Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kwa kweli hawa wahusika wa kivuko ni wahuni sana.

Haiwezekani meli yenye capacity ya watu 100 ibebe watu zaidi ya 400.

Ukijaribu kuwaelimisha watakwambia katengeneze meli yako upande ujinafasi.

Hata kwenye madaladala watu wanajazwa nyomi kama siafu.

Kila kitu shithole.
Mkuu,
Kwa vijijini siku ya mnada najua unajua usafiri tunavyojazana. Ukizingatia wamiliki wanataka pesa tu bila kutoa elimu kwa abiria. Just imagine overloading ya watu na mizigo wakimbilie upande mmoja, yale yale ya MV Bukoba watu kukimbilia upande na kutoboa meli watoke kumbe ndo disaster.
Kwa ufupi hatujifunzi hata 2012 MV. Spice highlander.
Tunahitaji uwajibikaji kwa mamlaka husika.
 
Ni vyema yakatolewa majina ya waliokufa kwenye hiyo ajali maana kuna wengine hawana ndugu huko na ni watafutaji maisha tu walikuwa kwenye mapambano, hivyo yakitolewa majina itakuwa rahisi kwa watanzania wengi kujua, hii yakuita watu wakatambue ndugu zao mambo ya zamani sana..

Idadi ya majeruhi wanajulikana majina yao, Majina ya waliokuwa kwenye kivuko lazima yapatikane then unatoa hao majeruhi na yatakayobaki ndio watakuwa marehemu unayaprint kila mtu anayaona.
Sidhani hata kama kuna abiria hata mmoja aliyeandika jina lake wakati wa kupanda, hata idadi kamili ya watu unaweza usijue mana kuna tiketi zao na za serikali
 
Chadema wengi ni mambumbu, hajui kuwa mambo kama haya ndio huwa yanawapa credit ccm!

Wao wanafiki kupata credit kwa wananchi ni kuitisha mikutano au maandamano na kuanza kubwata hili na lile!

Majanga kama haya yanapotokea wananchi wanaona nani kaja kuwa pamoja nao! Sasa wewe endelea kuita ni ujinga.

Uzuri wenyewe hao wananchi wa sasa hivi wanauelewa wa kutosha, hakuna fala wa kwenda kumuuzia face wakati wanajua hela zinatumika kurudia chaguzi za kishenzi. Nani anashoboka na face ya mwanaccm wakati mbunge wao alishaongelea suala la kivuko huko bungeni?
 
Kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kumemlazimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri Denice James kusitisha ziara yake ya siku tano ya kukagua uhai wa Jumuiya na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020 katika maeneo yanayowahusu vijana ili kushiriki zoezi la uokoaji.
View attachment 873271
Mbona simuoni akiokoa au ndiyo kutafuta sifa kwenye msiba kisisiemusisiemu! Tutaona nguo za kijani zimejaa kando ya ziwa wakijisefii.
Tuelezwe ujuzi wake kwenye uogeleaji na uokoaji.
 
Ni vizuri huo ushauri na majina nadhani wanayo huko kwa wale wenye utambulisho watanzania wengi hatuna utamaduni wa kutembea na utambulisho na namba ya mtu wa karibu ili muda wote unaokuwa nnje ya nyumba yako au safari yoyote kikazi,ofisini uwe na ki card au karatasi umeandika sehemu utokayo na namba ya ndugu wa karibu maana emergency zipo hasa ajari na kuuguwa ghafla au kufa ....

Unapokata tiketi kwenye safari kama hizo lazima manifest isome jina lako, namba ya simu, immediate contact na unapotoka.
Nchi zilizoendelea wao huswap card ambayo inadetails zote za mwenye card.
Kwa Tanzania tunapaswa kuwa na manifest kama ile ya nyumba za wageni inayoeleza details za mtu ili ikitokea dharura iwe rahisi kutrack na kutambua, Mabasi ya mikoani Ubungo huwa tunaandika namba za simu na majina ila inabidi waongeze na hiyo ya immediate contact incase of emergency, Ulaya walianza hivi baada ya kuendelea ndio wanatumia Card yenye full details.
Mbona kwenye ndege watu hubeba ID au Passport, huu ni utamaduni lazima tuwe nao..
 
