Ukatili wa peter scully: Kuumiza dunia nzima bila kuonesha hata chembe ya huruma wala kujali

Raphael Mtui

Senior Member
Joined
Nov 26, 2024
Posts
141
Reaction score
317
Raphael Mtui 0762731869

TAHADHARI!

HABARI HII INA MAELEZO YENYE KUUMIZA. CHUKUA TAHADHARI.

Peter Gerald Scully ni raia wa Australia, akitokea jijini Melbourne. Alipokuwa mtu mzima, alianza 'kujitafuta' ili naye 'atoke' kimaisha. Akagusa hiki kikafeli, akagusa kile kikafeli.

Siku moja, akapata wazo, japo la kitapeli. Akalitazama lile wazo, akaona linaweza kumpatia pesa nyingi, japo kwa njia za kitapeli. Akainama, akacheka, akasema: "Sina jinsi. Nataka pesa. Nitaanzisha kampuni. Nitaiita The Key Result. Itakuwa ni uwekezaji wa masuala ya nyumba."

Kijana akaanzisha kampuni. Kwa muda mfupi, akakusanya pesa za watu. Mwaka 2011 'arobaini' zake zikafika. Alikuwa ameshatapeli karibia dola za ki-Marekani milioni mbili, hapo sio chini ya shilingi bilioni tano za ki-Tanzania.

Ile tu anataka aanze kula maisha, 'manjagu' wa Australia wakamweka kwenye 'rada' zao! Wakasema kijana usitutanie. Vumbi likatimka. Kijana Peter akatoroka nchi. Huku nyuma akaacha kesi yenye makosa 117 ya utapeli! Mh! Makosa 117 wangemwua aisee!

Watu wakawa wamelizwa pesa zao namna hiyo. Wakabaki wanalia.

Shida ikaja kwamba, sio polisi wala nani aliyejua Peter ameenda wapi. Peter alikuwa ametoroka kwa umakini sana.

Kwa siri sana, Peter alikuwa ameenda hadi nchini Ufilipino. Akatafuta maeneo ya ndani-ndani kabisa aweze kujificha kisawasawa. Akaenda kusini mwa Ufilipino, akajichimbia maeneo ambapo watu masikini sana wanaishi. Akawa anaishi mkoa uitwao Mindanao, na pia akawa akiishi kwa siri miji ya Cagayan de Oro, Surigao, na Malaybalay.

Mpaka hapa, pengine Peter angesema hivi: "Nimeiba pesa za watu, na nimefanikiwa kutoroka. Ngoja nitafute mashamba huku nianze kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa. Niliowatoa machozi wanatosha. Acha nisiongeze laana."

Lakini Peter hakuwaza hivyo. Nyerere alisema ukila nyama za watu utaendelea kuzila tu. Kuna saa utazi-miss, maana kwako ni nyama tamu. Shetani na malaika wake Petiro Scully.

Badala Peter aachane na uovu, akaishia kusema: "Bado ninataka pesa nyingi. Tena kwa njia yoyote. Kama ni kuua watu nitaua hata dunia nzima! Nachotaka ni pesa nyingi!"

Peter alikuwa na roho ya aina yake. Akapata wazo lingine, wazo ovu mno. Muda mfupi ujao, alikuwa tayari kuiliza dunia nzima. Na wala hajali. Na kweli, Peter amejua kutuumiza. Peter ni moja ya watu wenye akili nyingi, lakini ni mtu mpumbavu kuwahi kukanyaga hii dunia! Furaha yake ni pale mtalia wote. Na mkilia sana ndio mnazidi kumchekesha. Wazo la Peter lilikuwa ovu mpaka shetani akaita karamu kuzimu. Najuta hadi kwa nini akaitwa Peter.

Alifanya hivi: alichukua mihela yake ya wizi. Akajenga studio nzuri, safi kabisa, akaiwekea teknolojia za hali ya juu za mitandao. Peter ana akili na ujuzi mwingi. Tofauti ni kwamba ni kwamba ana njaa ya kikatili kupindukia. Yupo tayari kuchinja na kuuza moyo na figo hata kama ni za mtoto wake mwenyewe!

Ili uelewe wazo la Peter, ngoja nikupe elimu kidogo, japo sio ngeni sana kwako.

Najua unajua intaneti. Ni kama hii hapa unasoma whatsapp, facebook, google, instagram, youtube, na kwingineko kwa kutumia simu au kompyuta yako.

Lakini, kuna ile intaneti ambayo 'ipo chini' yake, ambayo hujawahi kuiingia. Inaitwa Deep Web. Lakini tena sikia vizuri: ndani ya Deep Web kuna ule Mtandao Giza unaoitwa Dark Web. Huku ndio kwenyewe sasa!

Najua wengi mnajua hii Dark Web, angalao kwa kusikia tu. Huko, huingii tu kama tu unavyofanya, kuwasha data na kuanza kuperuzi mtandaoni. Pamoja na kwamba ndani ya Dark Web kuna vitu vizuri ambavyo inalazimu vipatikane huko tu, lakini unapotaja Dark Web unataja mahali ambapo shughuli chafu duniani hufanyika.

Hapa unazungumzia vitu kama biashara haramu za kuuza watu, biashara za uuzaji haramu wa silaha, miamala haramu ya fedha, makampuni ya kitapeli, ufisadi wa malundo makubwa ya fedha na mambo kama hayo.

Huku ndani ya Dark Web (Mtandao Giza) kuna data nyingi kuzidi haya ambayo yanapatikana kwenye hii intaneti ya kawaida tunayoingia kila siku!

Ndani ya Dark Web ni sehemu salama kwa magendo yote unayojua duniani. Ni mtandao ambao umesukwa kwa namna ambayo mtu anapoingia anaweza kuweka 'layer' za kificho kwa namna ambayo kamwe hawezi kujulikana ni nani.

Utaishia kuona uozo na uozo lakini hakuna jinsi ya kung'amua wahusika.

