Mh. Nape
naomba nisaidie kujua endapo hawa UKAWA hawatarudi bungeni kabisaa!! je idadi ya waliobaki inatosha kupitisha mchakato wa katiba?. Kuna hii kauli ya Lukuvi, na zile kauli za bungeni (hasa wawakilishi wa CCM) za ubaguzi wa pemba na ugunja, wana mapinduzi na wapinga mapinduzi ya serikali ya zanzibar, hizo unazichukulia vipi?
Ndugu kiongozi, wewe tayari upo huko kwa wananchi, na unaendelea na siasa je unadhani wananchi huko uliko na kwingineko, wanasubiri katiba mpya? na mwamko wao ni sawa na wenzetu wa zanzibar, kwa maana ya kukaa kusubiria katiba? na lini utaenda ugunja na pemba kuimarisha chama kama unavyo enda kigoma, Sumbawanga, n.k
Nisaidie ndugu yangu, mimi hofu yangu ni kwamba, zanzibar na hasa kwa ubaguzi na vitisho waliopewa wapemba wanaweza kupiga kura za hasira, kukataa serikali mbili ambayo BLK litapitisha, wewe kiongozi unategemea kitatokea nini? huoni kama CCM chama ambacho wewe ni kiongozi kitakuwa kimevunja muungano?
Mwisho kabisa, kwanini CCM chama chenye wanachama na wafuasi wengi, wasomi wa kila fani na wazoefu, wenye majina na maarufu, hamkuwa na plan B?, kwa mfano mngeona serikali tatu ni lazima, na tume ya rasimu imeleta mngetumia hiyo plan B, na kujijenga kisaikolojia, kuandaa muundo wa kiutawala, mgawanyo wa madaraka kwa serikali tatu, kisha uvunjaji ukaletwa na wengne? hamuoni hata muundo huo wa serikali tatu ungekuwa kwa faida ya chama?
Nakutakia ujenzi wa chama ulio na ufanisi
SP