Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Mnatuita majina mengi..wananchi wa kawaida,masikini,wanyonge kwenye nchi yetu huru,malofa nk....mnawezaje kutulinda na majanga wakati hatuna thamani mbele yenu...wananchi 2020 chagueni wengine labda hawatatuita kwa hayo majina...
 
Aise imenikumbusha wimbo wa Marijani Rajabu.........Dunia ya sasa imani imekwisha mioyo ya watu imebadilika wala hakuna uaminifu tena.............
Kumbe hauvumi lakini umo. Hebu tumiana mimi rambirambi yako nataka nikanunue kitimoto watoto wasilale njaa
 
Amani iwe nanyi wapendwa.

Rais wetu mpendwa Dr Magufuli jana ametoa salamu za pole kwa wote waliofikwa na msiba kutokana na ajali ya Mv Nyerere, pia salamu hizo zimelengwa kwa watanzania wote kwa ujumla ndiyo maana akatangaza siku nne za maombolezo na bendera za taifa kupepea nusu mlingoti nchi nzima.

Jambo la pili amewashukia kama mwewe baadhi ya wanasiasa viherehere waliofilisika kichwani ,ambao kwao ajali ya Mv Nyerere wameigeuza kuwa fursa ya kupata kiki kisiasa.
Ikumbukwe kuwa mara baada ya kutokea ajali hiyo mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe aliitisha vyombo vya habari na kuanza kutafuta kiki kwa kujigeuza mahakama na kuanza kushutumu na kuhukumu watu kwa mambo asiyoyajua vizuri.

Pia Zito Kabwe na James Mbatia hawakuwa nyuma katika kutumia msiba huu kama mitaji yao ya kiki za kisiasa .
Inasikitisha sana viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kuwahi eneo la ajali kwenda kutoa msaada kwa wapiga kura wao ,wanabaki twiter kukejeli wafiwa na kujijenga binafsi kisiasa bila kutoa msaada wowote!!!

Hongera sana Rais Magufuli kwa kuwavua nguo hawa wanasiasa uchwara ,wachumia tumbo na wanafiki ,ambao wao muda wote wanawaza siasa tu huku vyama vyao vikiwafia kwa kukimbiwa na wananchi..[/QUOTE]

Hapo nilipopigia mstari ni kama unajisema mwenyewe. Bila hata akili za degree, ni dhahiri kabisa kwa haya maandishi yako.. wewe unaonekana mchumia Tumbo, mnafiki na mwanasiasa Uchwara. Inawezekana JPM alikuwa anakusema wewe.
 
Mtanyooka tu nyinyi na mawazo yenu uchwara! Haya mbunge wenu amewatosa kwa maneno yenu ya uongo tuuu!!
Kabla ya mwaka 2015 wabunge wa CHADEMA walikuwa wachache kuliko wa CCM. Hiyo ilisaidia nini nchi yetu kuliko ilivyo sasa?
 
Mmoja ya wadau amesema possible reason ni kuwa watu walihama na kusogea mbele ili kuwahi kushuka baada ya kivuko kukaribia nchi kavu, kwahiyo uzito ulisababisha kivuko kuelemewa upande mmoja
Bado hiyo ni sababu ya kijinga tu! Chombo cha abiria 100 unapojaza zaidi ya mara mbili unatumia akili gani hiyo? yaani meli iliyobeba abiria wanaostahili inaweza kuzama kwa sababu ya watu kusogea mbele, Kweli?

Nimejaribu kujieleza kwamba taratibu za vyombo kama hivi hazistahili kusimamiwa na watu wapuuzi. Kuna watu hata kama wakisoma ujinga wa kupenda sifa kinyume na mafunzo yao hauwatoki.
 
Maboya ya kujiokoa yalikuwa yamefungiwa stoo kwa kufuli kubwa!....This is Africa!
 
Kuna kitu kwenye hizi updates sijakielewa. Kuna taarifa mbili kuwa, Nahodha anashikiliwa kwa kumpa deiwaka ambaye amesababisha ajali; taarifa ya pili inasema Nahodha Mkuu ni moja ya waliofariki! Hapa, sijaelewa.
 
Back
Top Bottom