Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Maxence Melo na Moderator sikuhizi JF imekufa kabisa kwenye live updates? Maana mpaka sasa ni zaidi ya miili 79 imepatikana lakini hakuna updates kwenye uzi. Nini tatizo? yaani kweli mnataka tusome comments zoote ndo tupate mwanga? Mmezuiliwa ku cover live events?
Kwa mujibu wa mwananchi mida ya saa nne asubuhi mkuu wa mkoa amesema ni miili 86 imeopolewa..Ukijumlisha na wale hai waliookolewa inaonyesha kivuko kilikuwa na watu wengi kuliko idadi inayostahili ya watu 101.
 
Dah majuzi waziri mmoja alipata ajali ilipatikana helicopter ya fasta kumuwahisha muhimbili, Jana mamia ya ndugu zetu maskini wanaangamia taa tu ya kumulika ili kuendelea kuwaokoa ndugu zetu maskini inakosekana na zoezi la uokoaji linasitishwa tukiwa hatujui hatma ya ndugu zetu...nawaza kama hawa voingozi wetu wanajali maskini au wanajaliana wao kwa wao
Binafsi nimehuzunishwa sana na Maamuzi ya mkuu wa mkoa,hivi ni kweli zoezi la uokoaji linasitishwa sababu ya giza? Watu wanahangaika usiku kucha kutapatapa kutafuta msaada hadi wanajifia hakuna wa kuwasaidia kwa sababu ni usiku?hata karabai tu zingeweza kutumika,boti zikafanya doria angalau wale watu wanaotapa tapa wangeona mwanga wakaufuata na wakaweza kuokolewa!! So sad R.I.P masikini wenzangu mliotangulia!!!! Miili yenu najua itakuwa imeshasombwa na mawimbi ya usiku!
 
naona helcopter inaelekea huko labda ndo uokoaji unaenda kuongezewa nguvu
 
Mkuu umeongea kweli tupu!

Kwa mujibu wa watu walioko kule ambao wamepata maelezo kutoka kwa manusura, inasemekana kivuko mbali ya kuwa na watu wengi, kulikuwa na mizigo mingi hasa mahindi na saruji, na magari makubwa mawili. Inasemekana wakati kinakaribia kufika ng'ambo ilibidi kukata kona ili kwenda kwenye uelekeo sahihi wa kupark. Sasa wakati wa kukata kona hapo ndo mzigo wa upande mmoja ulihamia upande wa pili hivyo balance ikakosekana kika -overturn upside down.

Haya ni maelezo ya awali lakini.
Mkuu! inamaana saruji na magari yalibimbilikia upande mmoja? picha sipati hata negative nimekosa kabisa.
 
Kwa mujibu wa mwananchi mida ya saa nne asubuhi mkuu wa mkoa amesema ni miili 86 imeopolewa..Ukijumlisha na wale hai waliookolewa inaonyesha kivuko kilikuwa na watu wengi kuliko idadi inayostahili ya watu 101.
Daah, aisee poleni sana Watanzania. Ni msiba mzito.
 
Eti ilipofika saa 12 jioni ilibidi wasitishe uokoaji kutokana na kukosa taa mpaka leo asubuhi! Yaani baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhuru tumekosa taa ya kumulikia au kupeleka umbali usiozidi mita 200 ziwani?! Hivi hata kama vifaa vilikuwa Dsm au Mtwara si wangechukua bombadia moja au hata Dream yetu na kujaza vifaa na waokoaji na kuwapeleka eneo la tukio? Kama hilo nalo lilikuwa gumu si wangepakia genereta kwenye boti na kuipeleka karibu na tukio na kuliwasha kupata mwanga? Hivi hata wangewaomba watu wa fiesta wawape yale mstaa yao si yangesaidia? Mimi sijaelewa kabisa! Sasa leo wanaokoa au wanaopoa?
 
Kuna video huko Instagram inatrend mbunge mmoja alitoa ANGALIZO kuhusu kivuko hicho na hakika imetokea, so [emoji17] maisha ya wapiga kura yamepotea.
Unaweza weka hyo vdeo hapo
Wengine insata gram hatukujui

Swaleh amesema nbonyeze reli ndo ntaingia ...nmebonyeza hadi kidole kinauma ... Sijaingia
 
Maxence Melo na Moderator sikuhizi JF imekufa kabisa kwenye live updates? Maana mpaka sasa ni zaidi ya miili 79 imepatikana lakini hakuna updates kwenye uzi. Nini tatizo? yaani kweli mnataka tusome comments zoote ndo tupate mwanga? Mmezuiliwa ku cover live events?
Mods tupo tunakunywa chai

Usitusumbue
 
Binafsi nimehuzunishwa sana na Maamuzi ya mkuu wa mkoa,hivi ni kweli zoezi la uokoaji linasitishwa sababu ya giza? Watu wanahangaika usiku kucha kutapatapa kutafuta msaada hadi wanajifia hakuna wa kuwasaidia kwa sababu ni usiku?hata karabai tu zingeweza kutumika,boti zikafanya doria angalau wale watu wanaotapa tapa wangeona mwanga wakaufuata na wakaweza kuokolewa!! So sad R.I.P masikini wenzangu mliotangulia!!!! Miili yenu najua itakuwa imeshasombwa na mawimbi ya usiku!
Mlikopeleka akili zenu nyie watu Mungu ndo anajua, hivi kwelikuna binadamu anaweza kukaa ndani ya maji tokea saa nae mchana hadi usiku akawa hai? anapumua kwa matamvua? kivuko kimepinduka karibuna ufukweni ho watu waliokuwa wakitapata usiku kucha uliwaona pekeako? according to you ni hekima kurisk uhai wa walio hai (waokoaji)ili kurecover maiti?!!! upuuzi wa hali ya juu.
 
Tuna flyover, reli ya umeme, barabara, etc.. we are on ze raiti traki. Tutembee vifua mbele
 
Back
Top Bottom