Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Mkuu, sijapingana na Mkuu wa Mkoa ila napingana na mtu kama wewe. Wewe ni Diver?
 
Wanasiasa hatar badala ya kujiuzuru kawageuzia kibao wataalam dah, hatutoendelea miaka 800 kwa akili hizi ambazo kwao maendeleo ni kuweka matuta yenye uwazi ambayo wanadai kuwa ni flaiova
 
Ndugu wanabodi;
Ajali ya MV Nyerere imeleta msiba wa kitaifa ambapo zaidi ya Watanzania wenzetu 225 wamepoteza maisha.

Idadi hiyo ni kubwa sana kwa taifa letu. Hivyo ni matarajio yangu kuwa hill si suala LA kutuma uwakilishi Bali viongozi wote wa kitaifa wa vyama vya siasa,madhehebu ya dini na taasisi binafsi wakiongozwa na Rais wa JMT walipaswa kuhudhuria.

Sasa ukipeleka uwakilishi kwenye jambo kubwa la kitaifa kama hill yaani wewe unakuwa na jambo gani la kitaifa jingine?

Namshauri Rais afike Ukara yeye mwenyewe asisimuliwe na MTU ktk hili.Nawashauri viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa wafike wenyewe Ukara wasipige lamli wakiwa DSM.

Tukishindwa kuonesha umoja wetu kama Watanzania ktk hili tutaonesha maadili na umoja wa Utanzania wetu ktk lipi?

Nasisitiza tena Rais ufike Ukara,tena ktk kipindi hiki cha majonzi vinginevyo Mimi kama RAIA mwema nitaona umelichukulia janga hili sio kwa uzito unaostahili.Nakumbuka ulivyowatembelea wagonjwa na majeruhi mbalimbali huko muhimbili .Naamini hata ktk hili utafika huko Ukara kuwafariji wafiwa ktk kipindi hiki hiki cha majonzi na si muda mwingine.

Nasisitiza tena viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa,madhehebu ya dini na taasisi mbalimbali mnapaswa kufika Ukara kufariji wafiwa ktk kipindi hikihiki cha majonzi. Hii itasaidia kudumisha maadili yetu kama Watanzania na kuonesha mshikamano wetu kama taifa ktk shida na raha.
 
Cc Drlove66
 
Wanasiasa hatar badala ya kujiuzuru kawageuzia kibao wataalam dah, hatutoendelea miaka 800 kwa akili hizi ambazo kwao maendeleo ni kuweka matuta yenye uwazi ambayo wanadai kuwa ni flaiova
Mbowe amejihuzuru baada ya chama kunyauka??
 
Kwa sasa Taifa linaomboleza kutokana na Kilichotokea huko Mwanza.
Wengi wetu tumekuwa na Kasumba za Kuchukulia Vitu kwa kawaida(Mazoea), ajali hiyo imetokana na Uzembe wa Wathirika, kushindwa kugundua na kuthamini Maisha yao kutokana na tatizo la mazoea "(HUWA) tunapanda usafiri hivi" , Lazima jamii zetu ziweze kugundua kuwa Maisha hayana spare hivyo Hatuna budi kuchukua tahadhali na Kujithamini sisi na Wenzetu. Kama chombo cha Usafiri kimejaa ni vyema ukavuta Subira ukapata kheri kuliko Harakaharaka Isiyo na Baraka. Kama watu wangalikuwa wanalijua hili vifo vya kizembe kama vile Visingalitokea.


Mamlaka za Usafiri pia zinapashwa kutoa Elimu kwa raia na Kuwaajibisha Wavunja Sheria
Kama hizi mamlaka zingalikuwa makini basi wangaliweza kuzuia hili lisitokee, kwq vile watumishi wa hizi mamlaka ni wanajami wenzetu ambao wamezoea kuchukulia mambo kirahisi .


Maeneo kama ya Kariakoo na kwingineko watu wamezoea kupanda Usafiri kwa fujo ama kukimbilia Gari inakuja, nionavyo zile tabia za Mazoea zitakuja kemewa endapo watu wakipoteza maisha. Tahadhali ni Bora kuliko Tiba kama tukiendelea na Tabia hizi tulizojijengea tutaendelea kupoteza ndugu zetu na Kuishia Kubandika picha za Mishumaa Mitandaoni.
 
Ni elimu tunayotakiwa kupeana, na pia mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kwa weledi na haki. Mfano, ikiwa imesemwa katika sheria kuwa mtumiaji wa barabara ana wajibu wa kulinda usalama wake na watumiaji wengine basi hili linahusu mtembea kwa miguu, mwendesha baskeli, pikipiki na gari. Naeleza hivi kwa kuwa nimeona nchi nyingine mtembea kwa miguu akivuka barabara sehemu isiyo na alama ya kuvukia akipatikana anapewa adhabu. Kwenye gari ndogo dereva wa gari alilopanda mtu asiyefunga mkanda adhabu ni kwa wote. Hapo na sisi tungelikuwa na utaratibu huo mtu asingelikubali kupigwa faini kwa kosa la kupanda chombo kikiwa kimejaa.
 
Angalia live sasa hivi
 
Reactions: rr4
Nchi hii ya maajabu, ilipozama MV Bukoba kuliundwa hadi kamati ya maafa, chini ya Waziri Mkuu. Leo hii wamekosa hata boat zenye mataa ya kumulika usiku wanategemea za wavuvi, halafu wanatutisha tusiwahoji! Only in Africa. Ajali zipo ila hii ya kujitakia, mnataka kutwambia CHADEMA ndio wamewaambia SUMATRA wawe bize Ubungo tu na barabarani na matochi yao na kusahau na Marine ni wao! Wapo bize Dar huko mikoani mjiendeshe wenyewe.
Wanatulazimisha tunyamaze na kututishia Polisi, siku moja nasi tutakuwa na nguvu kama hao Polisi tuone mwisho wake.
Kwa nini SUMATRA hawasimamii udadi ya abiria na mizigo inayobebwa na vyombo vya majini? Au hawa SUMATRA ni wapinzani? Najaga!
 
hivi ww jamaa akili zako huwa zipo sawa!hivi kwa akili yako kweli unaacha watu wafe eti kisa huko chini ya maji kuna hali mbala??
 
Yaan ingekuwa Kuna uzinduz wa kivuko kipya. Mh mtukufu His Excellency Dr JPJ angeshafika tena na TV na waandish wa habar kama wote yan. Sema kwa kuwa n mazish tena ya wanyonge. Anawakilishwa
 
Ajali hizi zinaletwa na wataalam badala ya kutumia nyenzo za kitaaluma mume walazimisha kutembea na ilani na kuzitumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…