Nimewahi kugombea mara moja tu ila kila nikifiria kurudi tena jimboni narudinyuma, kwani sina uwezo kifedha.
Simulizi ya Fatma Shaaban Mohamed (51), mkaazi wa Kiuyu Minungwini Wilaya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, inatuonesha ukata wa fedha unavyomkatisha tamaa kuingia tena jimboni katika Uchaguzi wa 2025.
Anasema amegombea Udiwani mwaka 2010 Jimbo la Wingwi Shehia ya Njuguni Wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mama huyo ambae amezaliwa katika kijiji cha Machengwe Ziwani, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Anasema amesomea taaluma ya uwalimu ngazi ya Cheti, katika Chuo cha Ualimu cha Wiyat kilichopo Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, na ana familia ya watoto saba.
Anasema ameanza harakati za siasa mwaka 2012 ameshawahi kugombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya matawi, na hata za kwenye Jumuia ya wanawake.
‘’Nimeshawahi kugombea nafasi nyingi kuanzia kwenye matawi, na hata nafasi ya ukatibu katika Jumuia ya akinamama ya Chama changu, ila sikuwahi kufanikiwa’’, anasema
Hakukata tamaa aliendelea kupambana na kukitumikia chama, kwa vile alikua ana imani siku moja ataweza kufanikiwa.
Suala la kufikiria kugombea alipata ushawishi kutoka kwa walimu wenzake wa Skuli na akashawishika, kwani alikua na ndoto za kua kiongozi tokea zamani.
Mnamo mwaka 2007 alianza kikamilifu kushuka tawini na kuanza kufanya shughuli ndogo ndogo za chama.
Fatma anasema mwaka 2010 alijiingiza jimboni na kugombea nafasi ya Udiwani, na kupambana na wanaume bila ya kua na khofu yoyote.
Katika kundi la watu waliojitokeza kuchukua fomu katika Chama chao kwa nafasi hiyo ya Udiwani, yeye ndie alieibuka mshindi, na kuingia kwenye kinyan’ganyiro na kupambana na wapinzani wenzake wa vyama vyengine, licha ya kuwa jamii ilimkubali vya kutosha, ila mwisho wa siku alianguka hakuweza kulikamata jimbo.
‘’Asikudanganye mtu kama huna pesa kwenye Uchaguzi huwezi ukashinda, na mimi nasubutu kusema, kilichoniangusha ni pesa tu sio kituchengine,’’anasimulia.
Kwakweli suala la pesa ni tatizokubwa na linawafanya wanawake wengi warudinyuma kuingia majimboni na shindwa kugombea.
‘’Sasahivi wanawake tuliowengi tumekua na hamu ya kugombea, ingawa umasikini unatufelisha, kama huna pesa hakuna yoyote unaempiga kampeni akakuangalia,’’anaeleza.
Amegundua suala la pesa ni silaha kubwa kwenye Chaguzi, na ndio inayowafanya wenyepesa zao sikuzote kubakia wao kwa wao majimboni, na masikini kuishia kuwa wapiga debe tu.
Anatamani kurudi tena jimboni, ila amekata tamaa, kwani ni masikini, hana pesa zitakazomsaidia kufanya shughuli za kampeni katika kipindichote cha Uchaguzi
FAMILIA YAKE
Kombo Khatib Bakar (60) mkaazi wa Kiuyu minungwini ni mume wa mwanamama huyo shujaa anasema baada ya mke wake kumpa wazo la kutaka kugombea hakumkatalia, alikua anamuamini ataweza, kwani alikua ni mpambanaji na mpenda maendele.
Alijitoa kihali na mali kumsaidia mke wake huyo kwa kila alichojaliwa nacho, kuhakikisha anapata nafasi, ili aweze kuja kuwa msaada kwa wanawake wenzake na hata kwa Taifa .
‘’Simkumzui wala sikua na hisia mbaya nae, bali nilimuunga mkono kwa kipindichote, kwani nilikua namini anaweza kupambana,’’anafahamisha.
Hivyo amewashauri wanaume wenzake kuwa na uthubutu kama yeye, wawaruhusu wenza wao kuingia kwenye fursa mbalimbali za maendeleo ili walete mabadiliko kwenye jamii,’’anafahamisha.
Salma Kombo Khatib (28) ni mtoto wa Fatma Shaaban yeye anasema walimpa mashirikiano makubwa mamayao, kwani walikua wanamuamini.
