Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Mtu huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 35 aliokotwa hapo, huku pembeni yake kukiwa na chupa yenye pombe.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo na kuthibitishwa na wenyeviti wa mitaa hiyo miwili huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa bado hakijajulikana na upelelezi wa kubaini wahusika ukiendelea kufanywa na jeshi la polisi mkoani humo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igubinya, Ndonho Nzella ameieleza Nipashe Digital kwa njia ya simu kuwa alipokea taarifa hiyo kutoka kwa mashuhuda na kufika eneo la tukio na kukuta mwili huo ambao haukutambilika.
“Nilipofika eneo la tukio niliamua kuwajulisha polisi ambao walifika na kuuchukua mwili kwa ajili ya kuuhifadhi hospitali, utambuzi na uchunguzi ili kujua chanzo na wahusika wa mauaji hayo,” amesema Ndonho
Awali akizungumza na Nipashe Digital, Mwekitiki wa Mtaa wa Nyanza, Barnaba Luswetula amesema alipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kata yake na kuelekea katika eneo la tukio.
Barnaba, amesema kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio alikuta tayari mwili wa marehemu umechukuliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi huku akieleza kuwa tukio hilo ni la pili kutokea katika mtaa huo.
“Hili limekuwa ni tukio la pili kutokea katika mtaa huu miezi michache iliyopita aliuawa kijana mmoja kwa kukatwa na panga na mwili wake ulitambulika huku jeshi la polisi likiendelea kufanya uchunguzi juu ya matukio hayo,” amesema
Akizungumza na Nipashe Digital kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Gidion Msuya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Amesema mwili huo ulichukuliwa katika eneo la tukio na bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini wahusika.
“Kwa sasa bado tunaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha mauaji hayo pamoja na wahusika vilevile binti huyo mpaka sasa hajatambulika, lakini akitambuliwa tutatoa taarifa kwa wakati," amesema
Chanzo: Nipashe