Ukaguzi wa Vyeti kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari.

Ukaguzi wa Vyeti kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari.

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
7,745
Reaction score
11,267
Katika kudhihirisha ule usemi wa "Huwezi kushindana na Serikali" tangu jana kuna zoezi la kuhakiki vyeti (academic) kwa walimu wa shule za msingi na sekondari za hapa jijini Mwanza. Wakaguzi wametoka Dar sijuhi wizara ya Elimu au Tamisemi, vyeti vinavyokaguliwa ni vile vya kidato cha Nnne na chuo. Cheti kinakaguliwa na maofisa wanne kwa kupokezana na wakikitilia mashaka wanatumia tochi maalum au wanacheki kwenye kompyuta na wasiporidhika ndiyo hivyo wanabaki na cheti chako. Zoezi limeanza na kata mbili za jiji na litaendelea kwenye kata zingine. Jamani hapa ni vilio vitupu si mnajua vile vyeti vyetu mangumashi:A S cry:

My Take:
Yaana Serikali ilisubiri wagome ndio iwageuzie kibao? mbona watu tuna Phd zetu feki na hatukaguliwi au mnasubiri tudai haki zetu. Watumishi hewa mmeshindwa veti ndio mtaweza?

Wana JF walisema maneno haya kitambo: Walimu wkigoma imekula kwao! Serikali sikivu hiyooooooooooooooooo!

SOURCE: Mimi mwenyewe nipo Hapa jiji najifanya malimu.
 
Mbona Hili ni suala Jema Kabisa!! Lilitakiwa Lifanyike Tanzania Nzima!! Unafikiri Hawa polisi wanaouwa Raia wangekaguliwa Vyeti Vyao Kuna ambaye Atapona kwa hilo? Wengi ni Vyeti Vya ndugu zao na marehemu ambao wengine walishatutoka!!
 
leo hii kila mtanzania akikaguliwa vyeti vyao basi kutakua hakuna mawaziri hakuna wabunge na hakuna ma CEOs
 
Back
Top Bottom