Kwa sababu ya mambo maovu kupindukia yanayofanyika ndani ya Dark Web, wewe kuingia na kuyatazama tu tayari huwa ni makosa ya kukupandisha kizimbani.

Ndio maana watu hawaingii kabisa kupitia simu, hata kama namna hiyo ipo. Ni hatari kabisa mtu kufanya hivyo. Hata watu wanapoingia kupitia kompyuta, kunahitajika umakini na uzingatiaji wa masharti magumu kabisa.

Kama nilivyosema, ndani ya Dark Web, kuna mambo ambayo kuyatazama tu ni makosa makubwa mno kutokana na 'content' yenyewe ilivyo.

Ninakupa mfano: ndani ya Dark Web kuna websites ambazo huonesha video za kutisha na kusikitisha, ambazo hupendwa na wale watu wanaoitwa 'sadists'. Hawa ni watu wanaopenda kufurahia kuona mateso.

Watu hawa huingia na kuanza kuchagua aangalie nini. Mfano, mhusika anaweza kuingia na kutaka aangalie video za mtu akiteswa kwa kuchomwa moto, au akikatwa kiungo kimoja baada ya kingine hadi anapokufa. Duniani kuna mambo ya ajabu mno! Sadists wanapenda wanapoona mtu huyo anavyoteseka na wanaburudika wanaposikia sauti za vilio vyake!

Kumbuka, hizi sio video za kutengeneza. Wako watu duniani wanaofanya kazi hiyo ya kurekodi video za mateso na wapo salama mradi ni ndani ya Dark Web.

Sadists wanapotazama kuna wanazolipia na kuna wanazotazama bure.

Kutazama video za namna hii ni makosa makubwa. Ni kuendelea 'ku-injinia' waandaaji wa mambo kama hayo. Ni kosa lenye adhabu kali kabisa. Kwa hiyo, usiwahi hata siku moja kutamani kutembelea Dark Web.

Katika kundi la websites za video za kutisha, kuna kundi la websites hizi ambazo huitwa 'Hurtcore.' Hili ndilo kundi baya kuliko makundi yote ya websites za video za kutisha na kuhuzunisha za Dark Web.

Hurtcore ni website za uovu uliopindukia kabisa. Hizi hurtcore, zinahusisha utengenezaji wa video za watoto wakifanyiwa ukatili uliokubuhu. Zinaitwa Child Sexual Abuse Material (CSAM).

Watoto wadogo wakiingiliwa kimwili, wakipigwa vipigo vya kikatili, wakiwa wamefungwa minyororo, na huku wakiwa wanapewa mateso yenye kuleta maumivu makali ya muda mrefu!

Sasa, Huyu bwana Peter akawaza afanye 'biashara' ya hurtcore. Ndio maana nilikuambia alifungua studio ya kisasa kabisa. Sasa, yeye aliamua ataifanya hii kama biashara ya daraja la kwanza kwa watazamaji 'Premium'. Nikisema Premium maana yake ataandaa video za mateso makali mno na kuziuza kwa bei ghali huko Dark Web. Pia, atakuwa akipokea 'oda' kutoka kwa watazamaji wake wakitaka video za mateso wanayotaka.

Fikiri video ukatili wa watoto zinavyoumiza! Wote hapa ni mashahidi pale video za namna hiyo zinapovujia mitandaoni.

Sasa, huyu Peter akaamua atakuwa akiandaa video za Hurtcore, zikionesha mateso kwa watoto wadogo! Sasa, kisheria hairuhusiwi kuandika maelezo ya mateso yanayohusu video fulani. Mfano useme, katika video fulani yenye jina fulani, mtoto anaingiziwa kisu sehemu zake za siri. Hilo ni kosa kisheria kwa kuwa unautweza utu wa huyu mtoto husika unayemzungumzia.

Peter aliamua kuwa atakuwa anafanya mateso ya kuwaingilia kimwili watoto wadogo kabisa, wa kike na wa kiume, huku akiwapa mateso mengine makali na kuwapiga vipigo vinavyoweza hata kusababisha kifo.

Kumbuka, hapa alikuwa akiishi kimaficho katika jamii ya watu masikini mno. Peter akajitafutia watu wa kushirikiana naye kwenye unyama wake. Kazi ya kwanza ikawa ni namna ya kupata watoto.

Hiyo haikuwa shida kwake. Kwa kuwa anaishi eneo masikini, kuwapata watoto ilikuwa kazi rahisi maana wazazi walikuwa wanakubali kuwatoa tu kwa ahadi za kwamba wanaenda kusomeshwa na kupewa mahitaji yote.

Watoto wengine walikuwa wakirubuniwa tu mtaani kwa kupewa pipi na biskuti. Peter sasa akawa ana studio safi kabisa, vifaa vya kisasa vya kurekodia, na mitambo yake ya kupost Dark Web.

Huko Dark Web akatumia akili zake kutengeneza website yake ambayo aliiwekea ulinzi "encryption" ipasavyo, kisha akaipa jina la No Limits Fun. Kutokea hapo akaanza 'kazi' zake rasmi.

Wale watoto aliowateka, akawa anawaficha huko ndani kwenye 'jela' yake. Akaanza rasmi kuwarekodi huku akiwapa mateso ya kuogofya!

Na kweli, akaanza kupata wafuasi. Kuanzia mwaka 2012, akaanza kujulikana huko Dark Web.

Fikiria, aliifanya hii 'biashara' kwa makali mpaka akaanza kupata oda! Sijui kama umeelewa. Mfano, mteja anamwambia: "Tengeneza video ya mtoto ukiwa unamnyonga kwa mikono kidogo-kidogo hadi afe! Hakikisha, wakati unamnyonga, awe amesimama juu ya makaa ya moto!"

Yaani, wateja wake wanamwambia aandae video za mateso ambayo wao ndio wanachagua! Ukisikia watu sadists ndio hawa sasa! Wana roho ya shetani kisawasawa! Yaani, wanafurahia kabisa wanachofanyiwa watoto hao, tena wanatoa oda ya video zingine za mateso sawasawa na matakwa ya oda zao.

