Ukaguzi wa Leseni za biashara maduka ya mtaani

DISPLEI

Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
73
Reaction score
47
Hili suala la ukaguzi wa maduka kubaini wasio na lesseni, vyeti vya afya, chombo cha kuwekea uchafu n.k. ni deal na maofisa wa serikali wananemeekea huko.

Anakuja mtu mmoja huyo huyo afisa biashara wa leseni. Huyo huyo TRA, afisa afya. Mwenye duka anaitwa kwa mtendaji. Akifika anatishiwa kuwekwa ndani na kupelekwa mahakamani. Baadaye anatakiwa kutoa 100,000 au zaidi kutegemeana na ukubwa wa duka ili ahachiwe.

Anaambiwa akate afya na kupewa risiti halali ya 5,000 lakini hela anatoa 10,000.


Hii katika serikali sikivu halijakaa sawa vyombo husika vilitazame watu wanateseka na kuliwa mitaji yao.
 
Awamu hii wajanja wanapiga hela balaa, maana wajinga ni wengi mno, ukiwatisha kuwa umetumwa na serikali basi watadondosha mkwanja wa maana.

Kweli penye woga mwingi huwa kuna ujinga mwingi pia.
 
Ukitaka kufanya biashara kwa furaha ww fuata tu sheria japo vitu ni vingi vya kufanya na vinapunguza faida kwa % kubwa sana. Usipofuata sheria watakuja watu wa serikali na fine zao sawa na mtaji wako na ukitaka kuwanyamazisha wanataka nusu fine.
 
Yaani sasa hivi sina mpango wa kufungua biashara youote tz kwa kweli maana huo mtitririko hapana
 
Nimekwambia napenda kulelewa soma uelewe nimekwambia sina mpango wa kuja kufungua niashara tanzania bora nifunhue huku niliko nje ya nchi hovyo unakurupuka tu kujibu
Kwa maadishi hayo labda upo nnje kwenu
 
TRA ni watu tofauti na afisa biashara na afisa wa afya. Hao watu wote hua wanatembelea maduka , TRA wanakagua mapato waliyo kukadiria kama umelipa while afisa biashara anakagua leseni ya biashara kama unayo au kama ime expire. Kimsingi akija mtu dukani akataka kukukagua vyote kwa pamoja fanya hivi; 1. Muombe uangalie kitambulisho cha halmashauri anayo tokea, kama hana usimpe pesa kirahisi rahis utaibiwa 2. Jitahidi unapoenda halmashauri kukata leseni chukua mawasiliano wa afisa biashara husika ili anapo tokea mtu anakagua mambo ya TRA , leseni,afya, sijui mazingira kwa pamoja basi muulize afisa biashara wako atakupa maelekezo kuhusu ukaguzi wa siku hiyo. T.O .....
 
Nimekwambia napenda kulelewa soma uelewe nimekwambia sina mpango wa kuja kufungua niashara tanzania bora nifunhue huku niliko nje ya nchi hovyo unakurupuka tu kujibu
Usijibizane na wendawazimu hao wachache wa huku tz, kama uko huko nakushauri baki huko huko na uwekeze huko huko... huku uje kama kusalimia tu ...
hamna mtu mwenye akili timamu atataka kufungua business huku saivi
 
Unaishi nae?!

Namshangaa hivi vitoto vilivyoijua jamii forum juzi nakununua vitecto mimi nasema vingine anakimbilia kujibu unapenda kulelewa ndio maana baba jesca anawanyoosha safi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…