Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Lile zuio la kutokutoka dar bila kibali maalum mmelisahau???

Mbowe ndio mwenye kikosi cha uokoaji???

Yule aliegonga twiga mlikimbizana usiku na mchana na machopa Leo hawa mnakosa taa za kuwaokolea ???


Vichaa on fleek
umeona takataka with mavi reasoning johnthebaptist
 
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi alipokuwa anatoa taarifa ya Serikali na kuwa bendera itaanza kupepea nusu mlingoti kuanzia Kesho Septemba 22-Pia, Rais ameagiza viongozi wa Taasisi na Mamlaka zinazosimamia usafiri wa majini wahojiwe, watakaobainika kuhusika kwa uzembe wachukuliwe hatua kali-Aidha, Mkuu wa Polisi Simon Sirro amesema idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo hadi sasani 136
Postmortem.Mbwembwe nyingi kwenye uopoaji wa maiti badala ya uokoaji wa watu.Shame shame shame
 
Kwani tatizo lilitokana na ubovu wa kivuko au makosa ya kibinadamu?


Makosa ya kibinaadamu hayana njia ya kuzuia ?

Idadi ya abiria kutojulikana ndo inanisikitisha inamaana ticket hazijulikani zilikatwa ngapi na sio za EFD kweli watu bado watakua wanapiga tu.

Mkuu hata Mkulu mwenyewe kwenye ziara alisema anawajua vizuri....kuna watu bado wanapiga ile mbaya, angalia idadi ya watu waliopanda kivuko mpaka leo kila mmoja anakuja na idadi yake
 
Hili Sakata lazma litaondoka na mtu tu mana kuna harufu ya uzembe mwingi mnooo
 
Unachanga ili zifanye nini? tuanzie hapo. let be logical in our reasoning, siyo matusi.
Kwani wewe umesema tusichange nini, aliemtukana mwenzie na kumwita fisi mbona hujamuuliza hilo swali, acheni mambo ya hovyo katika hiki kipindi cha majonzi ,
 
Zitaliwa, msitoe. Waombeeni tu waliofiwa, waliokufa , majeruhi Mungu awape kila lililo jema kwa kila kundi. Mambo ya rambi rambi achana nayo, zitaliwa au kupelekwa kusikojulikana.
Mungu wasaidie wote kwa faraja inayowafaa. AMEN
Msithubutu kabisa.Kama haina kazi nipigie nikuelekeze uifanyie nini hiyo hela.Kwani yeye ndo amekizamisha Bwana?
 
Zitaliwa, msitoe. Waombeeni tu waliofiwa, waliokufa , majeruhi Mungu awape kila lililo jema kwa kila kundi. Mambo ya rambi rambi achana nayo, zitaliwa au kupelekwa kusikojulikana.
Mungu wasaidie wote kwa faraja inayowafaa. AMEN
sio kwamba wasitoe RAMBIRAMBI ishu wapeleke RAMBIRAMBI kwa familia husika...na sio kenge yeyote aliyejiamulia kukusanya
 
Moja ya sababu alizozitaja rais za kumwondoa Mwigulu ni ajali zisizoisha na yeye kutuma rambi rambi peke yake bila Mwigulu naye kutuma.

Baada ya hapo akamteua Kangi Lugola anayejiita Ninja. Ninja akaingia na majigambo na makeke.kibao kuwa sasa ajali basi na rais atapumzika kutuma rambi rambi. Muda si muda makamanda wa polisi wakahamishwa hadi RC wa Mbeya akahamishwa kutokana na ajali nyingi kutokea mkoani kwake.

Kana kwamba hiyo haitoshi.kukaitishwa maombi ya dini mbali mbali na matambiko ya kiasili barabarani ili kuzuia ajali. Kitendo hiki kilifanywa na watu wasomi wengine wakijiita madokta. Huo ndio waliona ndiyo muatobaini wa kumaliza ajali Mbeya.

Haujapita muda.toka mabadiliko na matambiko yao ajali zikaanza kutokea tena na nyingine kubwa zaidi. Rais aliyesema amechoka kutuma rambi rambi akainua kalamu tena na kuanza kutuma rambi rambi lakini wakati huo huo Ninja hakutuma. Sasa imetokea ajali kubwa sana ya kupinduka kwa.MN NYERERE ambapo zaidi ya watu 130 wamepoteza maisha. Rais ameinua kalamu tena kutuma.rambi rambi wakati waziri wa mambo ya ndani akiwa ni ninja aliyeingia kwa majigambo na makeke mengi hadi kuwafukuza wadaidizi wake muhimu kwenye vikao.

Swali kubwa ni kuwa imekuwaje tena pamoja na mabadiliko hayo yaliyojaamikwara miiingi, matambiko na kejeli dhidi ya waziri aliyepita ajali zinaendekea kutokea? Kilichofanyika ni kulaumu tulipoangukia badala ya tulipojikwaa.
 
Leo ndio tunaona mie ricopta na miboti ya polisi nayo yamebeba viongozi tu wa polisi na wa kiserikali Huku waokozi wakiwa kwenye mitumbwi.
 
Pole kwa familia, ndugu na watanzania wote kwa kuondokewa na wapendwa wetu.
Pia serikali ijitahidi kuwa makini na vyombo hivi ajali zimekuwa nyingi sana nchini.
 
Back
Top Bottom