Ni wakati wa majanga pekee ndipo tunapata fursa ya kujifunza umadhubuti (strengths) na udhaifu (weaknesses) wetu. Majanga kama haya ndio fursa pekee ya kuipima serikali na taasisi zake kama kweli zinafanya kazi kwa maslahi mapana ya wananchi maskini au wanafanya kutafuta sifa. Kuna dhana inayoonekana kuwa serikali inajilazimisha kukimbilia kwenye vitu vichache zinavyookena kama madaraja, reli, ndege nk, huku ikisahau yale mambo ya huku chini yanayomgusa mwananchi wa chini moja kwa moja, mfano mishahara ya wafanyakazi, huduma za afya, elimu bora, huduma bora za usafiri, kuchochea ukuaji wa biashara ndogongogo na za kati, ajira kwa vijana, uhakiki wa ubora wa huduma anazopata mtumiaji wa mwisho nk.
Janga hili limeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye haya mambo ya chini ya kawaida ambayo ni haki ya msingi ya mwananchi yeyote kuzipata. Sina ujuzi wa taratibu zinazotakiwa kufuatwa katika haya mambo, ila akili yangu inanituma kuwa inatakiwa tume ya bunge kuchunguza hili tukio na mambo yote yanayohusiana na usafiri wa majini kwa ujumla. Hasa kwenye kipengele cha usalama, udhibiti wa ubora wa huduma, uchakavu wa vyombo vyote na kama bado vinafaa kuwa majini, taratibu za matengenezo na services, udhibiti wa uwezo wa kuchukua mizigo (loading capacity), mahitaji ya kila eneo lenye chombo yaani uwezo wa vyombo vs mahitaji (demand) na mengineyo ambayo wataalam wanaweza kuyashauri kwa uziri zaidi.
Ripoti kama hizi zitafaa sana kuwajibisha watendaji na kutoa mwongozo wa jinsi tutakavyoenda siku za mbeleni. Pia ripoti kama hizi zitalisaidia sana bunge kupanga bajeti zinazoendana na mahitaji husika kuliko kuiachia serikai ijipangie tu kutokana na matakwa yao na malengo ya kisiasa zaidi.
PARLIAMENT HAS TO ACT. SERIKALI KWA MAANA YA WAZIRI AMESHASHINDWA, LAZIMA BUNGE LIMSAIDIE HAPA.