Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Pathetic
 
Wakati zoezi la uopoaji miili ya wahanga wa ajali ya maji iliyotokana na kivuko cha Mv Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Kisiwa cha Ukara na Bugorora wilayani Ukerewe, Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi amesema kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati.

Amesema kuwa Kivuko hicho kilifanyiwa ukarabati miezi miwili iliyopita, hivyo kilikuwa sawa na kilikuwa mbioni kubadilishiwa ratiba ikiwemo kuongeza idadi ya safari ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo.

“Kuhusu hoja yangu niliyoitoa bungeni, ilifanyiwa kazi ambapo tulikuwa tunahitaji injini mbili ambazo zilipatikana na zikafungwa labda tu suala ambalo lilikuwa bado tunalifanyia kazi ni kuona namna gani tunaweza kubadilisha idadi ya safari”, amesema Mkundi

Aidha, amesema kuwa yeye mwenyewe ni miongoni wa watu waliopoteza ndugu katika ajali hiyo ambapo amedai kuwa takribani ndugu zake watatu wamefariki kwenye ajali hiyo.
 
poleni wafiwa wote sisi sote ni ndugu tunawaombea faraja!

waliokufa sio wasukuma pekee au wakara pekee ni watanzania wa makabila mbalimbali tuweke ukanda pembeni tulie na yaliyoyukuta
 
Wewe kuna kitu hutuambii kuhusu Mbowe na Chadema. Huenda ulitaka kupewa nae ila kakutosa. Haiwezekani uweweseke nae hivyo. Wewe na yule Mramba ni naona mmepewa special assignment ya kudeal na Mbowe. Kila siku unaanzisha uzushi kwa Mbowe na Chadema Baada ya kujifanya mwanachama watu wanakuchora tu. Pole maBwana wapo sema wanaoa waliotulia, vicheche hutumiwa na kuachwa
 
We ndugu

Mbowe alimtaka Rais aongee na sio Msigwa Kutoa Twite kwamba Rais amesikitishwa hatimaye Rais kazungumza, je ndio kuvuliwa nguo huko?

Pili lawama kwa serikali haiepukiki kwa sababu zilizo wazi. Moja ndio yenye jeshi la uokozi sio vyama vya siasa. Pili serikali ndio mmiliki wa kivuko, tatu serikali kupitia Sumatra ndio mkaguzi maswala ya usalama wa vyombo vya usafiri na mwisho ndio operator wa kivuko hicho sasa lawama apewe nani?

Tumeona wavuvi ndio wamefanya kazi ya uokozi na uopoaji wa maiti je jeshi letu la uokozi lipo wapi inafika usiku wanasimamisha kazi ilihali watu bado wamenasa ndani ya meli.

Kwa muktadha huo huoni aibu kwa uliyoyaandika. Tusifie pale panapostahili na tukosoe pale inapohitajika. Sio kila kitu kusifia natamani upate janga kama hilo ndio akili ikukae vizuri.

Roho za marehemu wote waliokufa kwenye ajali Mungu azipe pumziko la milele
 
Utafikiri sisi wote hatuna akili.Hao ni wanasiasa maarufu sana ndani na nje ya Tanzania.Ni wabunge na wanaeleweka.Hawahitaji msiba kuwa mtaji wao,mtaji tayari wanao ndiyo maana ni wabunge.Lengo ni kuzua watu wasihoji uzembe wa namna uokoaji ulivyofanyika,ukosefu wa vipaumbele na usitishaji uokoaji eti sababu ya giza.Hata wanasiasa wasipoongea,picha zinaongea pia.
 
Kwa kweli ni habari ya masikitiko kwa Taifa letu! Mungu atuongezee nguvu na kukabili hili janga la msiba wa kitaifa!
 
SUMATRA ni watozaji wa fedha tu usimamizi mbovu sana.
 
Maboya ya kujiokoa yalikuwa yamefungiwa stoo kwa kufuli kubwa!....This is Africa!
 
Safari hii kipaumbele ni dirimu laina, maswala ya vivuko yasubiri tufikishe idadi angalau 4 tuweze kumfunika jirani
 
Mbunge kamuumbua mwenyekiti wake Mbowe....... hii ni Aibu kubwa kwa KUB!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…