Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kudos!
Yaani nadhani hata adui akitushambulia usiku kupitia ziwa Victoria tutasema hatuna taa ya kumlika kufanya mashambulizi.
Ina maana Mwanza hatuna Navy force yenye boti na vifaa vya uokozi?
Jeshi letu la wanamaji hawawezi ku respond kwa catastrophe kama hii, sasa tutakuwa tayari lini?
Tunasubiri South Africa watuletee wanamaji kuokoa kama walivyofanya miaka 22 iliyopita??
Yaani hatupo tayari kwa disaster yeyote.
Adui mwenyewe atokee wp .....
Kenya ama Uganda....???
 
..una uhakika gani kama hizo "injini mpya" hazikuwa na matatizo?

..na pia kivuko kuwa na "injini mpya" haimaanishi kwamba hakina matatizo ktk maeneo mengine.

..kwa maoni yangu it is too early kujua chanzo cha ajali hiyo ni nini.

..Uchunguzi huru wa kitaalamu unatakiwa kufanyika kubaini kivuko kilipatwa na matatizo gani na kupelekea kizame/kupinduka.

Hehima kwako mkuu.

Nilikuwa naelewa ukiniona utakuja hapa, safi sana.

Sasa bila shaka unafahamu jinsi utaratibu ulivyo wa abiria kupata nafasi ya kupanda vivuko kama hivi.

Kwanza, kulikuwa na gulio hivyo watu wengi walitaka waende gulioni.

Pili, wasimamizi wakaingiwa hamasa ya kujaza abiria hivyo initial estimate ni zaidi ya abiria 300.

Tatu, wasimamizi wa kivuko ni miongoni mwa walozama na vifaa vyote muhimu vinavyohusiana na kukata tiketi na ambao mengine vimezama majini.

Hivyo "vital evidence" imepotea lakini taarifa zinakwenda Reuters na vyombo vingine vilivyopo pale vinaelewa namna ya kupata habari kwa uhakika.

Nne, kivuko ni kizima na hakikuwa na kasoro ya kukiwezesha kuzama zaidi ya kujaza abiria wengi kupita kiasi.

Kilichobakia ni kuomba wale vijana wenye simu zao ambao walikuwa ng'ambo wakirekodi tukio.

Hivyo hapo ndo tunawaachia polisi.
 
..mimi nadhani tumlaumu Mbunge wa Ukerewe anayetokea chama cha Chadema.

..kwanza, alipiga kura kukataa bajeti ya wizara ya uchukuzi.

..Mbunge alitegemea serekali itatoa wapi fedha za kununua au kukarabati vivuko?

..Pili Mbunge anapata milion 58 kila mwaka kwa ajili ya mfuko wa maendeleo. Angetumia fedha hizo kukarabati kivuko huenda ajali hii isingetokea.

Cc tindo
Unajua matengenezo yaliyotakiwa yalihitaji fedha kiasi gani??
 
Bajeti ya kununua hivo vivuko inapitishwa na wanasiasa.
Matengenezo yanategemea msukumo wa wanasiasa.
Usimamizi unategemea wataalamu na wanasiasa.
Hilo eneo lilihitaji zaidi ya kivuko kilichozama, pia ilihitaji wanasiasa wafanye maamuzi,
Vifaaa vya uokozi kwa jeshi la polisi na majeshi mengine yanahitaji wanasiasa wapitishe bajeti

Unatenganisha vipi siasa na matukio ya kizembe kama haya iwapo kina watu wanapaswa kuwajibika?

Mkuu wa Mkoa awajibike
Waziri wa uchukuzi awajibike
Polisi wawajibike kwa uzembe
SUMATRA wawajibike
Kivuko kina zama umbali wa mita 50 kabla ya kutia Nanga majira ya saa 8 uokoaji unaanza rasmi saa 12
 
Bwana Panzi na Jongoo, acha kubwabwaja bwabwaja kama hayawani.

Wavuvi huvua usiku.Kwa umri wako hujawahi kuona taa inayoitwa KARABAI?

View attachment 873423

Nenda kwa wavuvi waombe wakuoneshe karabai ikiwashwa usiku inakuwaje halafu rudi uje kubwabwaja.

View attachment 873428
Mwanga Wa karabai huwezi penya ndani ya maji wenyew unasambaa nje ya maji ndio maana dagaa wanaibuka kuufata, kama ungekuwa unafucha chini ya maji dagaa wasinge ufata juu,,,,pia hiyo spotlight ya helicopter nadhan ingekuwepo ingefanya kazi, nadhani ni suala la uelewa mcwe n mawazi ya funza
 
..mimi nadhani tumlaumu Mbunge wa Ukerewe anayetokea chama cha Chadema.

..kwanza, alipiga kura kukataa bajeti ya wizara ya uchukuzi.

..Mbunge alitegemea serekali itatoa wapi fedha za kununua au kukarabati vivuko?

..Pili Mbunge anapata milion 58 kila mwaka kwa ajili ya mfuko wa maendeleo. Angetumia fedha hizo kukarabati kivuko huenda ajali hii isingetokea.

Cc tindo
kwahio unamaanisha alipiga kura kukataa bajeti na bajeti haikupita hvyo kupelekea kukosekana kwa pesa ya kukarabati hcho kvuko? mi navyofaham bajeti ilipita labda utafute nyngne ya kumhusisha huyo mbunge wa chadema, nyie lumumba akili zenu mnazijua wnyw
 
Ndo muanze kudai mnunuliwe meli na boti za uhakika.
Sio mnanunuliwa ndege mnashangilia.wakati wanaopanda wengine.
Nyie mnapanda boti chakavu.
 