Chadema wengi ni mambumbu, hajui kuwa mambo kama haya ndio huwa yanawapa credit ccm!

Wao wanafiki kupata credit kwa wananchi ni kuitisha mikutano au maandamano na kuanza kubwata hili na lile!

Majanga kama haya yanapotokea wananchi wanaona nani kaja kuwa pamoja nao! Sasa wewe endelea kuita ni ujinga.
Kwa hiyo kivuko kikizama, Watanzania wakafa, serikali ya jiwe ikasitisha uokoaji na mwenyekiti wa uvccm akienda kuopoa maiti za Watanzania chama pendwa CCM kinapata credit dhidi ya CHADEMA?
 
Sidhani hata kama kuna abiria hata mmoja aliyeandika jina lake wakati wa kupanda, hata idadi kamili ya watu unaweza usijue mana kuna tiketi zao na za serikali

Ndio hapa tunapoongelea kila siku uwepo wa system imara itakayokuwa inasimamia mambo kama haya na kumaliza maujinga kama haya ili watu makini na maisha ya watu. Tuna mawaziri, makatibu, RC's ,DC's, DED, RAS nk woote hawa wanafanya nini kushindwa kusimamia mambo serious kama haya?
 
Mwaka 1996 MV Bukoba ilizama na kuua mamia ya raia, inasemekana chanzo kilikuwa ni kujaza abiria kupita kiwango.
Mwaka 2011, miaka 16 baadaye, Meli ya MV Spice Islander I ilizama, pia inasemekana ilibeba abiria na mizigo kupita uwezo wake.
Jana tena kivuko cha MV Nyerere nacho kimezama, pia tunaambiwa kilijaza abiria kupita kiasi.
Hivyo inaonekana pamoja na majanga yote haya, mamlaka zinazohusika zimeshindwa kudhibiti upakiaji wa abiria katika vyombo vya majini.
Mbona mabasi tunaweza kudhibiti, mbona kwenye ndege hakuna overloading? Kwa nini vyombo vya majini tunashindwa kudhibiti idadi ya abiria? Naamini kila chombo kinakuja na idadi ya abiria ambayo ni salama, kwa nini hazifuatwi? Watu wa TEMESA au SUMATRA wawajibike kwa kushindwa kudhibiti upakiaji wa abiria kwenye vyombo vya majini
Ifikie wakati tujifunze.
Yanapotokea majanga kwa mara ya kwanza inatakiwa ndio liwe fundisho la kubadili au kutunga upya kanuni za jambo husika.
 
Funny Enough mwezi huu wakaji Magufuli anazindua ujenzi wa meli mpya nilimsikiliza mwanzo mwisho.

Yule mkurugenZi wa mambo ya usafiri majini alikuwa kaimu na rais kamfanya awe kamili hapo hapo.

Rais aliwalaumu sana kwa uzembe na aka quote ule uzembe wa mv bukoba.

Rais alikuwa anaongea kwa uchungu sana tena sana.

Na akawaagiza waanzishe tiketi za electronics.
Aliwaambia anajua wanayoyafanya na aliwaasa waache upuZi na ujanja ujanja.

Nina uhakika kwa research yangu niliyoifanya. Tiketi zilizouzwa kihalali zilikuwa ni 70. Na magari mawili na mizigo basi.

Ila kivuko kilibeba watu zaidi ya mia nne.(imagine kivuko kina uwezo wa kubeba watu 101 ila wamezidi watu miatatu).

Tiketi zingine wahudumu walipiga pesa kwa ujanja ujana pamoja na kwamba rais mwezi huu aliidhinisha pesa za mishahara yao.