Peter anawajibu yuko tayari, mradi wajiandae kulipia. Peter alivyokuwa ameweka mfumo wake wa malipo, utachoka! Ilikuwa mtu akitaka kulipa, alitakiwa kutumia sarafu mtandao (crypto currencies) kama Bitcoin. Utamkamataje Peter Scully kama analipwa kupitia sarafu mtandao?

Unaona sura yake wazi wazi kwenye video, lakini utampata wapi? Kama anatumia Dark Web, utampataje?

Peter akaanza kuingiza pesa nyingi kutoka nchi za bara la Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini. Peter akatamalaki. Anaonekana, anajulikana, lakini yuko wapi? Yupo Marekani? Yupo Afrika? Yupo Ulaya? Yupo wapi? Watu waanzie wapi kumtafuta? Ikawa ni kitendawili.

Akaendelea na kazi hiyo hadi ilipofika 2014 alipofanya jambo la kutisha kuliko yote. Alipost video ya dakika kama 50, dunia nzima ikatoa machozi. Kila kitu kilisimama.

Video hiyo ni maarufu kwa jina la "Daisy's Destruction" Kwenye video ile kuna hadi mtoto wa kike wa mwaka mmoja na nusu akisulibiwa vilivyo na baba Peter! Kwenye video hiyo, walikuwa watoto watatu: 'Daisy,' 'Liza' na 'Cindy.'

Kama nilivyosema, hairuhusiwi kusema ni mateso gani haswa ambayo watoto wale walikuwa wakifanyiwa. Ni makosa kabisa.

Tuendelee:

Pata hii picha: Peter alitangaza kuwa ili mtu aweze kuitazama video hii, lazima alipe dola elfu kumi za Marekani!! Yaani, kama upo Tanzania na unataka kuitazama video hiyo, ulitakiwa ulipie shilingi milioni ishirini na saba! Tena, ukitaka kuiangalia tena mara ya pili, unatakiwa ulipie tena kwa mara nyingine tena!

Peter alikuwa na wateja matajiri kote duniani. Watu walilipa kutazama video ile.

Mwaka huo 2014, shirika moja la kutetea haki za watoto huko Ulaya (Dutch National Child Exploitation Team) wakashindwa kunyamaza.

Wakawasiliana na INTERPOL (International Criminal Police Organization). Pia, wakagonga hodi Marekani, wakawapasha habari FBI (The Federal Bureau of Investigation). Kama haitoshi, wakagonga pia milango ya AFP (The Australian Federal Police).

Kwenye matukio kama haya, INTERPOL na FBI huyachukulia kwa uzito wote. Kwa video hii, hapakuwa na kisingizio chochote. Kilichokuwa kinatakiwa ni kwamba Peter anatakiwa kukamatwa, na si vinginevyo.

Ni kweli, website ya Peter ilikuwa 'encrypted' kwa usahihi wa asilimia mia. Unampataje sasa? Utaanzia wapi? Lakini FBI, Interpol, na AFP waliapa lazima wamkamate tu.

Hata mifumo ya ulipaji wa Peter ulifanyika kupitia sarafu mtandao. Watampataje kama anatumia crypto currencies, na bado analindwa na Tor Network inayomfanya awe salama ndani ya Dark Web?

Lakini FBI, AFP na Interpol waliapa lazima wamtafute na wamkamate. Walijua shetani amevuka mstari kupindukia! Lazima akamatwe, akomeshwe haraka!

Kuanzia hapa; kazi ikaanza rasmi. Kutafuta zimwi, kulikamata na kulifungia mahali lisiweze kufanya tena ukatili huu!

Wakati huu habari za video ya Daisy's Destruction zilikuwa zimeshatapakaa dunia nzima. Sasa utauliza, kwa nini sikuona kwenye vyombo vya habari?

Iko hivi: Video za hurtcore zinaumiza sana. Zimejaa ukatili kiasi ambacho vyombo vya habari haviruhusiwi kutangaza habari za namna hiyo.

Watu wema wanaumia kimya-kimya! Huwezi kusikia viongozi wa serikali au watu maarufu wakitoka na kulaani vitendo hivyo. Kwa nini? Kwa sababu video hizo ni 'extremely traumatizing!' Mtu akiangalia anaweza kupata magonjwa ya kiakili na kisaikolojia.

Vyombo vya habari na watu maarufu kutaja video hizo ni kuzidi kufanya watu wakaangalie. Hiyo ni moja. Pili, ni kuzidi kudhalilisha wale watoto wanaofanyiwa ukatili huo. Wanaotendewa ukatili huo, (mara nyingi wakiwa uchi), ni kitu kinapaswa kuendewa kwa hekima sana.

Lakini kwa unyama ule, hakuna mtu ambaye hakutamani Peter atafutwe, akamatwe haraka sana na awajibishwe ipasavyo.

Kwa kesi ya Peter, hata hivyo ilikuwa ni hatari kabisa kutangaza jambo hilo kupitia vyombo vya habari na watu maarufu. Hilo lingeharibu kabisa uchunguzi wa FBI, AFP na Interpol.

Kama Peter angeona vyombo vya habari vinatangaza uchafu wake, lazima angekusanya mabegi yake akimbilie maficho mengine, na hilo lingezidi kuleta ugumu wa kumpata.

Mbaya zaidi, lazima angeua watoto ambao bado alikuwa akiwashikilia kwenye 'jela' yake pale studio. Angewaua kwa lengo la kupoteza ushahidi. Peter aliwahi kuwaambia watoto anaowashikilia wachimbe makaburi yao wenyewe kabla hajawaua!

Tuache hilo:

Tukasema, pamoja na ugumu wa kumpata lakini kila mtu alitamani Peter akamatwe haraka mno, na wasikie amekamatwa na amewajibishwa kisawasawa.

