Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Mnatuita majina mengi..wananchi wa kawaida,masikini,wanyonge kwenye nchi yetu huru,malofa nk....mnawezaje kutulinda na majanga wakati hatuna thamani mbele yenu...wananchi 2020 chagueni wengine labda hawatatuita kwa hayo majina...
 
Aise imenikumbusha wimbo wa Marijani Rajabu.........Dunia ya sasa imani imekwisha mioyo ya watu imebadilika wala hakuna uaminifu tena.............
Kumbe hauvumi lakini umo. Hebu tumiana mimi rambirambi yako nataka nikanunue kitimoto watoto wasilale njaa
 
 
Mtanyooka tu nyinyi na mawazo yenu uchwara! Haya mbunge wenu amewatosa kwa maneno yenu ya uongo tuuu!!
Kabla ya mwaka 2015 wabunge wa CHADEMA walikuwa wachache kuliko wa CCM. Hiyo ilisaidia nini nchi yetu kuliko ilivyo sasa?
 
Mmoja ya wadau amesema possible reason ni kuwa watu walihama na kusogea mbele ili kuwahi kushuka baada ya kivuko kukaribia nchi kavu, kwahiyo uzito ulisababisha kivuko kuelemewa upande mmoja
Bado hiyo ni sababu ya kijinga tu! Chombo cha abiria 100 unapojaza zaidi ya mara mbili unatumia akili gani hiyo? yaani meli iliyobeba abiria wanaostahili inaweza kuzama kwa sababu ya watu kusogea mbele, Kweli?

Nimejaribu kujieleza kwamba taratibu za vyombo kama hivi hazistahili kusimamiwa na watu wapuuzi. Kuna watu hata kama wakisoma ujinga wa kupenda sifa kinyume na mafunzo yao hauwatoki.
 
Maboya ya kujiokoa yalikuwa yamefungiwa stoo kwa kufuli kubwa!....This is Africa!
 
Kuna kitu kwenye hizi updates sijakielewa. Kuna taarifa mbili kuwa, Nahodha anashikiliwa kwa kumpa deiwaka ambaye amesababisha ajali; taarifa ya pili inasema Nahodha Mkuu ni moja ya waliofariki! Hapa, sijaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…