Amefahamisha kua walikua wanaimani endapo akapata jimbo ataleta maendeleo kwa wananchi wake, kupitia Nyanja mbalimbali ikiwemo Afya.
‘’Kiongozi mwanamke Tunakua na imani nae zaidi, kwani yeye pia ni mama, na siku zote anaejua utungu wa mwana ni mama mzazi,’’anaeleza.
JIRANI YAKE
Saumu Omar Hamad (40) mkaazi wa Kiuyu minungwini anasema jirani yao huwa anaweza kua kiongozi nzuri, kwani ni mtu anaekua karibu na wenzake, amekua akiwashauri mambo mengi ya kimaendeleo.
‘’Kwa Kweli jirani yetu huyo tunamkubali kua kiongozi, ametuhamasisha tumejiunga katika vikundi vya hisa, ambapo tukiwa na shida zutu tunakwenda tukikopa,’’amemalizia Saumu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wiala ya Micheweni Khamis Juma Omar anasema wanachokifanya kwasasa ni kuwasimamia wanawake wa Chama chao kupata mikopo serikalini, ambayo itawasaidia kuendesha shughuli zao za Uchaguzi.
‘’Tumekua tukiwasimamia na kuhakikisha wanapata mikopo ya mfuko wa uwezeshwaji wanawake kiuchumi ili kumudu kuendesha shughuli zao, kwa kipinduchote cha kampeni,’’anafafanua.
WANAHARAKATI
Hidaya Mjaka Ali mwanaharakati wa masuala ya watuwenyeulemavu kisiwani Pemba anasema ipo haja kwa Serikali na vyama vya siasa, kuweka ruzuku maalumu kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wanaotaka kugombea, ili kuona wamejitokeza kwa wingi majimboni katika uchaguzi wa 2025.
Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar kimesema kimekua kikifanya jitihada mbalimbali, kuona kumekua na mazingira rafiki kwa wagombea wanawake katika uchaguzi mkuu wa Octobar 2025.
‘’ Tunatamani kuona kumekua na uwezeshwaji wa kifadha kwa wagombea hususan wanawake, ili wawe na hamu ya kuingia majimboni na kugombea,’’ Amina Ahmed Kaimu Mratibu Ofisi ya TAMWA Pemba anashauri.
TAKWIMU
Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Kamati ya Kufuatilia Uchaguzi Tanzania kuanzia 2015 hadi 2020 Idadi ya Madiwani wanawake wa kuchaguiwa kutoka kwenye kata ni 204 ambao ni sawa na asilimia 5 ya Madiwani wote.
Kwa Zanzibar idadi ya waliojitokeza kugombea Udiwani katika Uchaguzi wa 2020 wanaume walikua 276 wanawake 74 Walioshinda wanaume ni 85 wanawake 25
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Zanzibar inawanawake wengi ambao ni 974,281 sawa na asilimia 51.6 kuliko wanaume, ikiwa wao ni 915,492 sawa na 48.4.
Ambapo licha ya uwingi huo bado idadi kwenye ngazi za maamuzi ni kidogo, Kati ya hao, ni asilimia 21.14 tu kwa wanawake 71 waliojitokeza kugombea udiwani.
ILAANI YA UCHAGUZI YA WANAWAKE
Ilani ya Uchaguzi ya wanawake, Uchaguzi wa Serikali za mitaa ya mwaka 2019 na Uchaguzi mkuu wa 2020, Madai ya mtandao wa wanawake wameitaka serikali kusimamia matumizi ya rasilimali fedha, hususani ruzuku zitokanazo na kodi ya Watanzania, ili kuhakikisha zinatumika kwa kuziba mapengo ya jinsia wakati wa uchaguzi.
ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
Moja ya mkakati wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2024 imesema, ni kuwawezesha wanawake kushiriki katika ngazi mbalimbali za mamuzi.
Hata katiba ya Zanzibar ya 1984 katika kifungu cha 21 (1) kinaeleza kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke na Taifa lake.
Mkataba wa kikanda wa Nchi za kusini mwa Afrika, uliotiwa saini mwaka 2008 kupitia kifungu nambari 13 cha mkataba huo, kinaelezea kuwekwa mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwashajiisha katika Nyanja mabali mbali za siasa.
Na Fatma Hamad – Pemba