UKAWA acheni utoto!

Ina maana walilipwa in advance posho yote?

inawezekana, na hii ndo weakness ya sirikali hii, mkiona watu wanapiga kelele hii iondoke mnasema UKAWA wachokozi , ona sasa sirikali walivo weak,wanalipa watu hata kabla hawajafanya kazi....
 


Ndugu yangu naona umelewa madaraka. Unadhani kisima cha fedha zenu za kuhonga hakitakauka? Subirini huku kwa wnanchi. Ipo shida ya watu wasiojijua kama wewe. Dalili la Anguko lenu sasa ni dhahiri....
 

@Nape Nnauye huna hadhi ya kuwashambilia UKAWA hata siku moja.
hawa UKAWA wanasimamia maslahi ya umma kinyume na wewe unayeendekeza utumwa wa kifkra wa enzi za zidumu fikra za kikwete.
 
Tatizo sio hao waliotoka tatizo ni hao waliobaki dah kuna wamama walikua wanachangia nkajiuliza hili ni bunge au ni kitchen party....

Wajipange sana
 

sina mengi naomba kunukuu wimbo wa lucky dube. Rastaman prayer
There comes a time
In everyman's life where he's got to face
The truth no matter what.
We are coming to you father
With our sins and everything
To thank you

Politicians thank you father
For making them to be able
To lie with a straight face
While the nation cries
They wanna thank you lor
 
Kwa hiyo katiba itakuwa ya CCM sio ya watanzania hata watakao piga kura za maoni watakuwa wa CCM pia.Chezea chama tawala.
 
Kwanini UKAWA wamechukua Posho kisha "wakapita hivi?" kwanini wasingesusia na POSHO? swali liko hapa!

Posho ni za ccm kwan nyie?
Pesa ngap za wananchi zinaliwa mnanyamaza
 
Haya yote yana mwisho wake. CCM wasidhani watatawala milele, soon tu wata-regret kwani wananchi wameshachoka hila zao.

Wamefunga akili as if wingi wao ndani ya bunge ndio wingi wa wenye nchi!!!

WAMEJISAHAU SANA!
 

Mdharau mwiba mguu huota tende.Tusidharau maoni/ hisia za wachache
 
Tatizo lako huwezi jenga hoja kila siku nakwambia unakurupuka tu angalia ulichoandika sasa..!! Tafuta mtu awe anakusaidia

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
nape? ww ndio wa kuwaita UKAWA watoto? we unaona kuwa hapo ccm umefika sana eh? unafurahia kula ela zetu na kutoka kitambi eh,. Mungu hataniwi endeleeni kuwaibia wananchi mwisho utaona faida yake.
 

Mbona yanayoendelea bungeni unayafuata kama wewe ni remote control? Umeongea kwenye mikutano ya hadhara juu ya lisu haijakusaidia kitu, leo unahamia kwa UWAKA sorry UKAWA, Wewe kama nani katika nchi hii?

Angalia wenzako pia huu hapa chini, wanaona nchi hii kama yao

1. Mwigulu - Serikali tatu, over my dead body, over my dead body

2. Januari Makamba, - Sisitunaokwenda kuiongoza nchi hii, hatutaki kuikuta ikigawana mali
 
Kwanini UKAWA wamechukua Posho kisha "wakapita hivi?" kwanini wasingesusia na POSHO? swali liko hapa!
Ndio hapo nimeshangaaje na kusikitika mwanzoni nilisema hawa wanatumiwa na isitishe wamehongwa sasa kila kukicha wanaona lengo lao halitiimi inabidi waanze plani B. waliyoiandaa ya kuvuruga mchakato mzima wa Katiba.

Sikutegemea Lipumba awaka very low kiasi hicho kwa kuwaita wenzie interahamwe huku akijua fika kuwa Interahamwe ni kundi la kihutu lililoongoza mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.. Hivi ukiunganisha nukta hupati jibu Kagame alishawahi kumtusi Kikwete anawasaidi FDRL ambalo ni kundi la Kihutu lililohusika na Mauaji ya Kimbali. Kisa tu alitoa ushauri wazugumze.

Sasa Lipumba kaona bora atamke Interahamwe kwa sababu wimbo ni ule ule wa kuwaambia Watanzania wote Wanaopenda amani, umoja na muungano uendelee leo wamekuwa ni wenye chuki na wanaojiandaa na mauaji ya Kimbari. kama INTERAHAMWE.

KWELI KUWA MZEE SIO KIPIMO CHA HEKIMA.
 
Hiyo siyo rasimu ya Warioba ni ya Kikwete(Raisi) wanapotosha kwani Warioba alitoka kwake akaenda kukusanya maoni bila kutumwa?Acheni kudanganya wananchi. Alichotumwa Warioba kwa Wananchi alileta ila Hawataki kuelewa kuwa hao ndio wananchi waliopendekeza sasa wanaandika yao. Ujanja ujanja tu. Ikiwezekana mwenye nchi asitishe Bunge maana wanaongea siasa za TANU NA ASP.
 
Lisu katukana mpaka basi baada ya matusi kuisha wametoka kwenye bunge wakatafute matusi mengine.
 
@Nape Nnauye huna hadhi ya kuwashambilia UKAWA hata siku moja.
hawa UKAWA wanasimamia maslahi ya umma kinyume na wewe unayeendekeza utumwa wa kifkra wa enzi za zidumu fikra za kikwete.
Umma gani ambao unazungumzia labda pengine ni umma wa tengeru na kibosho.
 

kwa Nape ni ngumu sana kukujibu
 

Kizuri ni kuwa watu walishaachaacha kukuchukulia serious but hata hivyo inabidi tukujibu tu.Wazalendo ndio wametoka kwa sababu wangetaka posho wangeendelea kukaa kama hao waliomo leo.CCM ndio walioharibu mchakato huu na UKAWA si UWAKA kama ulivyosema ilibidi wawaelezee wananchi mapungufu kama walivyofanya ndio waachie interahamwe yenu.Endeleeni mbona kinawauma na posho si zenu!!
 
....nape umekua lini kiasi cha kuweza kutofautisha UTOTO na seriouis business. Sijawahi na sitegemei kama kutawahi kutoka jambo la maana toka kwako zaidi ya kupigania maslahi binafsi. kama kweli mnajali maslahi ya nchi mngekuja na hoja na wala si ubaguzi, vitisho, matusi, kejeli na hata kuonyesha dharau ya wazi kwa mawazo yetu wananchi. WEKENI MEZANI HOJA ZENU TUONE KAMA ZINA MASHIKO NA SIO UHUNI UNAOENDELEA SASA. WAKATI WA KURA YA MFUMO WA VYAMA VINGI MLITUTISHA ITAKUJA VITA KAMA YA RWANDA NA BURUNDI, EO IKO WAPI.?CCM ACHENI UTOTO WA KUBAKA DEMOKRASIA KWA HOJA DHAIFU ZA MASLAHI BINAFSI. IPO SIKU MUNGU ATAWAHUKUMU KWA HILO....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…