Ukali na intelligence: Kipi kigezo bora anachopaswa kuwa nacho Kiongozi?

Ukali na intelligence: Kipi kigezo bora anachopaswa kuwa nacho Kiongozi?

Kwa nini Watanzania wanavutiwa na mtu mkali? Mara nyingi nimekuwa nikisikia watu wakimwagia sifa Kiongozi fulani kwa kuwa ni mkali, nimesikia watu wakisema kwa mfano ka Jafo kanafaa sana kuwa Rais kakali sana'', ukali unahusiana nini na Uongozi mzuri na makini wa nchi ? Vipi kuhusu intelligence?

Au ni jinsi tunavyolelewa labda kwa maana hata Shuleni Mwalimu anayesifiwa ni yule mkali na katili anayechapa watoto viboko bila ya huruma.

Hakuna correleration au uhusiano wowote ule kati ya ukali, intelligence na maendeleo ya jamii, mtoto hajifunzi vizuri kwa viboko ingekuwa hivyo Shule za private ambazo watoto hawachapwi zisingeongoza matokeo, leo hii kila mtu anaota kupeleka mtoto wake IST Shule ya kimataifa ambapo hakuna viboko kwa nini kama bila ya viboko mtoto haendi? Au asienda bila ya viboko ni mtoto wa wengine tu?

Ukali au intelligence kipi muhimu? Binafsi nachagua intelligence, sijawahi kusikia nobel laureate yoyote ambaye amewahi kusema siri ya mafanikio yake ni viboko alivyopigwa alipokuwa mtoto, kama ukatili dhidi ya wengine ungekuwa unajenga nchi Dunia nzima wangekuwa wanachapana viboko, lkn sijawahi ona nchi yoyote ile iliyoendelea na tajiri wakiwafanyia ukatili raia wao wenyewe.
Nani kakwambia tanzania raia wanafanyiwa ukatili !

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ukali ni mfumo wa kutumia nguvu zaidi ya akili.

Kujenga ushawishi na kukubalika ni mfumo wa kutumia akili zaidi kuliko nguvu.

Kuna Watanzania wengi wanapenda kutumia nguvu kuliko akili.
 
Dunia yenyewe inaendeshwa kwa misingi ya ukali

Intelligence ni umbo la nje tu la kuzugia

Ukweli wenyewe ni mkali

Nimemaliza
 
Ila nadhani kuna aina nyingi sana za ukali. (My perception!)

Let’s say ; 1)Ukali wa uso wa mbuzi (Huu ni ule muhusika haangalii Sura anapotoa maelekezo ama anapotoa adhabu , ila kwa kiasi chake anazingatia matokeo kadiri ya ufahamu wake!)

2)Ukali wa ukatili (Huu ni ule muhusika hajali matokeo yoyote yatakanayo na maelekezo yake ama adhabu zake, yawe matokeo positive ama negative, humwambii kitu!)

Bahati mbaya sana hapo kwenye “Intelligence “, sio wengi wetu tumejaaliwa kuitambua iliyopo ndani yetu na kuitumia ilivyokusudiwa!

Nafikiri kwa sauti!
Ukali wa mbuzi¿¿
Kwani ukali ni behavior, attitude au Values???
 
Back
Top Bottom