SoC04 Ukaushiaji dagaa bado kitendawili Mwanza

SoC04 Ukaushiaji dagaa bado kitendawili Mwanza

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mzalendo Mwidima

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Wakazi wa Mwanza ukaushaji dagaa bado ni kitendawili kwao kutokana na mwalo wa kuanikia dagaa kujaa maji.

Wakizungumza na NyakiTv wakazi wa Kijiwenu Chifunfu Sengerema Mwanza wameeleza changamoto wanazopitia kwenye ukaushaji dagaa Domina Benedicto Mwenyekiti wa kikundi cha Faraja ambacho kinajihusisha na uchakataji wa dagaa amesema changamoto wanazopitia wakati wa uchakataji ni Pamoja na kukosekana sehemu ya kuandika dagaa

“Dagaa zinaoza kutokana na kushindwa kukauka kwa sababu mwalo wetu umejaa maji hii inapelea kupata losi kwani dagaa hata ukinunua bei kubwa inakulazimu uiuze kwa bei ndogo”amesema Domina

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa mitaji yao inakatika kutokana na dagaa kuoza hasa kipindi cha masika “Mitaji imekatika kutokana na dagaa kuoza kipindi cha masika kwa hiyo mitaji imekuwa michache”

Pia katibu wa kikundi cha Faraja Riziki Jumamzizi ameeleza hasa changamoto wanazopitia ni kukosa vitendea kazi vya kuanikia dagaa hasa kipindi cha mvua

“Tunakosa vitendea kazi vya ukaushaji dagaa hasa kipindi cha mvua kutokana na mwalo wetu kujaa maji”amesema Riziki

vilevile ameongeza kwa kusema kuwa mbali na kukosekana vitendea kazi hawana mitaji ambayo ingewasidia katika biashara zao

“Hatuna mitaji ya kutusaidia katika biashara zetu”

Nae Amina Mkama mwana mama ambaye amefanya biashara ya uchakataji wa dagaa kwa mda mrefu ameeleza kuwa kukosekana kwa wateja na masoko maalumu ya dagaa ni changmoto kwao

“Hatuna masoko ya kuuzia dagaa pia hatuna wateja maana tunao wateja wa hapa na pale na kupelekea kuuza dagaa kwa bei ndogo”

Pia Mgendi Ndagabona nae ametoa kilio chake kwenye uchakati wa daga ni kukosekana kwa mifereji ya maji kwenye sehemu za ukaushaji wa dagaa kwani wanaanika chini dagaa hasa kipindi cha mvua

“Changamoto tunayo pata ni kukosekana kwa mifereji ya kupitisha maji kwenye maeneo ya kukaushia dagaa kwani tunaanika chini dagaa zinzasombwa na maji”amesema Mgendi

Wakazi wa kijiweni chifunfu sengerema mwanza wanao jihususisha na uchakataji wa dagaa wametoa vilio vyao kwa serikali kuhusu changamoto wanazo pitia kwenye uchakataji wa dagaa hasa kipindi cha mvua Bi Domina Benedicto amesema kuwa serikali iwasaidie mashine za kukaushia dagaa kwani walisha wapa semina kuhusu mashine hizo lakini hazijawafikia

“Serikali tuliomba itusaidie sola za kukaushia dagaa lakini mpaka hasa hazifika tunaiomba serikali itusaidie ”amesema Domina

Nae Amina Mkama ametoa ombi lake kwa serikali ni kuhusu kupatikana kwa masoko maalumu ambayo yatawasidia katika kuuza dagaa zao

“Naiomba serikali kutusaidia kupata masoko ya dagaa ambayo yatatusaidia kuuza dagaa zetu kwani mpaka sasa tuna wateja hapa na pale”amesema Amina

Akizungumza na NyakiTv Mwenyekiti wa BMU Kijiwenu Chifunfu Sengerema Mwanza Banyenzachi Kasunzu amesema kuwa moja kati ya changamoto wanazopata wachakataji ni mda wa masika dagaa hazikauki kwa wakati

“Wakati wa masika wachakataji wa dagaa wanapata tabu sana kutokana na maji kujaa na dagaa kushindwa kukauka kwa wakati” amesema Banyenzachi

Pia ameongeza kwa kuomba Serikali na wadau ambao wamekuwa wakitoa semina kwa vikundi mbalimbali vya uchakataji kuhusu mashine za ukaushaji wa dagaa bila kutimiza ahadi zao kwao

“Tangu mwaka jana wamekuwa wakitoa ahadi kuhusu vifaa vya ukaushaji wa dagaa wanaenda jumla tunaimba serikali itusaidie mashine za kisasa kwa wachakataji wa dagaa”amesema Banyenzachi

Hivyo basi kutonana na sekta ya uvuvi kuchangia pato 1.8hadi2.5kwenye serikali ni vyema serikali kuweza kujenga masoko maalumu ya dagaa pia kutafuta masoko kimataifa ili kuweza kuongeza pato la Taifa na wavuvi wenyewe kwenye shughuli zao za uvuvi pia Serikali inapaswa kuwawezesha wakina mama kwa kuwapatia mitaji ambayo itawasidia kwenye shuguli zao za uchakataji wa dagaa Chifunfu Sengerema Mwanza.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom