UKAWA acheni utoto!

UKAWA acheni utoto!

Nape Nnauye

MP Mtama
Joined
Dec 26, 2012
Posts
99
Reaction score
408
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!
 
Hivu bwana Nape Nnauye umeona ulichoandika kwenye tittle, umeandika UWAKA sijui ulikusudia kuandika UKAWA.
 
Last edited by a moderator:
Nape nakumbuka ulivyo sota pale Dodoma ukiwa huna dili, sasa naona una maneno kwelikweli kwani dili lilitiki na sasa unakula na kushiba na kukejeli watetea haki Mungu mkubwa na sio Nape
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!
Hujui uzungumzalo,
Kwanza UWAKA ndio nini?
 
Kaeni chini kama muangalie namna ya ku-handle hii issue pia kwa wale viongozi wenye nyadhifa za serikali hata kama ni wanachama wakienda sehemu kwa nyadhifa zao za kiserikali wasizungumze kuhusu misimamo yao kwa kuwa kitakachoonekana pale ni serikali ndio imesema. Wawaache nyie ambao ni purely mpo kwenye post za kisiasa muifanye hiyo kazi. Heading hapo ni UKAWA sio UWAKA
 
pasaka tamu kweli kweli, ukawa ndio wajanja, wamechukua chao mapema wamewaacha wenzao wakipiga miyao bungeni, hii ndi tz bwana
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

Ni jmbo la fedheha sana PR wa Chama Tawala kuandika andika vitu bila kuhariri.Unaishia kuandika vitu vya ajabu ajabu.It's very unprofessional!
 
Hahahaaa wanaotaka katiba mpya wanaogopa uwazi na uwajibikaji kuwa Tunu ya Taifa? Wewe tunakujua kutoka kwao si shida posho ni kodi yetu sisi masikini toka lini vigogo mkalipa kodi zaidi ya kuikwepa?
Huezi jadili mifumo ya serikali ambayo hatukuwatuma.
 
Kweli nape huna akili wewe unawaza posho tu ni jinsi gani unaonyesha ulivyo na njaa halafu siyo uwaka kaka Ni UKAWA
 
Ni jmbo la fedheha sana PR wa Chama Tawala kuandika andika vitu bila kuhariri.Unaishia kuandika vitu vya ajabu ajabu.It's very unprofessional!

Kwanini UKAWA wamechukua Posho kisha "wakapita hivi?" kwanini wasingesusia na POSHO? swali liko hapa!
 
Nape- uwe mwangalifu, wewe ni kiongozi. Kauli zako na porojo zako zinaweza zikazalisha chuki ambazo ni ngumu kuzituliza! Ona hata unakosea jina la kikundi! Wewe ndiye uliyejaa utoto kuliko wote. Kwa nini usikae kimya, ukashaurina na wenzio ndani ya CCM, mkatuletee utatuzi wa hali hii tete mliyotujengee. Huoni hatari katika hili? Kweli wewe u- mtoto hapana wewe ni litoto litukutu sana.
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

Unawaelekeza cha kufanya wewe kama nani kwao .au unajipendekeza !?
 
kwa hiyo nape na timu yake wamefikiria sana wakaona hoja ya msingi kwao dhidi ya UKAWA ni kuchukua posho na siyo hoja walizotoa kuwa kwa nini wanatoka bungeni??,kwani kuna am,baye hachukui posho pale ndani kwa hao walioendelea kukaa???kingine ni kuwa naona anaendelea kuthibitisha alichozungumza bosi wake kuwa wamechoka wapigwe tu..
 
Kwanini UKAWA wamechukua Posho kisha "wakapita hivi?" kwanini wasingesusia na POSHO? swali liko hapa!