Unawezaje sasa kujua mahali alipo? Malipo anatumia sarafu za kidijitali. Mahali pake pa 'kujivinjari' ni Dark Web, mahali ambapo Tor Network imemwekea 'makofuli' ambayo ni kitendawili kusema unaanza kumtafuta.

Kwa uchungu ambao Peter alifurahia kuipatia dunia, FBI, INTERPOL na AFP wakaanzisha msako mzito ulioitwa OPERATION NO LIMITS.

Kwamba, ni msako ambao hauna mipaka, yaani watatoboa kila mahali mpaka Peter akamatwe.

Msako huu umekuja kupewa jina la Massive international Manhunt, au Massive International Investigation. Kwa Kiswahili tuseme hivi: "Uchunguzi/Uwindaji Mkubwa wa Kimataifa wa Binadamu.*

Katika historia ya binadamu, huu ulikuwa ni moja ya misako ya hali ya juu mno kwa mataifa mengi kushirikiana kutafuta mtu. Msako kama huu ulihitaji ushirikiano kutoka mataifa mbalimbali, pamoja na mashirika mbalimbali ya usalama ya kimataifa.

Pia msako huu unajulikana kama one of the most complex digital forensic operations in history, involving the tracking of Bitcoin payments and encrypted communications on the Dark Web.

Yaani, ni moja ya operesheni tata zaidi ya uchunguzi wa kidijitali katika historia, ukihusisha kufuatilia malipo ya Bitcoin, na mawasiliano yaliyosimbwa kwenye Dark Web.

Kwanza kabisa, maafisa waliamua hakuna cha kuwashinda. Wakajifanya ni wateja, wakalipia kutazama Daisy's Destruction. Lengo la kulipia walikuwa wameamua kufanya kazi 'isiyowezekana' ya kufuatilia mwenendo wa hayo malipo ya Bitcoin. Mambo haya kwa uhalisia hayawezekani kabisa. Lakini mbele ya maafisa walioamua, waliamu kufanya yasiyowezekana yawezekane.

Teknolojia zikatafutwa, na ambazo hazipo zikaundwa, lengo tu ni Peter akamatwe. Kufuatilia mwenendo wa malipo ya sarafu za kidijitali ni kama ukichaa. Lakini hawakukata tamaa. Wakaamua kuchimba na kuchimbua. Hiyo sio kazi ya leo na kesho. Inahitaji muda mrefu usiojulikana, lakini muhimu ni Peter afahamike yuko wapi na wamkamate. Kufanya shughuli kama hii lazima kuna wakati teknolojia zitalazimika kuvunja sheria za mitandao, hivyo 'uhuni' utafanyika, lakini kwa nia njema.

Ikawa wazi kwamba ingawa wahalifu wanatumia teknolojia za hali ya juu kujificha mitandaoni, lakini bado polisi wa kimataifa wanawazidi na wanatakiwa kuwazidi mbio.

Bitcoin inajulikana kwamba ni 'anonymous' lakini ukweli ni kwamba ni 'pseudonymous'. Inaweza kujulikana. Kila muamala wa Bitcoin kokote duniani huwa unahifadhiwa kwenye 'public ledger' ambayo wengi tunaifahamu kama Blockchain.

Maafisa usalama walifuatilia anwani zote za miamala ambayo inaelekea kwenye website ya Peter ya No Limits Fun. Wakafuatilia hadi wakagundua kuna watu matajiri kutoka Marekani na Ulaya ambao wanalipia kutazama videos za Peter.

Lengo la kufuatilia Money Trail za wateja hawa, ni ili kujua ni wapi Peter atazi-withdraw ili ziwe pesa za kawaida mahali alipo ili azitumie kwa maisha yake. Pale atakapozibadili kutoka sarafu ya kidijitali kuwa fedha ya kawaida, (pesos ya Ufilipino) hapo maafisa wangejua huyu mtu yuko wapi.

Lakini hawakutegemea tu njia hii: waliamua kutumia kila kitu kilichopo kwenye video ile. Huu ni ufuatiliaji unaoitwa Digital Forensic Fingerprinting. Maana yake, kila kilichopo kwenye video kinatakiwa kitumike kupata 'location' yanapotendeka mambo hayo.

Kwanza kabisa, ushahidi uliowapa mwanga mkubwa ni kitu kinaitwa Electrical Network Frequency (ENF) Analysis.

Nitafafanua:
Hiki kitu kwa majina rahisi huitwa 'kelele za umeme, au mwingiliano wa umeme (Electrical noise/interference).

Maana yake nini? Kila laini ya umeme unayoiona mtaani, na duniani kote, ina mawimbi yake yasiyofanana na laini yoyote duniani. Jinsi umeme unavyopita kwenye nyaya na kuingia majumbani, unajijengea tabia ya kipekee ya mawimbi (frequencies) ambayo haifananii kabisa na laini nyingine yoyote duniani.

Ni rahisi kwamba: jinsi watu wanavyotumia umeme wa laini fulani, katika siku fulani, haiwezekani siku hiyo kuwe laini ambayo watu wake walitumia tumia umeme katika kiwango hicho hicho. Haiwezekani kabisa hicho kitu kutokea.

Kila sekunde, matumizi ya laini fulani huwa yanabadilika-badilika kutokana na umeme unavyotumika. Wakati mtu fulani anazima friji, mwingine anakuwa amewasha la kwake, huyu anazima taa, yule anawasha, huyu anapasi nguo zake, wengine hawapasi, huyu hajawasha chochote, kuna mwingine amewasha mashine zake zote.

Nakupa mfano sasa, laini fulani inaweza ikawa inachezea frequencies zake kwenye 48.00002 na zinapanda hadi 50.41397, zinafanya maelfu ya mizunguko lakini hazizidi hapo wala kupungua hapo.

Baadhi ya serikali kubwa duniani huwa wanatunza tabia hizi kwenye 'metadata' zao.

