Ukahaba Wetu Unatuponza!

Ukahaba Wetu Unatuponza!

Mada hii inatangulia vitu vyote!.. Shukran Rev. Kishoka, shukran sana ningeomba tu kwa kutumia maelezo yako Utungwe waraka wa Watanzania kwa serikali yetu kuwafahamisha kero za wananchi kwani kwa mara ya kwanza kabisa naona hoja nzito na pengine ndicho Kirusi cha maradhi yetu ya Ufisadi..​
 
China leo inasheherekea miaka 60 ya ukomunisti. They have made necessary changes and reforms without allowing to lose their identity.I agree, they still have a long way to go. But one thing is very clear that the economy is growing together with middle class size of citizens among chinese people.
If they have more people with bigger purchasing power and right education keep in mind the large population, they will have power to dominate the future econimic and political trends of the world.
Down the road, almost 50 years after independence, our beloved country is in a rush to return back to where it had already moved.
Hii habari ya kutembelea ulimwengu mzima kulialia tunataka wawekezaji ni idea ya nani? Hivi hatuwezi kujifunza kuendesha mambo yetu kwa mafanikio mpaka tuombe ombe kama watoto yatima? Mbona China wameweza! Mbona Botswana wameweza! Sisi tunashindwa nini?
Duuh!! Kwa mtindo huu tutajaza matapeli na wala si wawekezaji.
Kila kukicha unakuja msemo mpya..mara usipowajibika ole wako, mara uwazi na ukweli, mara kasi mpya mara kilimo kwanza.eeh
 
Issue ya kilimo namna ya kuishughulikia ipo wazi ni ubinafsi tu wa viongozi wetu ambao all the time wanaangalia whats in for them and not whats in for the country as a whole. Inajulikana wazi kuwa kuna sehemu mbali mbali ambazo ni bora kwa vilimo vya tofauti,sehemu ambazo ni bora kwa mahindi,kahawa,mpunga,viazi,matunda nk Na hata kilimo cha mauwa. Lakini kwasababu ni wazi kuwa hatuwezi kutegemea mvua peke yake,ni wazi kwamba kilimo cha umwagiliaji ndio solution,zana bora za kilimo pamoja na vitu kama mbolea nk. Serikali ikiamua kulivalia njuga suala la kilimo basi basi ni lazima waje na plan mithili ya ile ya Marshall.

Inahitaji fedha pia ambazo zinatumika kununua vipodozi ie kujitangaza kama walivyofanya CNN ili kuvutia aina nyingine ya mabwana(watalii) na huku mapato ya investment hizo yakifujwa.

Mfumo mzima wa kilimo ni lazima ufanyiwe kazi,kuanzia kwenye uzalishaji hadi kuuza mazao ya ziada mara baada ya kuwa processed. Pia kuna mazao ya biashara ama cash crops,hiyo ni idara nyingine ya kilimo inayohitaji iwe segmented na kupewa priority yake.

Hiyo ndiyo investment nzuri ya ardhi yetu ambayo si tu ina rutuba bali pia rasilimali. Hakuna nchi ambayo haina wawekezaji kutoka nje,ila sisi wawekezaji wetu pamoja sera zetu za uwekezaji havionyeshi matunda yoyote yale kwa nchi yetu...Kwetu ni wachukuaji badala ya wawekezaji. Chamsingi serikali inatakiwa ijenge mfumo ambao hata kama kuna wawekezaji wa nje basi mnufaika awe mwananchi kwani ndiyo mwenye ardhi,kama serikali ikishindwa kusimamia ardhi ya wananchi kwa niaba yao,then wananchi wanaweza wakachukizwa....Ila cha kusikitisha ni wamba asilimia kubwa ya wananchi hao wameridhika na shida,wengi wao wakiamini maneno ya Rais wao kuwa nchi ni masikini...Viongozi wetu wanachezea akili za wananchi hao ambao wengi wao hawaelewi kuwa wanachezewa kwani kwa mujibu wa Maslow Hierachy,wananchi hao hawawezi kufanya hivyo kwani wanaamini kuwa wao ni masikini na inakuwa rahisi kwa wengi wao kuamini hivyo kutokana na shida za lazima kama vile chakula,mavazi na hata malazi. Hivyo basi kufanya immediate needs za wananchi hao kuwa zile ambazo ni basics needs za level ya kwanza ya hierachy,hivyo basi kuendelea kudumaa kimaendeleo na kifikra na huku tabaka flani likiendelea kunufaika na vile vinavyouzwa na huku mwavuli wa soko huria waliopewa na mabepari hao wezi wenye kujiita wawekezaji wakisaidiwa na mawazo ya viongozi wetu ya kikahaba,ukiwakinga dhidi ya mvua za lawama kuwa mfumo huo si wa haki dhidi ya wananchi na si sahihi kwani haki za kibinadamu pia zinakuwa jeopordized in a different dimension.

