A
Anonymous
Guest
Wakazi wa Kijiji cha Bwisya, Kata ya Ukara, Wilaya ya Ukerewe, tuna changamoto mbili kubwa, kuna Kampuni inaitwa JUMEME inayotoa huduma ya umeme wa jua (solar system). Wakati inaanza huduma tuliahidiwa umeme utakuwepo kwa Saa 24, iwapo jua halitakuwepo, watatumia jenereta ili tusikose huduma.
Ajabu, iwe kuna jua au hakuna, umeme unakatwa mara kwa mara, kuanzia Saa 3 au 4 usiku, unarudi siku inayofuata Saa 5 Asubuhi au Saa 6 Mchana. Ikifika Saa 9 au Saa 10 Jioni wanakata tena mpaka Saa 1 au Saa 2 Usiku.
Jambo la kushangaza zaidi, akitokea kiongozi yeyote anayetembelea Ukara, umeme haukatwi kabisa au unakatwa kwa saa moja au mawili tu hata kama hakuna jua.
Pia, wasimamizi wa umeme huu inaonekana wana ubaguzi wa kishabiki, Timu ya Simba ikicheza hawakati lakini Yanga ikicheza wanakata huduma, hii inaonyesha wazi kuwa wanafanya makusudi. Mamlaka zipo, hususan Meneja wa TANESCO wa Wilaya, lakini hakuna anayefuatilia, Wananchi tunateseka sana.
Aidha, hivi karibuni wamekuwa na tabia ya kukata na kurudisha umeme mara nyingi kwa usiku mmoja (hata mara 10), jambo linalounguza vifaa vyetu vya ndani. Ukijaribu kuhoji, wasimamizi hao wanakuwa wakali sana.
Umeme wa Shilingi 5,000 unapata Unit 2 tu hiyo ni sawa na Shilingi 2,500 kwa Unit moja. Tunalipa gharama kubwa sana lakini huduma hatupati ipasavyo, hali hiyo inasababisha mawasiliano kuwa shida kubwa katika Vijiji vya Bwisya, Bukiko, Kome, Chifule na Chibasi.
Pamoja na kwamba minara ipo, Mtandao hakuna na Mtu anaweza kukupigia simu asikupate kabisa.
Serikali ingeelekeza fedha zinazotumika kununulia vitendeakazi kama pikipiki na baiskeli katika kutatua tatizo hilo kwa kutuletea umeme wa TANESCO, kwani hilo linawezekana.

=====================================
Ufafanuzi wa TANESCO 👇
Mimi ni mkazi wa Mwanza, Wilaya ya Ukerewe, Kata ya Ukara, Kijiji cha Bwisya. Kuna changamoto mbili kubwa huku kwetu, naomba utusaidie kupaza sauti, kuna kampuni inaitwa JUMEME inayotoa huduma ya umeme wa jua (solar system).
Wakati wanaanza kutoa huduma hii, waliahidi kuwa umeme utakuwepo saa 24, na iwapo jua halitakuwepo, watatumia jenereta ili tusikose umeme.
Cha ajabu, iwe kuna jua au hakuna, umeme unakatwa mara kwa mara. Wanakata umeme saa 3 au saa 4 usiku, na unarudi siku inayofuata saa 5 au saa 6 mchana. Ukirudi, ukifika saa 9 au saa 10 jioni wanakata tena mpaka saa...