zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Hizi ripoti huwa zinaenda bungeni na waliotajwa huitwa na kuhojiwa kwa kutoa maelezo ya ziada baada ya hapo bunge linakuja na maazimio. Sasa enzi zile PAC Iko chini ya Zitto mawaziri kibao walikua wanang'olewa na hakukuwa na maandamano.Ingekuwa Kenya raila angeitisha maandamano ya kutaka mamlaka za uwajibishaji hapa kwetu uteuzi zichukue hatua dhidi ya wezi wa kodi za wananchi.
Bahati mbaya kwa sasa hatuna mpinzani wa kuweza kufanya ya Raila.
Hivi ni nini mbadala wa upinzani hapa kwetu kinachoweza kuchukua nafasi ya upinzani kushinikiza serikali kuçhuku hatua?
Enzi hizo ripoti ya PAC ikisomwa wote tunakaa kwenye redio au Tv zetu maana tunajua Kuna vichwa vitaliwa. Ila tokea bunge la Ndugai tumeona PAC Haina makali, upinzani nao wakamweka Kaboyoka ambaye sio radical, so tokea hapo ikawa wezi wanasalimika tu Hadi leo.
So nadhani issue ni kubana wabunge tuliowachagua kama watakua mabubu basi imekula kwetu maana tuliwaingiza kwa kishindo!!