Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

"Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao...fikisha salam mimi

John Kisekwa.
 
Deiwaka kwamba hajui kbsaa kuendesha icho chombo au deiwaka nae ni dereva mzuri sema hakua na chombo cha kuendesha tokana na ufinyu wa vyombo vya majini?by the way jiwe asije kusema kama yale ya bukoba mbele za watu na ikiwezekana abaki ukouko dar tu awe anatutumia salamu isije kua mkosi wake unahusika
 
Mbowe njoo,kuna msaliti huku,fanya haraka[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tukiendelea na maombolezo ya wapendwa wetu,niwape pole nyingi wafiwa na Watanzania kwa ujumla.Majeruhi wetu Mungu awaponye mapema.
Katika salam za pole toka kwa mkuu Jana,sina uhakika ilikuwepo haja ya mkuu kuwajibu ama kutoa angalizo kwa viongozi wa kisiasa.Na sina uhakika ule ulikuwa Muda muafaka kwa yeye kama baba na Mtanzania no.1.Kuanza kujibu maoni na ushauri toka Watanzania wengine.
Tunajenga taifa la ajabu la kutokusikiliza maoni na mawazo ya watu wengine.Kama taifa tujenge na kuheshimu utamaduni na mifumo tuliojiwekea.
 
Reactions: prs
Zimetangazwa siku tatu za maombolezo na sio siku ya mapumziko.

Nenda kazini ukiwa unatafakari na kuwaombea rehema ndugu zetu.
 
Nakuunga mkono ndugu, Ila ujue Pia kujaza zaidi huwa chombo kinadidimia chini y'a floating level ! Hapa issue ni centre of buoyancy ndio inafanya chombo kupinduka ! Mizigo zaidi huzamisha !!! By the way kama mizigo ilizidii upande mmoja na pia watu wakaelekea huko huko lazima chombo kipinduke ! Ndio inakuja lack of qualified skilled people
 
Huyu jiwe anasema aliyezamisha kivuko alikuwa deiwaka ,hivi kazi hiyo ya professional kweli inadeiwaka .aache kuwa laghai wananchi ila yule mkuu wa mkoa aliyesema saa mbili giza tualishe mpaka kesho mungu anakuoana.roho za watu zinaangamia kisa giza wakati mngeweza funga sport lighting mambo yangeendelea.
 
Dah inauma sana ila nawaza tu tamko la RC isiwe ishu kiasi hicho, ni makosa ya kibinadamu, lakini pia nahisi alihofia maisha ya waokoaji, maana kwenye Maji kuna mamba, chunisi etc so may be alohofia waokoaji kwenye Giza kudhurika
 
Sumatra hivi wanazo patrol boat zao kwa ajili ya kukagua muenendo wa hivi vyombo vya majini vilivyosajiliwa Tanzania?
Nazungumzia doria za mara kwa mara kwenye maziwa yetu na mito ili kujua mwendeno wa hivi vyombo mara kwa mara na si kukaa ofisini na kutuma wakaguzi chombo kikiwa kimepaki bandarini au kwenye gati. Hizi ni basics tunatakiwa tufanye ili kuzuia matatizo kabia na si kusubiri yatokee tuanze kukimbizana..
 
Binaadam na kusahau kupo
Kuna meli iliokuwa imekula nyomi la watu na mizigo kama MV BUKOBA??
Lawama zilikua kama hizi za Mv Nyerere
Ohh!!meli/fery ilikua Over Loaded!!Ohh,hamna uboreshaji mzuri wa waokoaji.
Tena kibaya zaidi Mv Bukoba waliitoboa kwa moto wa gesi ndio ikazama kilaiiiini,,na maelf ya watu walipoteza maisha
Je kuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa waliohusika/kusababisha hio ajali??
Cha msingi tuendelee tu kuwa wastahamilivu na tuzidi kumuomba mola wetu atuepushe na majanga haya
 
huyu mtoa mada kachanganyikiwa kiasi..
cha msingi ni kwamba
KIVUKO CHA POMBE kimeua, alikinunua mwaka 2004 akiwa waziri wa miundo mbinu, tukumbuke pia pombe alinunua kivuko kingine kibovu cha MV DAR ES SALAAM..
pombe huyuhuyu kajenga hosteli mbovu zinazopasuka zikiwa bado mpya..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…