Adui mwenyewe atokee wp .....
Kenya ama Uganda....???
Just thinking loudly.
Unadhani hao hawawezi host wahalifu. Kama Idd Amin alijaribu unadhani hakutakuja marais vichaa kati ya majirani asiyeheshimu mipaka itakuwaje.
Au mpaka itokee?
 
Nimesikitika sana kusoma kwamba sababu ya kivuko kupinduka ni abiria kukimbilia upande mmoja ili wawahi kushuka kivuko kikitia nanga, hivyo kupelekea kivuko kuzama. Abiria wanatakiwa kupewa elimu ya jinsi uwiano wa uzito ulivyo muhimu kwa kivuko kuelea majini.Nashauri kwenye vivuko kuwe na "vessel attendants" kama ilivyo kwa "flight attendants" kwenye ndege ambao kazi yao ni kuelekeza abiria nini cha kufanya waingiapo kivukoni, wakati gani wa kuanza kujiandaa kushuka, kuonyesha jinsi ya kuvaa boya(maybe thru a tv screen)n.k. Hii ajali insingetokea iwapo kungekuwa na watu wa kuwazuia/elekeza abiria kusubiri walipo hadi kivuko kitie nanga.
Anyway, yameshatokea. Nawapa pole wote walioguswa kwa karibu na maafa haya.
RIP marehemu wote.
Kama kweli sababu ni hii basi ni uzembe wa operators! Kiviko kinaponunuliwa huwa kinakuja na safety operating procedures ambazo ni LAZIMA zifutwe kila siku bila kuzembea.
 
Yani huyu anaetoa matamko sijui anafikiria kwa kutumia matako?? Hivi untuambiaje ikifika saa 12 jioni zoezi la uopoaji litakuwa limesitishwa rasmi ana uhakika gani wa kuwapata masalia wote 232 walibakia???? Ukifikiria sana unawaza kukufuru Mungu bure
 
Hivi, unafahamu kwamba kuna vyanzo vya uhakika vinasema kwamba abiria walokuwamo humo kwenye kivuko ni zaidi ya 200?

Na pia hakuna anaefahamu zaidi ikwamba inawezekena abiria wakawa zaidi ya 400 aana wengi walokuwa wakienda gulioni?

Sasa waziri wa uchukuzi anaingiaje hapo?

Cha msingi ni kwamba kivuko ni kizima na hakikuwa na kasoro yoyote ile kwani hivi karibuni kilipata injiini mbili mpya.

Suala linaanzia kwenye msimaizi wa hicho kivuko ambae anasimamia kwamba ni tiketi ngapi ziuzwe na abiria wangapi waruhusiwe kuingia kwenye kivuko.

Hivyo usimamizi kwamba kivuko kinabeba uzito upi, namba ya abiria, mizigo na korokoro zingine si jukumu la waziri.

Hilo ni jukumu la wasimamizi wa kivuko ambao ndo wanapaswa kuwajibishwa.
Tunapoongelea mambo ya uhai wa watu tuwe tunaacha kidogo pembeni mambo ya unafki na kutafuta kiki au kujitetea kusiko na msingi.Bhasi tuassume waziri hausiki directly na ajali lakini tumuongelee waziri indirectly

1.Waziri ndio huwa anapeleka bungeni bajeti je alikua hajui kwamba katika wizara yake kuna vifaa na wataalamu wa uokoaji wamepungua au hawapo?,au hizo bajeti anazopeleka bungeni ni kwaajili ya posho na ziara za kushtukiza pamoja na makamera?

2.Waziri amefanya juhudi gani kujaribu kuwaokoa majeruhi wa ajali hii maana ajali imetokea saa nane mchana lakini mpaka usiku walifanikiwa kuwaokoa watu 37 na maiti 44,Je waziri hakuona umuhimu wa kupangua bajeti yake ili awezeshe zoezi kuendelea mpaka usiku maana toka ajali imetokea walikua na uhakika kwamba wanaweza wasimalize kazi ya uokoaji kwa mwanga wa jua.Je waziri hapaswi kuwajibika kwa kutokutoa bajeti ya emergrnce ili kazi ya uokoaji ifanyike mpaka usiku?

Tuache unafki wa kuunga juhudi
 
Wakijiuzulu watoto wao utawalipia karo na kuwapa chakula?

Mkuu Tanzania Uongozi ni biashara kama biashara nyinginezo. Uwajibikaji ni sifuri. Ndo maana wakiteuliwa wanafanya sherehe na kuiba. Hakuna kitu kama kuhudumia wananchi.

The sad part of it, hao hao viongozi kesho watakuja kuomba kura kwa kutumia hicho kivuko kama mtaji. NA wananchi walivyo na akili nyingi watawachagua kwa kishindo!

Africa bado tuna safari ndefu sana!
Ndio kusema uongozi kwa Tanzania ni ajira? Nje ya uongozi ni kulala njaa?

Napenda sana aina ya viongozi wa Kenya; wengi wanatafuta uongozi kwa ajili ya kujenga jina na si kipato
 
Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata. Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko. Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!! Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika. Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa? Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe. Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
Huo ni uzembe, usituletee ujinga wako hapa
 
Mwanga Wa karabai huwezi penya ndani ya maji wenyew unasambaa nje ya maji ndio maana dagaa wanaibuka kuufata, kama ungekuwa unafucha chini ya maji dagaa wasinge ufata juu,,,,pia hiyo spotlight ya helicopter nadhan ingekuwepo ingefanya kazi, nadhani ni suala la uelewa mcwe n mawazi ya funza
Ipo siku yako, kwa sasa hakuna lugha unaweza elewa. Hiyo siku ikifika, utaiona posibility ya mtu kuogelea na mkono mmoja huku wa pili kashika mshumaa
 
Back
Top Bottom