamoto Freeman kwa sababu namuelewa kitambo Sana kabla ya hizi Siasa, ni mtu muungwana!
 

Nani alijua Ruto au Gachagua ni wapole na wenye kutaka maridhiano hivi?

Your browser is not able to display this video.


Ama kweli Raila baba lao.

Kwetu wenzetu wanang'aka tuandamane wenyewe.

Kwamba asubuhi moja ya neema, kila mtu atoke kivyake vyake nyumbani kwake kwenda barabarani.

Bila shaka bila kichwa wala miguu.
 
Bwashee wanaogeuza Siasa Kuwa Uadui ndio wanatucheleweshea maendeleo

Binafsi huwa napenda kumpa changamoto Freeman kwa sababu namuelewa kitambo Sana kabla ya hizi Siasa, ni mtu muungwana!

Tatizo lenu wengine ni vipenyo huwala wengine mumo kwa mumo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…