Jiulizeni walikaa zaidi ya miezi kumi hawalipwi mishahara sasa walikuwa wanaishije?

Ndio upumbavu kama huu.

Nashauri hawa jamaa wanyongwe.

Uzembe unaanzia kwa mkuu wa mkoa kushuka chini.
Wote ni wazembe askari wote walikuwa wanaona jinsi wananchi wanavyojazwa kwenye kivuko.

Shiriki la usafiri majini linasema eti haijulikani watu wangapi walikuwa kwenyw kivuko hicho.
Hili ni jibu kutoka kwa wataalamu ambao wamesoma na wanasimamia rasilimali zetu.
Kudos
Hatujifunzi kabisa mkuu ya 1996, 2012 Zanzibar.
Kama basi la abiria tu majina yanaandikwa kuhifadhi kumbukumbu za abiria leo kivuko cha majini SUMATRA hawana rekodi ya idadi wala majina ya abiria.
Yaani ni uzembe mkubwa sana.
Wamiliki wa vyombo wazembe sana.
Mbona ATCL hawazidishi abiria, jibu ni kwamba usafiri majini umejaa non professional personnel ambao hawajui au wana makusudi.
Kutoa elimu ya usalama kwa abiria awapo majini napo hakuna.
Watu 400 wamezidi na wakimbilie upande mmoja kwa sababu hakuambiwa risk za kufanya hivyo kabla ya safari.
Yaani nchi zetu hizi ni tupo Ujima.
 
Unapokata tiketi kwenye safari kama hizo lazima manifest isome jina lako, namba ya simu, immediate contact na unapotoka.
Nchi zilizoendelea wao huswap card ambayo inadetails zote za mwenye card.
Kwa Tanzania tunapaswa kuwa na manifest kama ile ya nyumba za wageni inayoeleza details za mtu ili ikitokea dharura iwe rahisi kutrack na kutambua, Mabasi ya mikoani Ubungo huwa tunaandika namba za simu na majina ila inabidi waongeze na hiyo ya immediate contact incase of emergency, Ulaya walianza hivi baada ya kuendelea ndio wanatumia Card yenye full details.
Mbona kwenye ndege watu hubeba ID au Passport, huu ni utamaduni lazima tuwe nao..
Sawa sawa ile sehemu ya dharura ndo muhimu kwa contacts kuliko zote ..... mimi nilikuwa na wazo labda kama kitambulisho cha taifa kinakuwa na chip ambayo sehemu kama airport,stand za magari,stesheni kwa train,bandalini au kwenye vivuko kunakuwa na mashine una swap inarecord mtu fulani anaenda kuboard unalipa unakwenda na usafiri unao tumia ukifika unaswap umetoka inakuwa na in and out ....hii ingekaa poa kwa kutumia kitambulisho cha taifa na wasio kuwa navyo as hao below 18 wanatumia manual normal receipt
 
Hawa ccm wanatia hasira sana maana wakiambiwa matatizo kama ya meli chakavu wanapiga risasi wapinzani
 
Ni vyema yakatolewa majina ya waliokufa kwenye hiyo ajali maana kuna wengine hawana ndugu huko na ni watafutaji maisha tu walikuwa kwenye mapambano, hivyo yakitolewa majina itakuwa rahisi kwa watanzania wengi kujua, hii yakuita watu wakatambue ndugu zao mambo ya zamani sana..

Idadi ya majeruhi wanajulikana majina yao, Majina ya waliokuwa kwenye kivuko lazima yapatikane then unatoa hao majeruhi na yatakayobaki ndio watakuwa marehemu unayaprint kila mtu anayaona.
Mkuu
Hakuna rekodi ya watu walioingia. Naskia ni kupanga tu mstari unaingia chomboni.
Ukisikia statistics za 400 (yaani takwimu za sufuri mbele) huwa ni makadirio ya siyo na uhalisia.
Pathetic agencies!
 
Back
Top Bottom