Watu wengi wamekuiwa waikjiuliza kuhusu nani aweza kuwa mgombea urais kupitia muungano wa ukawa.kwa maoni yangu, hili sio swali gumu kuliko lile la nani atasimama kwa niaba ya ukawa katika viti vya udiwani na ubunge.
kwa maoni yangu na wengine wanaofatilia siasa za tanzania, swala la mgombea urais kupitia ukawa lipo wazi kabisa kwamba mgombea atakayeweza kukidhi vigezo hivi hapa chini ndiye hasa atakayeweza kuiwakilisha ukawa.na sio vinginenvyo;
1. RUZUKU YA CHAMA HUSIKA.
Kwakuwa ukawa sio chama, ila ni taasisi inayoundwa na vyama na kwa kuwa uchagui mkuu kwa ujumla ni gharama kubwa sana, ni wazi chama kilicho na ruzuku kubwa ndicho kinaweza kutoa mgombea urais labda itokee ukawa wapewe fedha z kusimamisha mgombea urais toka nje ya ruzuku ya vyama husika.kwa maneno mengine, ni kuangalia tuu kati ya chadema, cuf na nccr-mageuzi ni chama kipi kina ruzuku kubwa zaid.
2. UHAI WA CHAMA
Ni wazi kuwa ili ukawa wawezeekushuinda uchaguzi katika ngazi ya urais kama zilivyo ngazi za ubunge na madiwani ni lazima iweke mgombea anayetoka katika chama chenye uhai zaidi.hii ni kwasababu chama chenye uhai kina wapenz na wafuas wengi zaidi.jambo la kujiuliza ni kuwa kati ya vyama vinavyounda ukawa, ni chama kipi chenye uhai zaidi?.
(japo tunaweza kutofautiana katika vigezo vya uhai wa chama).kwa maoni yangu, uhai wa chama waweza kupimwa kwa kuangalia mikutano na shughuli za kisiasa zilizofanywa na chama husika katika kipindi cha kutoka 2010 hadi sasa.kama chama husika sio hai kisiasa, sio rahisi kutoa mgombea anayeuzika kwa watu.
3. MTANDAO WA CHAMA
Kadhalika, ni lazima mgombea husika atokkwenye chama chenye mtandao nchi nzima.hii itasaidia kuratibu shughuli za kampeni na ufuatiliaji wa kura za mgombea husika.chama husika lazima kiwe na mtandao imara na unaofanya kazi a kiuongozi nchi nzima au angalau semehmu kubwa ya nchi ili kweli kiweze kurahisisha kazi ya mgombea urais
4. UMAARUFU WA MGOMBEA HUSIKA.
Bila kujali vigezo vingine kama umri na elimu, mgombea wa urais kupitia ukawa ni lazima awe na mvuto na umaarufu kwa wapiga kura kuliko wagombea wengine wanaoweza kutoka ndani ya ukawa.
Hii ni kwasaabu siasa zetu bado hazijaama kutoka katika umaarufu wa mtu binafsi na kwenda katika sera ake na mipango ya chama husika. kwa maoni yangu,mgombea urais kutoka ukawa atapatikana[pamja na vigezo vingine vyovyote kupitia vigezo hivyo hapo. Nawasilisha