Sasa basi: Peter alikuwa akifanyia kazi zake ndani ya studio yake. Video yake ilikuwa ndefu hadi dakika hamsini. Sikia; ambacho Peter hakujua ni kwamba, haya mawimbi au sauti za umeme huwa zinarekodiwa na kamera zake mwenyewe. Ndio! Umeme una sauti zake (Electric noise).

Hata wewe unaporekodi video ukiwa ndani, video yako huwa inarekodi pia hizo 'electric noise'

Kupitia vifaa vilivyochomekwa kwenye soketi ukutani, 'sauti' hizi hurekodiwa. Lakini pia kupitia mwanga wa taa za ndani, 'sauti' hizi huweza kurekodiwa. Vifaa vya Peter mwenyewe vilikuwa vinamsaliti muda si mrefu.

Maafisa lazima wawe mbele ya muda. Wakatumia forensic softwares kutoa sauti hizo kutoka kwenye video ya Peter.

Masoftware yakaingia kazini. Frequencies zikachambuliwa na kusomwa. Zikaanza kutafuta dunia nzima ni wapi palikuwa na gridi inayosoma sauti zile?

Kumbuka, hii nayo si kazi rahisi. Kazi ni ngumu zaidi pale ambapo hujui video ya Peter ni ya lini. Frequencies ulizonazo lazima ziwe ni frequencies zilizojitengeneza siku fulani. Lakini wataalamu hawakuchoka. Wakafuatilia. Hata kama ingewachukua mwaka mzima hawakujali. Wakatia bidii kufuatilia.

Mwisho wa siku sasa; lahaulaa! Frequencies za umeme kutoka video ya Daisy's Destruction zikapata gridi yake. Zilisoma kwamba hii ni gridi iliyopo nchini Ufilipino!

Likawa ni jawabu kubwa. Sasa hakuna tena kufikiria kumtafuta Peter kila mahali duniani. Ni kumtafuta nchini Ufilipino upande wa kusini mwa nchi hiyo.

Mamlaka za Ufilipino zikashtushwa sana kumbe zimwi lile lipo ndani ya mipaka ya nchi yao. Polisi wa Ufilipino wakaungana na kina FBI, AFP na Interpol kufanya msako.

Wakarudi tena kwenye video. Kwenye video kuna soketi za umeme za ukutani. Wakazichunguza, hadi zikaonesha kweli ni za Ufilipino. Ufilipino wanatumia soketi za Type A na Type B sawa na za Marekani.

Bado tena: Kwenye video zinasikika kelele mbalimbali za wanyama, ndege nk. Zikachunguzwa kujua hao ndege ni ndege wa aina gani, na huwa wanapatikana wapi. Yote haya yakazidi 'ku-narrow down' mahali Peter alipo.

Bado tena: kwenye video kunaonekana miti wakati 'kamera boy' alipomulika nje kipitia dirishani. Ikachunguzwa "flora and fauna". Kwenye vitu kama hivi, huwa hakuna kitu cha kupuuzia. Manjagu hao hapo! Wanakaribia kumkamata Peter.

Bado tena: kukawa kuna sauti zilisikika kwenye video kama pikipiki au bajaji. Zikafanyiwa uchunguzi wa kina. Hadi 'toyo' za Ufilipino zikamfunua bila yeye kujua! Zile kelele za toyo zikagundulika ni za Ufilipino.

Kwenye video kunaonekana ilikuwa mchana. Lakini swali ni je, ilikuwa ni asubuhi, mchana au jioni. Hiyo nyumba imekaaje? Mashariki au Kaskazi ni wapi? Wataalamu wa mambo hayo wakaletwa. Wakapiga kazi hapo. Ikajulikana ilikuwa muda gani wakati video inarekodiwa, na wakajua Kaskazini ni wapi na hivyo wakang'amua pande zote za nyumba ulimofanyika unyama huo.

Ili kupata uhakika zaidi ni wapi hasa nyumba ya Peter ilipo, maafisa wakaja na ile mbinu iitwayo "Trace an object". Hapa, ni kila kitu kidogo au cha kawaida kinachoonekana kwenye video. Sabuni, mafuta ya kujipaka, chana, kijiko, mapazia, rangi ya nyumba, 'tailz' za chini sakafuni nk. Kwa kifupi, kila kitu kwenye video kilitumika kufanya uchunguzi kujihakikishia vitu vya namna hiyo hupatikana wapi hapa duniani. Maafisa walitengeneza vitu kama vinavyoonekana kwenye video, wakawa wakizunguka navyo huko Ufilipino kusini wakiuliza huwa vinapatikana wapi au kuuzwa wapi. Hiyo ndiyo inaitwa Trace an Object.

1. Zile gridi za umeme zilisaidia kugundua nchi aliyomo Peter.

2. Hivi vitu kama tailz, rangi ya nyumba, vifaa vya mbalimbali vilisaidia kujua mitaa ambayo Peter amejificha.

3. Local Tip -Offs zilisaidia kuijua nyumba alimojificha Peter. Nikisema local tip-offs namaanisha ni zile taarifa za siri ambazo wananchi huzitoa kwa polisi au vyombo vya usalama.

Mtu anayejua anatafutwa huwa ana tabia ya kwenda kujichimbia kwenye nyumba fulani. Anajitahidi asijulikane, lakini lazima kuna namna ataacha alama tu kwenye macho ya jamii. Mfano: raia anaweza kumwambia polisi, "Kuna nyumba jirani kwangu yaani anayeishi huwa hatoki nje wala hajawahi kufungua mapazia".

Mfano wa ishu ya Peter, watu waliripoti kwa polisi: "Kuna mzungu anaonekana tajiri huwa hatoki humo ndani. Kuna watoto wadogo huonekana wakiingia na kutoka katika nyumba hiyo. Mzungu huyo huwa ananunua vifaa vya kisasa vya gharama kubwa. Huyu mtu anaonekana ni tajiri lakini anaishi huku kwenye mazingira mabaya ya kimasikini."

Taarifa kama hizi zilitumika kuipata nyumba alimokuwa akiishi huyu bwana Peter.

