Copy and Paste
Tarehe 25 March 2016, huko Watchet, West Beach, Laguna, California.
COASTGUARDS, boti za uokoaji (lifeboats) mbili, paramedics (watoa huduma ya kwanza) pamoja na chopa (helicopter) zilihusika katika usiku wa kuvutia, kwa zaidi ya masaa sita wakati wa kuokoa baharia mmoja ambaye MASHUA yake ilipigwa na mawimbi mazito na kukosa uelekeo na kuzama.
Baharia huyu mzoefu sana, umri wa kati alikuwa akiendesha chombo hicho kutoka Penarth kwenda Watchet usiku wa Jumamosi tarehe 25/03/2016 kwenye mashua yake ya rangi ya blue 25ft fin-keeled, wakati 'injini' ilipogoma kufanya kazi.
Shuhuda wa tukio akatoa taarifa kwa haraka, baada ya kuona mashua ikipigwa na upepo wa Kaskazini Mashariki (North~easterly wind) kupelekwa kwenye miamba kutoka kwenye ukanda wa West Street Beach.
Shuhuda wa tukio hilo anaitwa Jeff Bourne, akatoa taarifa kwa LAPD (Los Angeles Police Department) wao wakafika na chopa, paramedics, na lifeboats mbili kwa ajili ya 'kuokoa mtu mmoja' walitumia saa sita kumtafuta, kumpata na kumuokoa (kama inavyoonekana pichani).
Tarehe 20 September 2018, Bugolora, Ukerewe, Mwanza, Tanzania.
Kivuko cha Mv.Nyerere chenye kufanya safari zake Bugorora hadi Ukara, kupitia Ziwa Victoria, kinazama majira ya saa 10 jioni just mita 100 tu kabla ya kufika ufukweni. Boti za wavuvi zinajaribu kuokoa watu kwa njia za jadi. Wavuvi hawana nyenzo wala hawana skills za uokoaji lakini wanajitahidi kuokoa watu karibu 40 wakiwa hai.
Kwa zaidi ya masaa matatu serikali haijachukua hatua yoyote zaidi ya kuangalia wavuvi wanavyozamia kuokoa manusura. Hakuna helcopter, hakuna boti za uokoaji, hakuna vikosi maalumu vya uokoaji, hakuna life jackets, hakuna paramedics, hakuna lifeboats. Kitu pekee kilichokuwepo ni mashangingi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya, ambao wamesimama kando ya ziwa wakiangalia wavuvi wanavyohangaika kuokoa waliozama.
Saa 2 usiku Mkuu wa mkoa wa Mwanza anazuia zoezi la uokoaji lisiendelee kwa sababu "GIZA" limetanda. Yani alishindwa kabisa kufikiri kuhusu kuleta 'chopa' imulike eneo la tukio uokoaji uendelee? Labda tungeokoa watu wengi zaidi.
Kwamba hata kufikiri kuhusu kutafuta msaada wa haraka wa kununua spotlights zenye watts 1500~2000 ilishindikana? Au hata kuongeza Jenereta la KV 7 ili 'uokoaji' uendelee alishindwa? Kwamba kwa uwezo wake wa kufikiri aliona heri watu waendelee kufa aje kuokota maiti asubuhi, kuliko kutafuta alternative ya mwanga usiku? Hizi ndio akili za viongozi wetu? Na bado yupo ofisini hadi sasa?
Hivi huko ziwani Askari wa maliasili wanatumia boats gani kwenye ulinzi dhidi ya wavuvi haramu? Kwanini hizo boti hazikuitwa kusaidia uokoaji?
Kweli jeshi la polisi hakuna chopa? Kamandi ya JWTZ huko Lake zone pia haikuwa na helcopter? Mwanza nzima hakuna huduma ya rescue inayotumia chopa? Kwamba tulikosa Mwanga kabisa wa kumulika eneo la tukio? The best option tukaona ni kuhairisha zoezi, tukalale, tuamke asubuhi tuje kuokota maiti? Seriously?
Fidel Castro wakati wa jaribio la mapinduzi ya kumuondoa Dikteta Fulgencio Batista madarakani, mmoja kati ya wapiganaji wenzake alizama kwenye maji, safari ya kwenda Sierra Maestra ilihairishwa ili 'mpiganaji' huyo atafutwe na apatikane.
Mwandishi wa vitabu, Muingereza George Orwell alipata kusema "All human beings are equal but some are more equal than others" kwa tafsiri isiyo rasmi Orwell alimaanisha; Binadamu wote ni sawa lakini kuna ambao ni sawa zaidi kuliko wengine"
Hebu jiulize huko kwenye kivuko kungelikuwa na mtoto wa Rais, Waziri Mkuu, au IGP je huyo mkuu wa mkoa angetoa amri ya kusitisha zoezi la uokoaji kwa sababu ya giza? Au lets assume mtoto wake mwenyewe angekuwa huko, je angeruhusu watu kwenda kulala ili asubuhi aje kuokota maiti ya mwanae? Amin, amin nawaambia mtoto wa Mongela angekuwepo kwenye kivuko asingekubali kwenda kulala aje kuokota maiti ya mwanae asubuhi. He could fight to infinity because he believe to be more equal than others. Hivi ndivyo viongozi wetu walivyojengwa.
Hii inatufundisha nini? Marekani na nchi zilizoendelea uhai wa mtu mmoja ni muhimu kuliko jambo lolote. Wanathamini utu wa kila mtu bila kujalisha ni kiongozi au sio kiongozi, ni maarufu au sio maarufu, ni mzee au kijana. Kwao utu kwanza. Ndio maana wapo tayari kukesha ndani ya maji kutafuta mtu mmoja aliyepotea baharini na kumuokoa akiwa hai, bila kujalisha wametumia gharama kiasi gani.
Lakini hapa Tanzania thamani ya mtu inategemea yeye ni nani? ni wa chama gani? ana undugu na kiongozi gani? Hujawahi kuona watu wanabaguliwa kwa sababu ya chama? Hujawahi kuona watu wananyimwa fursa fulani kwa sababu hawana ndugu zao ambao ni viongozi? Hivi ndivyo jamii yetu ilivyojengwa. Ndio maana Mongela alipoona hakuna kiongozi yeyote kwenye hicho kivuko, wala hakuna mtoto wa Rais, PM, waziri au viongozi wengine wakubwa akaamua waokoaji waende kulala, watakuja kuokota maiti asubuhi.
Lakini asingepata usingizi kama kungekuwa na mtoto wa kiongozi mkubwa kwenye hicho kivuko. Wala asingethubutu kusimamisha zoezi la uokoaji. Angepambana zipatikane helicopter za kumulika hata kama ni za kukodi. Angepambana kupata boti za uokoaji, angepambana kupata life jackets za kuwarushia manusura. He could do anything save lives. Hapa sasa ndipo utamuelewa George Orwell aliposema "All human beings are equal but some are more equal than others"
Miaka 22 baada ya Mv.Bukoba tumejifunza nini?
CREDIT. Ninja
Citation
https://www.facebook.com/