Nina amini kuwa wananchi kama watoto ni product ya ukahaba wa viongozi wao kama wazazi na huku wakiwa hawawafikirii tena watoto wao na wakiwaacha wafe njaa kwa madai kuwa hajapata chochote,kwamba wao ni masikini.Kama mnakumbuka,Mwinyi alisema watanzania wameukalia uchumi na huku kiongozi mwingine (JK) akija na kudai kuwa wao ni masikini,hizo ni kauli tofauti za viongozi wetu wa juu.

Mfumo mzima umewafanya watanzania kwa ujumla kuwa na tabia kama hizo hizo za kikahaba,bila rushwa hata mtu wa kawaida anaona kama hajapata Huduma inayotakiwa,kwamba uwezo wa kutoa rushwa ni status kubwa sana tu kwenye jamii,NA WENYE UWEZO WA KUTOA RUSHWA ILI WAPATE HUDUMA NDIO WENYE KUHESHIMIWA,na hivyo kupelekea kuwa na utamaduni wa rushwa ama kuwa na jamii yenye kutaka kuwa na uwezo wa kutoa rushwa,ni kama priveledge,kama ufisadi,ni mtoto ama kijana gani ambaye hatapenda kuwa fisadi? Fisadi pia ni status kwani hata Rais si alishakiri kuwa hawawezi?Fisadi yuko juu ya sheria,fisadi ana nguvu kuliko serikali,nani hatopenda kuwa fisadi?

Back kwenye kilimo,kwa kifupi ni kwamba inawezekana kabisa kuwa tuna wataalam wa kutosha ila serikali haijaamua kuwa serious kwenye kulimaliza hili suala la kilimo once and for all,assuming kwamba tuna wataalam wa kutosha kwa kuanzia,then...Namba moja ni zana bora za kilimo, kilimo cha umwagiliaji kwa mazao both ya chakula na biashara,uzalishaji wa mbolea,mbegu bora,pia food processing na packaging kwa ajili ya kuuza surplus pamoja na cash crops.

Hatuwezi kuuza ardhi yetu simply tu kwa madai ya uwekezaji,ni lazima tujiulize maana halisi ya uwekezaji,wananchi ni muhimu waulize maswali muhimu kuhusiana na issue kama hizi,ni kivipi wananchi wanaweza kuunganishwa ili waihoji serikali bila siasa kuingizwa? Yaani wananchi ambao haijalishi hata kama wako vyama tofauti na itikadi tofauti lakini waweze kuuliza kuwa ni kivipi hakuna manufaa ya uwekezaji ambayo hayaonekani kwa mwanachi wa kawaida? Na mbona machoni petu uwekezaji huo unaonekana kama ni uchukuaji? Nchi kama ya marekani ilijengwa na wawekezaji kutoka nje na uwekezaji huo ukawanufaisha wamarekani na Taifa kwa ujumla,madini na rasilimali nyinginezo vikawanufaisha wananchi,kwetu sisi ni tofauti.

Mabadiliko ya kweli yataletwa pale wananchi watakapoamua kutoridhika na umasikini na kuuliza maswali muhimu,kuukataa ukahaba kwa nguvu zetu zote,si rahisi,inahitaji pia kujitolea kwa viongozi wetu kwani tabia hiyo imekuwa ni tabia sugu,mapinduzi ya kifikra na kijamii yanahitajika kwanza ili serikali ije na mfumo utakaoinua kilimo na maisha ya wananchi ambao wengi wao wanategema kilimo.
 
Rev hilo neno kali mno hakuna m-badala wake?

Hilo ndilo safi. Ndilo neno lililowavutia wasomaji wengi wa post hii,including wewe. Au ulikuja kwa kutaka story ipi huku? Neno kalitumia kiufasaha kabisa. Big up rev.Kishoka!
 
Nendeni mkapige kura muwang'oe wale wasiofaa ili tusiendelee kuwa makahaba!
 
Back
Top Bottom