Baada ya kujiridhisha kuwa wamepata uhakika kuwa Peter yupo kusini mwa Ufilipino, katika kisiwa cha Mindanao, ndani ya mji wa Malaybalay uliopo jimbo la Bukidnon, sasa ilikuwa ni maandalizi ya wiki tatu za kumvamia na kumkamata Peter Scully.

Wiki tatu kabla ya kukamatwa kwa Peter, shirika la kishushu la Ufilipino (Philippine National Bureau of Investigation (NBI), wakiwa wameshapewa taarifa zote na FBI, AFP na Interpol, walianza maandalizi kabambe ya kumkamata.

Kwa wiki hizo tatu, maafisa wa NBI walikuwa wakiifuatilia kwa karibu nyumba aliyokuwa akiishi bwana Peter. Usiku na mchana, jicho la kina la NBI liliendelea kufuatilia kwa makini mienendo ya nyumba hiyo.

Lengo lilikuwa ni kuhakikisha asilimia mia moja ya kwamba Peter Scully anayetafutwa na dunia nzima yupo katika nyumba ile. Pia, walitaka kujua ni namna gani watavamia ili Peter asije akafanya jambo baya kwa watoto waliofichwa ndani, pengine akawaua haraka-haraka kabla hajakamatwa ili kuzuia ushahidi wa matendo yake kwao.

Saa 48 kabla ya uvamizi wenyewe kufanyika katika nyumba ya Peter:

Mji mzima walisambazwa askari wenye weledi maalumu. (Special Forces).

Maafisa maalumu kutoka NBI ndio waliokuwa wavamie nyumba ya Peter. Walikuwemo pia maafisa kutoka Philippine National Police (PNP) na wengine kutoka Criminal Investigation and Detection Group (CIDG).

Pia, walikuwepo maafisa maalumu kutoka AFP na Interpol, ambao kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha vifaa vyote vya Peter vya kuhifadhia data kama kompyuta, simu, flash, hard drives vinabaki salama.

Kazi yao ni kuhakikisha Peter hapati nafasi ya kuviharibu. Kama ilivyo kwa wahalifu wa aina ya Peter, huwa wanajiandaa muda wote kwamba ikitokea anakamatwa, basi haraka wanakimbilia kitu kinachoitwa Kill Switch. Wahalifu huwa nayo muda wote na kuibonyeza haraka sana ili kuharibu kila kitu kilichohifadhi ushahidi muhimu dhidi yao.

Hata majasusi wanapokuwa katika operations muhimu zenye hatari kubwa, huwa muda wote wanatembea na kidonge ambacho kama akikamatwa, huwa anakikimbilia haraka kukimeza ili afe kumwepusha na mateso atakayokutana nayo lakini muhimu zaidi kuepusha yeye kusema siri zote atakazotakiwa aseme.

Tuache hilo.

Pia, kulikuwa na timu ya madaktari ambao walikuwa 'standby.' Walijua huenda wakakuta watoto ambao wapo katika hali mbaya kiafya, kutokana na matendo waliyokuwa wakifanyiwa.

Kazi ya pili muhimu ya timu hii ilikuwa kuwaokoa watoto watakaokutwa hai, na kwenda kuwaficha kwenye nyumba salama (safe houses) ambazo zipo maeneo ya siri kwa ajili ya kuanza kuwatibu watoto hao kwa zile tiba za daraja la juu za kisaikolojia na kimwili, na kuhakikisha wanatunzwa kwa siri kubwa.

Usiku wa tarehe 19 February 2015, mambo yalikuwa tayari kabisa.

Kesho yake, siku ya Ijumaa, mida ya saa nane mchana kwa saa za Ufilipino, siku ya tarehe 20 February 2015, uvamizi ukafanyika.

Maafisa usalama walikuwa wameshajua ni muda gani sahihi wa kuvamia, ambao watamkuta Peter akiwa na 'zero opportunity' ya kujaribu kufanya chochote. Pia, walijua muda huo hana walinzi. Walijua atakuwa mbele ya kompyuta zake akiwa amechoka. Walijua hatakuwa na muda wa kufanya chochote kujaribu kujiokoa au ku-activate ile 'kill-switch'.

Ndio maana kukamatwa kwa Peter kulikuwa laini sana. Maafisa walivamia ndani. Kurupushani zilikuwa kidogo mno. Hakuna risasi hata moja iliyolia.

Peter alitiwa nguvuni haraka sana, na bila kupoteza sekunde alipelekwa kuzuini.

Vifaa vyake vyote, kuanzia vitunza data kama flash, memory cards, hadi compyuta zake, zilikamatwa salama. Kamera zake za hali ya juu na vifaa vya kisasa vya kurekodia vilikamatwa

Kutoka kuanza kumtafuta baada ya chapisho la Daisy's Destruction, palikuwa pamepita muda usiopungua miezi sita. Huenda alitafutwa kwa mwaka mzima.

Swali utakalojiuliza: vipi wale watoto watatu waliokuwa wakiteswa kwenye video ya Daisy's Destruction? Walipona? Walipatikana? Hali zao zipoje?

Kwanza, tuanze na huyu mtoto ambaye jina lake ndio hilo Daisy. Huyu alikutwa mle ndani akiwa hai, lakini alikuwa ana majeraha ambayo yaligeuka kuwa "vilema vya maisha." Majeraha hayo ni yale yaliyotokana na video ya Daisy's Destruction.

Mtoto wa pili ni Liza. Huyu naye alikuwa hai, na haraka alipelekwa mafichoni kuanza matunzo na matibabu maalumu.

Mtoto wa tatu ni Cindy. Bahati mbaya kabisa, huyu alifariki. Mwili wake ulipatikana mji uitwao Surigao baada ya msaidizi wa Peter kuongoza maafisa kwenda kuonesha walikoufukia mwili. (Walikuwa wameufukia mwili wake kwenye shimo fupi).

