Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Kwa nini Watanzania wanavutiwa na mtu mkali? Mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wakimwagia sifa Kiongozi fulani kwa kuwa ni mkali, nimesikia watu wakisema kwa mfano ka Jafo kanafaa sana kuwa Rais kakali sana'', ukali unahusiana nini na Uongozi mzuri na makini wa nchi ? Vipi kuhusu intelligence?
Au ni jinsi tunavyolelewa labda kwa maana hata Shuleni Mwalimu anayesifiwa ni yule mkali na katili anayechapa watoto viboko bila ya huruma.
Hakuna correleration au uhusiano wowote ule kati ya ukali, intelligence na maendeleo ya jamii, mtoto hajifunzi vizuri kwa viboko ingekuwa hivyo Shule za private ambazo watoto hawachapwi zisingeongoza matokeo, leo hii kila mtu anaota kupeleka mtoto wake IST Shule ya kimataifa ambapo hakuna viboko kwa nini kama bila ya viboko mtoto haendi? Au asienda bila ya viboko ni mtoto wa wengine tu?
Ukali au intelligence kipi muhimu? Binafsi nachagua intelligence, sijawahi kusikia nobel laureate yoyote ambaye amewahi kusema siri ya mafanikio yake ni viboko alivyopigwa alipokuwa mtoto, kama ukatili dhidi ya wengine ungekuwa unajenga nchi Dunia nzima wangekuwa wanachapana viboko, lkn sijawahi ona nchi yoyote ile iliyoendelea na tajiri wakiwafanyia ukatili raia wao wenyewe.