esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 552
Mwenyekiti wa Bodi ya Tasac, Profesa Thadeo Sata, alitoa taarifa hiyo alipozungumza na waaandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa meli hizo zinazotegemewa kuanza safari mwezi Machi, 2020. Prof. Sata alisema lengo la ziara hiyo iliyoongozwa na uongozi wa kampuni ya meli MSCL ni kuhakikisha viwango vinavyohitajiwa kwa usalama wa vyombo hivyo katika kuvikarabati vinakuwa sawa.
Naye msimamizi wa miradi hiyo kutoka kampuni ya meli Mhandisi Abel Gwanafyo, alisema ujio wa bodi hiyo ni faraja kwao na kwamba watahakikisha kuwa wanafanyia kazi yale yote waliyowaelekeza.
"Viongozi hawa wamefanya ziara Kanda ya Ziwa katika kutekeleza moja ya jukumu lao kubwa la kuhakikisha kuwa viwango vinavyohitajika kwa usalama vinakuwa salama," alisema. Mhandisi Gwanafyo alisema mpaka sasa kontena 37 kati ya 56 zilizokwama katika Bandari ya Dar es Salaam, zimewasili huku zilizosalia kuendelea kuja katika bandari hiyo. Mradi wa ukarabati wa meli ya MV Victoria unaoigharimu serikali Sh. bilioni 22.
Septemba 3, 2018, Rais John Magufuli alishuhudia utiaji sahihi wa mikataba minne ya ujenzi wa meli mpya, ujenzi wa chelezo, ukarabati mkubwa wa meli ya MV Victoria na MV Butiama kazi ambayo tayari inaendelea chini ya usimamizi wa kampuni ya huduma za meli MSCL.