Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Wadau hii imekaaje?

Nilikuwa nangalia vipindi vya maombolezo kupitia tivi ya taifa.

Sasa mbona maombolezo haya yamekaa kikristu kristu zaidi?

Wanyarwanda na nyimbo zao wanafunika.


Najua wapo watakaokuja kuniponda kwa ukweli niliouona.

Nipo tayari kukosolewa.
 
Hivi kaokolewa ? Au kaibuka mahali au katapikwa kama yona Na samaki baada ya siku tatu?
 
Hiki kivuko kikiibuliwa na kukarabatiwa kisitumiwe tena na raia kikabidhiwe jeshini ili kiwe kifaa cha kijeshi, wananchi tusikijadili tena chenyewe na huu mkasa
 
Pole sana mkuu. Nayahisi maumivu muliyoyapitia.
 
duu inasikitisha sana ndio naamin kuwa kuna watu wengi wangepewa msaada mwanzo wa tukio wangeweza kuokolewa yan uzembemkubwa sana ulitumika kwenye tukio hili.
 
meli kupinduka ilikuwa mipango ya Mungu, ila vifo vingi vilikuwa kwa mapenzi ya serikali yetu.
Ni akili finyu na mbovu za mwenye jukumu la ulinzi na usalama wa mkoa husika, ndiye wa kunyooshea kidole kuhusu idadi ndogo ya waliookolewa wakiwa hai.
 
Mkuu wa mkoa kasema wataalamu ndo walimwambia kua giza lishaingia so hawawezi kuendelea
Source video clip Instagram Issamichuzi

Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa.

Aliambiwa na nani.. Maamuzi yote alikuwa nayo yeye.
 
Ila mm hii nimeshindwa kuimeza asee maana kuna sehemu alikuwepo kulikua na hewa ya oxygen aliweza kupumua kwa izo siku3 jmn
 
Mongela you need to be proactive.
Ungeanza kujipanga mapema na mahema. Majenereta. Bulbu.fedha kidogo na chakula kwa waokoaji. Huyu aliyeokolewa hai leo angetoka na wengine wengi wasio na hatia.
Mongela alifika eneo na tukio na smart phone minus washauri wake na hakua na mkakati wowote zaidi ya kupigwa picha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…