Mkuu hapa nadhani unachanganya mada,
Kimsingi ni kweli lengo mahsusi ni kuwaondoa wavamizi wa mashamba, ambao kwakweli naishukuru serikali kwa moyo wa dhati kwa kulifanyia kazi jambo hili!
Yaani ni kama walisha unda jeshi dogo na himaya yao, mtu alipokuwa akisogelea eneo lao anaulizwa maswali na wasipo rizika na majibu wanakupa mkong'oto haswa! Na usilogwe ukasogea na gari, na kama lina namba za serikali ama SU ndo kiama yako imekukuta! KWA KWELI KWA HILI NAIPONGEZA SANA SERIKALI KUKOMESHA UHUNI HUU,
Angalizo:
Kuna askari wasiokuwa waaminifu ambao wametumia mwanya huu kudhulumu mali za wananchi wasio kuwa na hatia. Na pia kumekuwa na tatizo la kubomoa hadi nyumba zisiziko husika. Nawasihi waongeze umakini kwa haya mambo mawili yasiharibu nia njema ya kukomesha uharamia huu.