Lakini, kuna watoto wengine nane walikutwa ndani ya nyumba hii ya Peter. Watoto hao ni wa umri kuanzia mwaka na nusu hadi miaka 13.

Huyu mtoto wa umri wa mwaka mmoja na nusu alifanya ulimwengu ushtuke sana. Alipelekwa kwenda kulelewa na Idara ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ya Ufilipino (Department of Social Welfare and Development (DSWD).

Peter alikabiliwa na makosa mengi kiasi ambacho ilibidi kuwe na awamu mbili za hukumu. Mwezi June 2018 alihukumiwa kifungo cha maisha jela huko Ufilipino kwa makosa ya kusafirisha binadamu na makosa ya ubakaji wa watoto watano.

Awamu ya pili ilikuwa ni November mwaka 2022. Hapa alihukumiwa miaka 129 gerezani kwa makosa makubwa ya mtandao (extensive cybercrimes), ukatili dhidi ya watoto, (Child Abuse), na kwa kumiliki na kufanya shughuli za picha za uchi mtandaoni (pornography operation).

Peter Scully yupo ndani ya gereza lenye ulinzi mkali liitwalo Davao Penal Colony lililopo kusini mwa Mindanao huko Ufilipino.

Wakati akiwa gerezani, dunia ilikuwa na hamu ya kujua jambo moja: "Je, anajutia alichokifanya?" Watu walitamani kusikia neno kutoka kwake, ili wajue kama yupo katika hali ya majuto na masikitiko kwa vitendo vyake au la.

Ndio hapa akaruhusiwa mwandishi nguli mwanadada Tara Brown kutoka chombo cha habari kiitwacho 60 Minutes Australia, ambapo alipewa fursa ya kwenda kumhoji Peter Scully.

Bahati mbaya kabisa, majibu yote ya Peter yalikuwa ya kikatili, ya kukwepa kujibu anachoulizwa, na yaliyokuwa na uongo wa hali ya juu.

Tupitie kidogo interview aliyofanyiwa na Tara Brown tuone vile Peter Scully alivyokuwa akijibu:

Swali la kwanza aliulizwa *"Kwa nini hasa ulifanya matendo ya kikatili namna ile kwa watoto?"

Hapa tulitegemea jawabu la unyonge na unyenyekevu wa machozi. Lakini Peter, akiwa amekaa kama mtaalamu anayefanya uchambuzi wa research chuo kikuu, alijibu hivi:

*"Ninaandika 'journal' kujaribu kutafuta majibu ya maswali hayo mwenyewe".

Hapo, amejiweka kuwa mchambuzi wa makosa yake mwenyewe! Kwamba yupo gerezani akiandika tafiti za kujitafiti mwenyewe. Kiburi!

Tara aliamua kumchokoza kwa kumtajia mateso aliyokuwa anawapa watoto kwenye video zake, lakini Peter alijibu hivi:

"Hakuna 'excuse' kwa kilichotokea"

Anatumia neno "kilichotokea" wakati alitakiwa kutumia neno "kwa nilichofanya." Anajaribu kuiambia dunia kwamba kilichotokea kilikuwa bahati mbaya tu.

Kuna wakati Peter akawa anataka kupata huruma kutoka kwa Tara, pale anapoanza kuhadithia hivi:

"Niliwahi kubakwa na padre wa Katoliki, huko ndiko shida zote zilikoanzia." Anajaribu kusingizia kwamba alifanyiwa ukatili hivyo na yeye akawa mkatili.

Alipoulizwa kwa nini aliamua kutengeneza mtandao wa vitendo viovu ndani ya Dark Web tena kwa lengo la kupata pesa, alijibu hivi: "Hilo ni takwa la wateja, sio langu. Nilifanya tu kile watu walichotaka."

Huu ni utetezi wa kipuuzi kabisa! Kwamba mtu akikutuma kaue unaenda kuua kutimiza anachotaka, na wewe upate pesa!

Alivyokuwa anaongea alikuwa anajionesha kama alikuwa mfanyabiashara aliyekuwa anazingatia mahitaji ya wateja wake.

Lakini kuna ile sehemu ambayo nayo iliudhi sana. Tara alimwuliza, je, anakubali alifanya matendo mabaya na anajisikia kujutia?

Peter alijibu: Ndio. Anajisikia kujutia. Tara akamwuliza kwa nini? Akajibu: "Bila shaka kila mtu duniani ana majuto yake."

Hapa, anataka kusema kila mtu duniani ni mkatili kama yeye tu. Kwa hiyo tusimfanye asionekane kama amefanya jambo la ajabu kuliko watu wengine.

Tara akamkatisha na kumfafanulia tena swali hilo kwa maneno marefu kidogo, na kumalizia kumwuliza ".. unajuta kwa sababu ya matendo yako au unajuta kwa sababu ulikamatwa?"

Badala Peter ajibu, anaanza kumpongeza Tara kwa swali zuri.

Mbaya zaidi, anacheka! Akampongeza Tara akisema anaiweza kazi yake vizuri. (Yaani, anajifanya kama mtaalamu mashuhuri wa masuala ya uandishi wa habari ambaye anampongeza Tara kuwa anajitahidi kufanya vizuri kazi yake!

Mwishowe, anatoa jawabu la kukasirisha kabisa;

"I’m not going to sit here and say I’m sorry." "There is no point in saying that. It doesn’t change anything."

Kwamba, "Sitakaa hapa kisha niombe radhi. Hakuna maana ya kusema hivyo. Haibadilishi chochote."

Maneno haya yanaonesha wazi kwamba hajisikii kujutia wala haoni uzito wa makosa yake.

Lile neno 'journal' alilitumia mara nyingi kuonesha kwamba yeye ni mtaalamu fulani ambaye anataka watu wasiwe na haraka ya kupata chambuzi zake anazoandika kuhusu matendo yake.

Tuache hilo. Tumalizie na hili. Peter hakukamatwa mwenyewe. Alikamatwa na wasaidizi wake pale ndani.

