Nikiona jiwe karibu naongezea ili asiamuke kabisa. Washenzi sana hawa
Kuna siku nilikua napita Coco beach,nikasema nisimame pale , kulikua na show ,ilikua siku ya Iddi . Jioni ilikauimesha ingia , giza nene ,nikiwa nimepaki gari nikashuka nikanza kutembe kuangalia vijana wanao onekana ni wahuni wakisherehekea Idd. Nikafika ufukweni, hapo nikamuona jamaa mmoja anatembea peke yake kama anaelekea nilipo, huku akiongea na simu mbele yangu nikaona kundi kama la watu 10 la vijana wa huni , likija kwa kasi ,lika nipita na kumfuata yule kijana, kilichofuata ni yule kijana kutaka kunyang'anywa simu ,akawa ana bisha , akajaribu kukimbia , alipo kua ana kimbia lile kundi likaanza kumkimbiza na kusema "uyo , uyo , uyo" .
Hapo ndipo kila aliye jirani aliamka na kuanza kumshambulia yule kijana wakidhani ni kibaka, wale wahuni waka mkamata , waka mchukulia simu, raba, jeanz na tishirt halafu waka mwacha, ila watu walio dhani ni kibaka wakaanza kumpiga mawe. uzuri beach hakuna mawe makubwa yule kijana alipigwa mbaka akazimia, huku akitokwa na damu nyingi kichwani tukajua amekufa , ndio wakamwacha. Kilichofuata ni sisi kumbeba na kumkimbiza hospitali , akapelekwa ICU, tunashukuru ni mzima leo .
Je cases kama hizi ni ngapi na kama tuna chukua sheria mkononi je watakufa wangapi bila hatia?