Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Real point
Sio suala la abiria kujua kuwa kivuko kina beba watu wangapi, hapo kinachoangaliwa ni uwezo wake wa kubeba ni tani ngapi!! Kama kina beba jumla ya watu 100,na tani 25 za mizigo, je kama siku hiyo kimebeba mizigo tani 10,abilia wanaweza panda hata 200,hilo ni wasimamizi wake ndio wanajua. Je wakataji tiketi wanapokata hawajui idadi inayotakiwa? Na tamesa wote wanajua kuwa huwa vinazidisha abiria kwani mapato yake ya siku c wanayaona? Dsm tu daladala ni nyingi na mtu unalazimisha kujibana humo humo wakati baada ya dk tano kuna nyingine inafika!! Sembuse usafiri wa visiwani ukiikosa leo hadi baada ya siku tatu tena?? Na kama huko ukara hi mala moja kwa wiki alhamisi tu!! Na wao tamesa wanafurahia tu kwani ni trip moja kwa wiki ila mtu wake ni nyomi ya kufa mtu!! Sema limetokea hili ndio watajifanya kuwa ni bahati mbaya!!
 
Jina la kivuko kilichoza huko Ukara linatukumbusha muasisi wa Taifa letu ambaye alituunganisha kuwa Taifa moja la kusaidiana katika shida na Raha bila kubaguana kwa dini zetu Wala itikadi nyingine zozote zikiwemo za kisiasa.

Juzi tumepatwa na majonzi ya kuondokewa na ndugu zetu baada ya kivuko kuzama ambapo badala ya viongozi wetu kuwa kitu kimoja tulishuhudia kila mmoja kwa nafasi yake akiandika na kuongea anachojisikia katika media mbalimbali.

Tumeshuhudia Televisheni za nje zikirusha matangazo ya janga la ajali kwa muda mrefu kuliko hata Televisheni zetu ikiwemo Televisheni ya Taifa ambayo inaendeshwa kwa Kodi za wananchi. Labda niwakumbushe wamiliki wa vyombo vya habari kuwa watu hawakutaka warushe matangazo mubashara kwa lengo la kuona picha za ajali bali tulitegemea media zipaze sauti kuwaalika wadau mbalimbali wa uokozi walete ujuzi na vifaa katika kusaidia kuokoa ndugu zetu, ninyi mliona ni vyema mpige mziki na kuendelea na vipindi vyenu kwa manufaa mnayoona yanafaa.
Tumeshuhudia wanapotutoka wasannii wakubwa na viongozi wa mbalimbali mkisitisha matangazo mengine na kuomboleza kwa muda wa masaa au siku kadhaa bila hata kupewa maelekezo kutoka popote lakini kwa Mv Nyerere amkufanya hivyo....hii ni dalili ya mgawanyiko na ubaguzi ambao mwalimu aliupiga Vita.

Kilitolewa kigezo Cha Giza kusitisha uokoaji na sijaona media au KIONGOZI wa chama Tawala na serikali aliyejitokeza adharani kukemea tamko hilo lakini tumeshuhudia ajali za viongozi na wanasiasa namna zinavyoshughulikiwa..hiki kilichotokea kinatufumbua macho kuwa sisi siyo wamoja tena kwani hata viongozi wa vyama vya upinzani walikuwa na uwezo wa kwenda kuwahamasisha wananchi wakakesha wakifanya uokozi lakini nao wamebakia kwenye media kutoa matamko na kulialia bila kuchukua hatua...ubaguzi Ni dhambi kubwa.

Viongozi wa dina nao badala ya kukemea wamekuwa wanatoa kauli Tata mitandaoni bila kutoa dira na hivyo kuonyesha Kama vile wanaogopa Jambo flani japo na amini hakuna hofu kubwa kuliko hofu ya Mungu..mkiwaogopa binadamu kuliko Mungu mtaliteketeza Taifa, zungumzeni na kusimamia haki kwa Taifa Kama dini zinavyowaelekeza na siyo kuangalia binadamu anataka nini.

Ukiona Taifa limegawanyika kwenye mambo Kama haya tambua Taifa linafungua milango kwa maadui kuingia ndani kwa kupitia mianya na mgawanyiko tulioutengeneza.

Mwisho:Tunaweza kuwa na vyama vya siasa na asasi mbalimbali kwa wingi na mahitajio tunayotaka lakini hatuwezi kuwa na Tanzania zaidi ya hii tuliyonayo Sasa.

