Mkuu, mfariji pekee kwenye jambo kama hili na asiye mnafiki ni MUNGU. Tumwombe kwa nguvu zote, atoe faraja na roho za matumaini mapya kwa waliopotelewa na Ndugu zao na wale majeruhi wapone haraka. Sisi binadamu ndo muda wa kujionyesha mara nyingi kinafiki sana kana kwamba hili suala ni la mtu mmoja au wa aina fulani, ndo wao tuu waongee!!!! Wengine wataambiwa wanaongea siasa!! Duu, sijawahi ona haya mambo!! Msiba ni wa Taifa, watu wawe huru kutoa maoni yao ili tupate machungu au faraja, tuone la kufanyia kazi ili kesho yasitusibu tena!!!!
Nakumbuka hapo nyuma kidogo, jambo kubwa kama hili kunakuwa na coverage kubwa ya viongozi wa kitaifa, kivyama, kidini kupewa fursa kutoa maoni.
Mfano kuna clips nyingi zisizo rasmi kwenye you tube, mpaka wenyeviti wa vijiji wanasema,walishaomba siku nyingi na kupiga kelele kuhusu kurekebishwa usafiri wa eneo hilo.
Nimemsikiliza mzee mmoja ,nafikiri ni Bugora pale alishauri mambo 3.
1. Kivuko kile kiongeze safari , ziwe 4 badala ya 1 au 2 kwa siku ili kupunguza mlundikano.
2. Waliomba zamani tuu, waletewe kivuko kukubwa au kuongezewa kivuko kingine kukidhi ongezeko la idadi ya wasafiri na mizigo
3. Kuwe na soko jingine kule Ukara kupunguza idadi ya wanaovuka kwenda kuhemea Bugorora.
Najiuliza, kutisha mtu kama huyu ili asitoe maoni, yawafikie wadau wengine ni jambo jema? Na je, hiyo nayo ni siasa?
Ninafikiri, Nia ya Raisi wetu ni njema sana, huenda tunaangushwa sana na watendaji wake. Na huenda ndo maana, anajtahidi kwa kiasi chake,afanye ziara nyingi ajionee mwenyewe hali halisi. Pia aliyasema mengi akiwa Simiyu namna mambo mengine hapewi ukweli.