Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!

Seriously kama hujalewa basi una matatizo makubwa ya akili!!!
 
Tunapoongelea mambo ya uhai wa watu tuwe tunaacha kidogo pembeni mambo ya unafki na kutafuta kiki au kujitetea kusiko na msingi.Bhasi tuassume waziri hausiki directly na ajali lakini tumuongelee waziri indirectly

1.Waziri ndio huwa anapeleka bungeni bajeti je alikua hajui kwamba katika wizara yake kuna vifaa na wataalamu wa uokoaji wamepungua au hawapo?,au hizo bajeti anazopeleka bungeni ni kwaajili ya posho na ziara za kushtukiza pamoja na makamera?

2.Waziri amefanya juhudi gani kujaribu kuwaokoa majeruhi wa ajali hii maana ajali imetokea saa nane mchana lakini mpaka usiku walifanikiwa kuwaokoa watu 37 na maiti 44,Je waziri hakuona umuhimu wa kupangua bajeti yake ili awezeshe zoezi kuendelea mpaka usiku maana toka ajali imetokea walikua na uhakika kwamba wanaweza wasimalize kazi ya uokoaji kwa mwanga wa jua.Je waziri hapaswi kuwajibika kwa kutokutoa bajeti ya emergrnce ili kazi ya uokoaji ifanyike mpaka usiku?

Tuache unafki wa kuunga juhudi
Mkuu wa mkoa ndo AMEONEKANA zaidi katika vyombo vya ahabari vya ndani na nje kuliko Waziri wala msaidizi wake.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Anahitaji pongenzi sana kwa juhudi alizojaribi kumobilize uokoaji.
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
Naniliu yuko huko?
 
Huyo mwenyekiti wenu mnamficha wa nini? Au mnaona haya vile hajafika huko pamoja na kabineti yake ndio mnatafuta pa kujificha? Oneni aibu hivyohivyo na msijifiche nyuma ya mbowe kufikisha ujumbe wenu. Pelekeni kama ulivyo na uliza kulikoni hatukuoni huku? Wajinga na waoga kuliko mbwakoko lumumba st!
Maneno mengi ya nini sasa?
 
Swali la kipuuzi sana hili.
Ulitakiwa uulize
1)Ni kwa nini matukio haya yanaendelea kutokea tena na tena miaka 22 baada ya kuzama MV bukoba?
2)Kwa nini hii ajali imetokea?Ilikuwa haizuiliki?
3)Katika Karne ya21,Kwani uokoaji usitishwe kwa sababu kuna giza?
4)Kwa nini haijulikani hadi sasa ni watu wangapi walikuwepo?
Bado kuna uzembe mkubwa hivi hata wa kutunza kumbukumbu za abiria?Ni nani alipaswa kujua idadi halisi ya abiria
5)Kama taifa tunajua vipaumbele vyetu? Tunawezaje kununua ndege kwa mabilioni ya pesa kwa ajili ya watu wachache,huku tukishindwa kuboresha usafiri wa majini unaotumiwa na ni tegemeo la wananchi wengi?

Ya Mbowe yaache kwanza sio muhimu kwa sasa,hawajibiki kwa chochote hapa,kuna watu waliopewa mamlaka ya kukusanya kodi zetu,tuanze na hao.
Mjadala uendelee.
 
Si utani ngoja nikutajie listi

1. Kingunge alitembelewa mwishowe akavuta

2. Maria na Consolata mwishowe akavuta

3. Samuele Sita mwishowe kavuta

4. Yule aliyechora nembo ya taifa mwishowe kavuta

5. Mzee Majuto naye alivuta

6. Mzee mmoja wa CCM (jina nimelisahau) naye kavuta

7. Wengine niliowasahau nao wamevuta

Yaani hawaponi kabisa!

Duh nimeaanza kumuogopa kwa kweli ata nikiumwa nikimsikia anakuja ntakimbia na dripu zangu maana maisha matamu
Daah...!!
 
Mods mmeleta huu uzi huku

Hivi mko serious kwan hili ni jambo la kisiasa

Achen hizo mnazingua wakuu
 
Vijana wa Lumumba kuweni na busara na huruma kwa hao waliofariki mnaleta mzaha kweli?
 
Acheni kuleta siasa kwenye maisha ya watu. Huu upumbavu wa CCM na Chadema unaanza kukera, kuweni na mipaka.
 
Kwa nini Amiri jeshi mkuu asiwepo Ukerewe awe anasaidia wanajeshi wanaofanya uokoaji?

Kwa nini rais asiwepo Ukerewe akawafariji 'wapiga kura wake'??


Mngemsikiliza Mkundi kuhusu kivuko cha Mv Nyerere sasa hivi tungekuwa hatuna msiba wa taifa.

Majimbo ya watoto wa kambo (wapinzani) hayapelekewi maendeleo hadi kina ccm yapate maendeleo
 
Mbowe anahusika nini hapa?! Au unataka kutumia “ubaya” wa Mbowe kuhalalisha kutowajibika kwa wanao takiwa kuwajibika ishu ya kivuko??!!
Ilikuwa on a lighter note si zalau ila ni/KUCHEKA KIDOGO!
Samahani mkuu.
 
Hivi vivuko vinabeba sana kupita uwezo wake sio hicho tu kuna vivuko vinabeba mizigo na watu hadi vinakema.

Usimamizi na umakini unatakiwa kwenye vivuko vyote nchini, pia sijajua kama MV Nyerere haikuwa na maboya.



Maboya hata yakiwepo sidhani kama yanatosha kwahivyo wanavyozidisha idadi ya watu. Hata hivyo unakuta yamefungwa kwa pamoja badala ya kugawia watu wavae kabla ya kuanza safari.
 
Back
Top Bottom