Unaweza kuhama vyama na dini utakavyo na ukaendelea kuishi huru Tanzania lakini usitegemee kuishi huru nje ya nchi yako.

Unaweza kutumia nguvu na jitihada nyingi kujenga taasisi au chombo chochote ndani ya Taifa lisilo na mgawanyiko lakini adui anaweza kubomoa taasisi na vyombo vyote pale mnaporuhusu mgawanyiko na maslahi binafsi kuwaendesha.

Pole kwa ndugu na jamaa mliofikwa na msiba.
 
HAPO WA KULAUMIWA NI @SUMATRA..Hao polisi TRA,hayo sio mamlaka yao,,kama polisi,kitengo cha Marine wao wanasubiri order tu kutoka Sumatra.
Police wanasimamia pale ..tra inajua capacity ya kivuko mana wanakatisha ticket kwann wasiseme
 
"Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao...fikisha salam mimi

John Kisekwa.
Hebu tuambie mlikuwa wangapi ndani ya Kivuko??
 
Baada ya mbunge wa Ukerewe kuongea kuwa kivuko kilifanyiwa marekebisho baada ya yeye kuwasilisha hoja bungeni, Ufipa imewauma sana kwa huu USALITI wa mbunge wao.
Naona sasa watahamishia majeshi kwenye hoja hii ya jamaa kupona na serikali kusitisha zoezi la uokoaji.
Da, watu wapo kwenye majonz wewe unaleta mambo yako ya uchama, da kuwa na huruma basi dada, chama umekikuta na utakiacha.
 
Hivi kaokolewa ? Au kaibuka mahali au katapikwa kama yona Na samaki baada ya siku tatu?

Sasa sijui inakuaje na huyu aliyesitisha zoezi la utafutaji siku ya kwanza kisa Giza na kuhitimisha hakuna atakayekuwa hai.
 
Habari zinazoripotiwa kutoka eneo la tukio zinasema mtu mmoja ameokolewa akiwa hai asubuhi hii

Mtu huyo ambaye ni engineer wa ferry hiyo amekutwa akiwa hai

Chanzo: ITV

Kumbe serikali imefanya makosa sana kuzuia uokozi usiku ule,wangeokolewa wengi wakiwa hai

Wao wanasafiri kwa V8, wanashida gani?

Anyway huyo aliyeokolewa akiwa hai ana mengi ya kusimulia, nadhani kama kuna hukumu ya kimahakama basi huyo atazamwe kwa jicho tofauti, kifungo alichokipata kwa saa 36 kinatosha
 
Kwa kweli huyu jamaa jana kaniudhi sana kwa kukosa ubunifu. Boti iliyozama iko mita 50 toka nchi kavu. Huyu mkuu badala ya kuwasha genereta hata nne tano na kuziweka kwenye boti na kuwasha taa na kuendelea na uokoaji. Kirahisi tu huyu mkuu linasema kuna giza tukalale turudi kesho asubuhi. Kweli ? Really ? Leo baada ya kuhakikisha hakuna mtu aliye hai zoezi linaendelea usiku.
Huyu atumbuliwe kwa kukosa ubunifu akaongoze zizi
Bishoo huyo.Mtoto wa waziri sehemu kubwa ya uhai wake.It was time to sleep,mum said.Lazima aondoke kulala.
 
Habari wanaJF....!!!

Kwa huzuni na majonzi[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]makubwa kupitia tukio la kitaifa la kuwapoteza ndugu zetu na majirani zetu kwa ajali ya MV Nyerere Wilayani Ukerewe.

Tuungane pamoja kuwapa faraja na kuomboleza vifo vya wenzetu waliyopoteza uhai kupitia ajali hiyo ya majini. Mpaka Sasa miilli wapatao 157 imeopolewa.
IMG-20180922-WA0004.jpeg
 
#ITVupdate:Mmoja wa Mainjinia wa Kivuko cha Mv.Nyerere kilichopata ajali ya kuzama ziwa Victoria ameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai.
Nina uchungu na hawa nyang'au Mungu ndo anajua. Juzi Mkerewe mzima kisa tu Ukuu wa Mkoa anasitisha uokoaji eti kisa Giza.? Na vimada wa Lumumba humu JF wakaja na hoja nyepesi za kipuuzi. Niliwauliza usiku ule Nani aliyewapima wahanga mle ndani ya meli na kugundua WOTE wamekufa? Haya nyie kunguni mnaoishi kwa kujipendekeza njooni tena muunge mkono kauli za Mongela!!
 
Back
Top Bottom