Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Zitaliwa, msitoe. Waombeeni tu waliofiwa, waliokufa , majeruhi Mungu awape kila lililo jema kwa kila kundi. Mambo ya rambi rambi achana nayo, zitaliwa au kupelekwa kusikojulikana.
Mungu wasaidie wote kwa faraja inayowafaa. AMEN
Hela ya tetemeko imetuvunja moyo sana !
 
Kwani Jimbo la Ukelewe lina Mbunge wa chama gani? "AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO MBAYUWAYU"
Mbona mnataka kuleta siasa mpaka misibani, sasa mbunge angekuwa wa chama kingingine angezuia ajali isitokee.
 
Jamaa yupo magogoni anazisubir rambirambi aanze kuzila badala ya kwenda ukerewe
 
Msiba wa MV Nyerere umepoteza watu zaidi ya 137 ( kizembe zembe kabisa ). Hakika ni msiba mkubwa sana. Ila sasa ni lazima hawa marehemu waondoke na watu wengine walio hai hapa duniani. Lazima wawajibike.

Niipongeze serikali imeanza kuchukua hatua.Mh. Rais tayari kamtuma Waziri Mkuu huko Mwanza.Nawapongeza sana.


Bendera zitapepea nusu mlingoti kwa siku 4 . Sijajua kama kazini hatuendi. Na kama ndivyo sijajua mshahara wa mwezi huu utatoka lini maana utaathirowa na siku ya j3 ( watu hawatafanya kazi ipasavyo ).

RIP kwa wote.

Tuje kwenye mada: TBC1 na maombolezo :-



TBC 1 wamekuwa wakiomboleza misiba ya kitaifa kwa nyimbo za dini ( za kila aina ) muda karibu wote wakiwa hewani.

Kwa kuwa Channels zingine kama ITV , Star TV, etc zilipata pata shida hivi karibuni… tumekuwa watu wa kukomaa na TBC 1 tu muda mwingi.

Maombolezo maombolezo maombolezo TBC 1 kila sekunde, kila dakika ukiwasha runinga yako!
 
Swali la kipuuzi sana hili.
Ulitakiwa uulize
1)Ni kwa nini matukio haya yanaendelea kutokea tena na tena miaka 22 baada ya kuzama MV bukoba?
2)Kwa nini hii ajali imetokea?Ilikuwa haizuiliki?
3)Katika Karne ya21,Kwani uokoaji usitishwe kwa sababu kuna giza?
4)Kwa nini haijulikani hadi sasa ni watu wangapi walikuwepo?
Bado kuna uzembe mkubwa hivi hata wa kutunza kumbukumbu za abiria?Ni nani alipaswa kujua idadi halisi ya abiria
5)Kama taifa tunajua vipaumbele vyetu? Tunawezaje kununua ndege kwa mabilioni ya pesa kwa ajili ya watu wachache,huku tukishindwa kuboresha usafiri wa majini unaotumiwa na ni tegemeo la wananchi wengi?

Ya Mbowe yaache kwanza sio muhimu kwa sasa,hawajibiki kwa chochote hapa,kuna watu waliopewa mamlaka ya kukusanya kodi zetu,tuanze na hao.
Mjadala uendelee.
Mbwiga hapa namzungumzia Mbowe kama KUB...........siyo yule wa Bills use unaelewa!
 
Kwa nini Amiri jeshi mkuu asiwepo Ukerewe awe anasaidia wanajeshi wanaofanya uokoaji?

Kwa nini rais asiwepo Ukerewe akawafariji 'wapiga kura wake'??


Mngemsikiliza Mkundi kuhusu kivuko cha Mv Nyerere sasa hivi tungekuwa hatuna msiba wa taifa.

Majimbo ya watoto wa kambo (wapinzani) hayapelekewi maendeleo hadi kina ccm yapate maendeleo
Nampongeza Mwita Waitara kwa kufanya maamuzi sahihi!
 
Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata.

Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko.

Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!!

Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika.

Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa?

Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe.

Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina ju u ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.
Acheni kukandamiza maoni mbadala.Hivi kukosekana uokoaji kwa zaidi ya masaa sita huku jeshi,polisi,zimamoto vikiwepo ni siasa?.Hivi kusitisha uokoaji na kusubiri uopoaji ni siasa?.Tunahaki ya kulinganisha umakini wa serikali kwenye ziara za Rais,Uchaguzi,mikutano au matukio ya wapinzani na hili la maafa
 
Umeshapanic!!.......Ukerewe ni jumbo linaloongozwa na mbunge wa Chadema mbona hamumpi ushirikiano. Mbona wakati Sugu anatoka jela KUB alikuwepo!
Wewe nakufundisha kila wakati jinsi ya kujenga hoja lakini una kichwa kigumu kisichoelewa kama chama unachoshabikia! Kwanini uwabague waliopoteza ndugu zao kwa uzembe wa serikali kwa kutumia itikadi za vyama?
Hivi ninyi ccm, ni lini mtaacha kuitumia misiba kama uwanja wa siasa zenu za kibaguzi?
Au maana yenu ni kuwa raia akiwa na itikadi tofauti anapoteza uraia wake? Hebu acheni siasa hizi za kijinga za kibaguzi kwani hazitujengi na kutuunganisha katika kuwafariji waliopoteza ndugu zai badala yake zinatufanya tuonekane mahayawani mbele ya majirani zetu na watoto wetu ambao wanatakiwa kujifunza kwetu! Badilikeni ccm!
 
Anaongea Leo alikuwa wapi siku zote mbili hizi
Lazima liongelewe kisiasa kwani pesa za kununua ferry na mengineyo kwa ajili ya maendeleo ya walipa kodi mnarudia chaguzi zisizo na tija
Hapa huchomoki hata usemeje
Haya sasa mnaanza kuunda tume watu wale posho za bure badala ya kurekebisha miundo mbinu
Hii nchi imelogwa kupitiliza
Siasa mumo kwa mumo mpaka muwaelewe walipa kodi na dharau zenu
 
haisaidii hata ikiwekwa chini ya mlingoti
Ndugu yangu kuomboleza ni MILA NA DESTURI, DUNIANI KOTE, hata Marekani kila mwaka ikifika September 11, wanaombieza "Airplane bomming of WTO!!??!!, Kwahiyo Serikali yetu kupeperusha nusu Mlingoti ni ishara ya kuomboleza kwa wa Tz waliofariki ajalini, kwenye majanga kama haya usiingize itikadi za Vyama!!!??!
 
Dak mbili tu kwa mtu wa kawaida hazimalizi ndani ya maji sembuse masaa 24? mnashangaza sana. Hata kama waokoaji wangepeleka kwa chop maafa bado yangekuwa yaleyale tu maana chombo kilipinduka suddenly na kufunika watuna dakika 10hata daiva mzoefu hamalizi nani ya maji lazima afariki maana hatumii gills kupumua, lawama nyingine za kipuuzi kabisa.
Watu 40 wameokolewa. Kama waokoaji wangekuwa na akili kama zako basi baada ya dakika 25 tuu wangetangaza watu wote waliokuwa kwenye kivuko wamekufa.
 
Wewe nakufundisha kila wakati jinsi ya kujenga hoja lakini una kichwa kigumu kisichoelewa kama chama unachoshabikia! Kwanini uwabague waliopoteza ndugu zao kwa uzembe wa serikali kwa kutumia itikadi za vyama?
Hivi ninyi ccm, ni lini mtaacha kuitumia misiba kama uwanja wa siasa zenu za kibaguzi?
Au maana yenu ni kuwa raia akiwa na itikadi tofauti anapoteza uraia wake? Hebu acheni siasa hizi za kijinga za kibaguzi kwani hazitujengi na kutuunganisha katika kuwafariji waliopoteza ndugu zai badala yake zinatufanya tuonekane mahayawani mbele ya majirani zetu na watoto wetu ambao wanatakiwa kujifunza kwetu! Badilikeni ccm!
Jibu swali, kwanini mmemtenga mbunge Mkundi?
 
Back
Top Bottom