Ukarabati MV Victoria, MV Butiama waridhisha

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552


Mwenyekiti wa Bodi ya Tasac, Profesa Thadeo Sata, alitoa taarifa hiyo alipozungumza na waaandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa meli hizo zinazotegemewa kuanza safari mwezi Machi, 2020. Prof. Sata alisema lengo la ziara hiyo iliyoongozwa na uongozi wa kampuni ya meli MSCL ni kuhakikisha viwango vinavyohitajiwa kwa usalama wa vyombo hivyo katika kuvikarabati vinakuwa sawa.

Naye msimamizi wa miradi hiyo kutoka kampuni ya meli Mhandisi Abel Gwanafyo, alisema ujio wa bodi hiyo ni faraja kwao na kwamba watahakikisha kuwa wanafanyia kazi yale yote waliyowaelekeza.

"Viongozi hawa wamefanya ziara Kanda ya Ziwa katika kutekeleza moja ya jukumu lao kubwa la kuhakikisha kuwa viwango vinavyohitajika kwa usalama vinakuwa salama," alisema. Mhandisi Gwanafyo alisema mpaka sasa kontena 37 kati ya 56 zilizokwama katika Bandari ya Dar es Salaam, zimewasili huku zilizosalia kuendelea kuja katika bandari hiyo. Mradi wa ukarabati wa meli ya MV Victoria unaoigharimu serikali Sh. bilioni 22.

Septemba 3, 2018, Rais John Magufuli alishuhudia utiaji sahihi wa mikataba minne ya ujenzi wa meli mpya, ujenzi wa chelezo, ukarabati mkubwa wa meli ya MV Victoria na MV Butiama kazi ambayo tayari inaendelea chini ya usimamizi wa kampuni ya huduma za meli MSCL.
 
Mimi nilitarajia kuwa MELI MPYA inanunuliwa/inatengenezwa kumbe ni ukarabati tu. Billioni 22 haiwezi kununua/kutengeneza meli mpya?.
 
Mimi nilitarajia kuwa MELI MPYA inanunuliwa/inatengenezwa kumbe ni ukarabati tu. Billioni 22 haiwezi kununua/kutengeneza meli mpya?.
 
Ni kazi kubwa, na inawezekana. Si swala la kujaribu. Ina stage 3: under water wielding kuziba tundu lililotobolewa kwa maelekezo ya wanasiasa ( na kuizamisha meli), kupump hewa ndani kuchukua nafasi ya maji, kuivuta ufukweni na kuigeuza. Jeshi letu lina weledi huo, na wa kuzidi, japo wanatumika kufanya shughuli za kisiasa ambazo 'mjinga' yeyote anaweza kuzifanya.
 
Zipi? Kusomba korosho?
 
Aliahidi mpya,kumbe anarekebisha na kupaka rangi..sio Mbaya lakini
 
Mimi nilitarajia kuwa MELI MPYA inanunuliwa/inatengenezwa kumbe ni ukarabati tu. Billioni 22 haiwezi kununua/kutengeneza meli mpya?.
Meli mbili zinakarabatiwa na meli ya tatu mpya inajengwa, na chelezo kipya kinajengwa.
 
MV Liemba ilizamishwa na wajerumani, miaka kadhaa baadae iliibuliwa na waingereza. MV bukoba kuna umuhimu wa kufikiria kuiibua na project hiyo jeshi linaweza.
Hii inawezekana tayari kuna kampuni za wa Norway na Italia kazi zao ni kuibua meli zilizozama (Wrecks).

Na kama mnataka pesa wao wanainunua kama skrepa kwa bei nzuri kwa kila kilo ya chuma.
 
Mimi nilitarajia kuwa MELI MPYA inanunuliwa/inatengenezwa kumbe ni ukarabati tu. Billioni 22 haiwezi kununua/kutengeneza meli mpya?.
Uwekezaji wa meli ni gharama kubwa sana. Hiyo Billion 22 haiwezi kununua meli kubwa.
 
Bukoba ilikuwa imepakwa rangi wakati ikizama
Pumbafu zenu mnapaka rangi vimeli vibovu ili kutoa sadaka wananchi kama mlivyofanya kwa MV. BUKOBA?
vimeli vimechoka ile mbaya mnaanda kafara, mtaanza kufa ninyi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…