Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Kwa muda mrefu sasa, Tanzania imekuwa ikishuhudia matukio yanayoacha maswali mengi miongoni mwa wananchi: matumizi ya nguvu kupitiliza na ukiukwaji wa sheria na kanuni za Jeshi la Polisi.
Katika matukio mbalimbali ya kukamata waandamanaji, kutawanya mikutano au kufuatilia visa vya uhalifu, mara nyingi kumeibuka taarifa za wananchi kuumizwa vibaya, wengine kuachwa na ulemavu wa kudumu, na wachache hata kupoteza maisha. Yote haya yamekuwa yakijenga taswira ya uadui kati ya raia na polisi, jambo linaloweza kuwa hatari kwa usalama wa taifa.
Mara nyingi, viongozi wa serikali na hata wa dini husema, “tusiiwachie hasira zituongoze, tuache sheria ichukue mkondo wake.” huku wengine wakisema "Hasira hukaa kifuani mwa mtu mpumbavu".
Lakini changamoto kubwa ni pale wananchi wanapoona sheria hiyo hiyo inateleza au inageuzwa silaha ya kuwalinda wahusika badala ya kutoa haki. Askari polisi waliotajwa kuhusika na matukio mabaya mara nyingi hukaa kimya bila kuchukuliwa hatua, na hili ndilo linalochochea hali ya kukata tamaa miongoni mwa wananchi.
Kuna swali kubwa ambalo linahitaji mjadala wa kina: je, itakuwaje siku moja wananchi wakiamua kulipiza kisasi? Hali hii siyo ndoto bali ni hatari inayoonekana wazi na ni bomu linalokaribia kulipuka.
Tusisahau kuwa Polisi na familia zao wanaishi miongoni mwa wananchi wa kawaida. Wanakula katika migahawa pamoja na wananchi, hununua mboga sokoni, na kupata huduma kwenye maduka ndani ya jamii.
Lakini fikiria kama muuzaji huyo wa duka amepoteza kaka yake mikononi mwa polisi? Fikiria kama mpishi mgahawani ana jeraha la maisha kutokana na risasi ya polisi?
Hasira hizi zikigeuka chuki na kuchukua mkondo wa kisasi, taifa linaweza kuingia kwenye janga la mauaji ya kulipizana, ama kwa sumu katika chakula, ajali za kutengenezwa, au mashambulizi ya siri.
Kwa sasa, hali bado inashikiliwa na imani ya wananchi kuwa kuna uwepo wa sheria na taasisi zinazoweza kutoa haki. Lakini ikiwa hali hii ya ukimya wa mamlaka itaendelea, upendo wa wananchi kwa polisi unaweza kuyeyuka na badala yake kuzaliwa wimbi la kulipiza kisasi.
Hatua hii ingeifanya Tanzania kuwa uwanja wa vita vya ndani kati ya raia na polisi, hali ambayo inaweza kuangamiza mshikamano wa kijamii na usalama wa taifa kwa ujumla.
Ni muhimu kwa Jeshi la Polisi kutambua hatari hii na kuanza kujisafisha kwa vitendo. Askari wanaokiuka maadili wachukuliwe hatua waziwazi ili kurejesha imani ya wananchi. Polisi wanapaswa kukumbuka kuwa wao siyo “miungu watu,” bali ni watumishi wa umma wanaopaswa kulinda maisha na mali ya kila raia bila upendeleo.
Bila mabadiliko ya kweli, hatari ya kisasi inaweza kuibuka siku ambayo hakuna yeyote atakayeweza kuizuia.
KUMBUKA JAMII NI WATU, NA JAMII NDIO MAJIRANI ZENU.