Lakini, wateja wake wengi sehemu mbalimbali duniani walikamatwa.

Ikumbukwe, wakati Peter anakamatwa, maafisa walifanikiwa kuchukua vitu vyake vyote vya kazi, kompyuta, hard drives, na simu zake. Vifaa hivi vilisaidia kufungua 'database' zake zote.

Na kwa sababu website yake ya No Limits Fun aliiendesha kama 'premium', alitunza rekodi za wateja wake waliolipia kutazama video zake na waliolipia kumtazama 'live'.

Maafisa walitumia anwani za 'Bitcoin Wallet' na rekodi za miamala ya fedha iliyopatikana kwenye vifaa vya Peter, kufuatilia malipo yao hadi kufikia benki walizotumia na kadi zao za benki.

Wateja wengi walipatikana kutoka nchini Marekani, UK, Ujerumani, na Brazil.

Sasa sikia; kwa sababu 'hurtcore' ndio kundi baya kuliko yote linalohusu utesaji wa watoto, mamlaka za usalama zilichukulia mtu yeyote aliyelipia kutazama ni mtu hatari.

Ndio maana ilibidi wateja hao watafutwe.

Makumi ya wateja waliokuwa wamelipia maelfu ya dola na kutoa 'oda' kwa Peter aandae video za mateso kama wapendavyo, wote walipatikana, wakavamiwa, wakakamatwa, na wakashtakiwa na kuhukumiwa katika nchi zao.
 
"Maana yake nini? Kila laini ya umeme unayoiona mtaani, na duniani kote, ina mawimbi yake yasiyofanana na laini yoyote duniani. Jinsi umeme unavyopita kwenye nyaya na kuingia majumbani, unajijengea tabia ya kipekee ya mawimbi (frequencies) ambayo haifananii kabisa na laini nyingine yoyote duniani."
Hapa umetupiga, frequency ya umeme haibafikiki ni either 60 au 50. Nothing more
 
da wewe ni kati ya wachaga waongo.

Walimjuaje?
  1. Kidokezo kutoka Polisi wa Uholanzi: Siri ya mtandao wake ilianza kuvuja baada ya Polisi wa Uholanzi kunasa diski ngumu (hard drive) na kufanya upekuzi kwa mnyanyasaji mwingine wa watoto nchini mwao. Kwenye ushahidi huo, waligundua video za kikatili zilizokuwa zikitengenezwa nchini Ufilipino na kusambazwa kwenye mtandao wa siri (Dark Web).
  2. Kugundulika kwa Wasichana Waliotoroka: Mnamo Septemba 2014, wasichana wawili wenye umri wa miaka 9 na 12 walitoroka kutoka kwenye nyumba aliyokuwa amewafungia minyororo na kuwanyanyasa. Kutoroka kwa watoto hawa kulitoa ushahidi wa moja kwa moja kwa polisi wa Ufilipino (NBI) kuhusu eneo na matendo ya Scully.
  3. Ushirikiano wa Kimataifa: Kikosi maalum cha kimataifa cha kupambana na unyanyasaji wa watoto kwenye mtandao (Virtual Global Taskforce), kikishirikisha polisi wa Australia (AFP), Uholanzi, na Interpol, kilifuatilia anuani za mtandao (IP addresses) na miamala ya kifedha iliyomunganisha Scully na biashara hiyo ya pay-per-view (kulipia ili kutazama).

Alikamatwaje?
  • Mtego na Ufuatiliaji (Stake-out): Baada ya kubaini eneo lake la siri katika mji wa Malaybalay, timu ya pamoja ya maofisa wa Ofisi ya Kitaifa ya Upelelezi ya Ufilipino (NBI), Polisi wa Jinai (CIDG), wakisaidiwa na maajenti wa polisi wa Australia na Uholanzi, walifanya mtego wa siri na kumvizia kwa muda wa wiki tatu.
  • Kuvamiwa na Kukamatwa: Mnamo Februari 20, 2015, maofisa hao walivamia nyumba aliyokuwa amepanga huko Barangay Violeta, Malaybalay. Walimkamata Scully akiwa ndani, na wakati wa upekuzi, walikuta watoto wengine wakiwa wamefungwa minyororo sebuleni kwake.
Baadaye, upelelezi zaidi kwenye nyumba nyingine aliyowahi kupanga katika mji wa Surigao ulisababisha kugundulika kwa mabaki ya mwili wa msichana wa miaka 12 aliyekuwa amemwua na kumzika chini ya sakafu ya jikoni.

hayo mambo yako ya Frequency ni uwongo mtupu.
jifunze frequency hapa kwenye kitabu changu cha 2.

"Maana yake nini? Kila laini ya umeme unayoiona mtaani, na duniani kote, ina mawimbi yake yasiyofanana na laini yoyote duniani. Jinsi umeme unavyopita kwenye nyaya na kuingia majumbani, unajijengea tabia ya kipekee ya mawimbi (frequencies) ambayo haifananii kabisa na laini nyingine yoyote duniani."
Hapa umetupiga, frequency ya umeme haibafikiki ni either 60 au 50. Nothing more
kabisa
 
Hatari sana ,no one is safe kwenye ulimwengu huu
Kule kwa moto sana... Back then kama 2013 kuna laptop ya jamaa alikuja nayo school kipindi nipo o level hapo kuna video alikuwa nazo tukawa tuna watch ..si unajua ushamba ushamba ule mtu kama 20 mnachungulia laptop moja ku watch kilichomo humo.. Kuna video moja ya ngono ya mtoto....ile video iliniachia trauma mbaya sana mpaka kesho kila nikijaribu kuikumbuka....asee sio poa ..itakuwa huyo jamaa aliitoa humohumo.. maana laptop yenyewe ilikuwa ni ya ticha mmoja hivi wa field ambaye ukimchunguza kiaina alikuwa na pigo na tabia za wale psychopaths.
 
Aisee. Hatari sana mkuu!
 
Back
Top Bottom