Ya Epa ccm walichukua wakapita hivi bilioni 113.
Unazungumzia hiyo ambayo haitoshi kufanyia sherehe za Uhuru wa Tanganyika ya Kusadikika.
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

MKUU hivi pale mnajadili nini?rasimu ya warioba au rasimu gani?maana kwa uelewa wangu ilitakiwa ijadiliwe rasimu ya Warioba ambayo tumeigharamikia mabilioni kwa mabilioni kuipata, au nyie hamuoni uchungu na pesa zetu?
anyway kwasababu hamlipi kodi hamuwezi kuwa na uchungu na hizo pesa, na ndio maana mmeanzisha yenu mnayoyajua. Mimi ni raia huru nisiye na chama lakini nakuambia walichofanya hao jamaa ni sahihi kabisa. na kama nyie mna ubavu basi endeleeni kujadili hiyo katiba, tuone itakuwa katiba ya nani.. mtaipata 2/3 ya kura kuipitisha?labda mchakachue kanuni kama ilivo kawaida yenu, otherwise......
Endeleeni na kikao cha kutengeneza katiba ya chama chenu....
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

Mh. Nape
naomba nisaidie kujua endapo hawa UKAWA hawatarudi bungeni kabisaa!! je idadi ya waliobaki inatosha kupitisha mchakato wa katiba?. Kuna hii kauli ya Lukuvi, na zile kauli za bungeni (hasa wawakilishi wa CCM) za ubaguzi wa pemba na ugunja, wana mapinduzi na wapinga mapinduzi ya serikali ya zanzibar, hizo unazichukulia vipi?

Ndugu kiongozi, wewe tayari upo huko kwa wananchi, na unaendelea na siasa je unadhani wananchi huko uliko na kwingineko, wanasubiri katiba mpya? na mwamko wao ni sawa na wenzetu wa zanzibar, kwa maana ya kukaa kusubiria katiba? na lini utaenda ugunja na pemba kuimarisha chama kama unavyo enda kigoma, Sumbawanga, n.k

Nisaidie ndugu yangu, mimi hofu yangu ni kwamba, zanzibar na hasa kwa ubaguzi na vitisho waliopewa wapemba wanaweza kupiga kura za hasira, kukataa serikali mbili ambayo BLK litapitisha, wewe kiongozi unategemea kitatokea nini? huoni kama CCM chama ambacho wewe ni kiongozi kitakuwa kimevunja muungano?

Mwisho kabisa, kwanini CCM chama chenye wanachama na wafuasi wengi, wasomi wa kila fani na wazoefu, wenye majina na maarufu, hamkuwa na plan B?, kwa mfano mngeona serikali tatu ni lazima, na tume ya rasimu imeleta mngetumia hiyo plan B, na kujijenga kisaikolojia, kuandaa muundo wa kiutawala, mgawanyo wa madaraka kwa serikali tatu, kisha uvunjaji ukaletwa na wengne? hamuoni hata muundo huo wa serikali tatu ungekuwa kwa faida ya chama?

Nakutakia ujenzi wa chama ulio na ufanisi

SP
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

Yaani Nape Nnauye, hivi posho kwa mustakabli wa nchi ni kitu gani? Halafu, hivi unawasikia wale wabunge (hasa wa CCM kutoka Z'bar) namna wanavyoongea matusi na lugha za aibu? Tuwe wakweli kuwa wajumbe walio wengi wanaongea zaidi kuhusu mtu/watu/kikundi badala ya kujikita kwenye mjadala wa vifungu vya Rasimu ya Katiba. Zaidi, wajumbe wengine (hasa CCM) wanaapa kabisa kuwa "kamwe serikali mbili lazima iwepo", kiapo hiki huashiria nini?

Onyo la kutokurudi Bungeni....je, unadhani ni onyo sahihi kwako.....? Haitakiwi kuwa hivyo, kwani Katiba ni mali ya wananchi na sio chama cha siasa, na kudhani kuwa CCM itatawala Tanzania milele basi huo ni upotofu mkubwa.

Nyakati huwa zinabadilika, na ipo siku watanzania watajua haki zao na kudai haki hiyo kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom