''UKAWA - Mbowe, unatambua hili

''UKAWA - Mbowe, unatambua hili

maguzu masese

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2013
Posts
283
Reaction score
139
Sehemu ya 1 kati ya 5.

10 October 2001, kulifanyika muafaka baina ya CCM na CUF, nakutiwa saini na Philip Japhet Mangula, na Seif Sharif Hamad, na kushuhudiwa na Kingunge Ngombale-Mwiru, Ali Haji Pandu, Mohamed Aboud Moham na Hamad Rashid Mohammed. Mbele ya: Benjamin William Mkapa Ibrahim Haruna Lipumba na Amani Abeid Amani Karume. Moja ya malengo: Kuimarisha mazingira ya maelewano na kuaminiana
Angalia hii orodha, ni ya watu wa aina gani Kirahisi rahisi tu eti leo kweli hawako pamoja, Kingunge ninayemsikia ( nakujifanya namjua), Mkapa ( huyu jamaa tunamchukulia poa sana) Kiukweli tu Lipumba mi hata simzimii kabisa ( kibinadamu sina sababu ya msingi basi tu nimeamua hivyo, nim kama vile Masha mwaka 2010) Kisiasa sioni anachokifanya chenye manufaa kwa taifa hili Zaidi ya asili ya mwanadam ‘selfishness’, CV yake ya kuhama madarasa ndio inampa jianbut sio Kiongozi , any way inferiority complex ni kubwa sana miongoni mwa watanzania , Hata mimi niliyemaliza Form IV ya zamani ( kabla ya division 5) nahisi namzidi mbali sana na hata tukifanya mjadala nitamshinda vizuri tu hili halina ubishi.
Hamadi ( inasemekana ) kuwa anahusika na ADC, So to speak, ni kama ilikuja kwa nia ya kuweka upinzani CDM ( hoja Hii nitaitetea). Mbowe umesahau kuwa kipindi frani kadi za CDM zilikuwa zinachapishwa nchi ya Jirani na zinatumika kwa propaganda? Nadhani hadi sasa bado zinaendelea!!

September28,2012 moja ya vichwa vya habari ni ‘’ CUF yaisaidia CCM kushinda Umeya Mwanza’’ Turufu ya nani anakuwa Meya wa Jiji ilikuwa mikononi mwa CUF ambao walikuwa na wajumbe wawili ndani ya baraza hilo, ambapo ilikuwa wakiamua kuunga mkono upande wowote huo ndio ungeibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho’’ Hatimaye leo Ndg, Mabula ni Meya wa jiji, kwani hata miaka miwili bado haijatimia. Brother hii pia umesahau?

January 4, 2012 Moja ya vichwa vya habari ‘’HAMADI RASHIDI AFUKUZWA ( huyu kumbuka alikuwa moja wa shuhuda wa makubaliano) nab ado siri ya makubaliano anayo. Hii ndio sababu imekufanya leo uone CUF ni washkaji ? anyway hii acha tuipotezee kiaina lakini kwani Kwani ‘’ Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV’’ kipindi kile ulikuwa na sura gani hasa ama mimi ndio mjinga ( mtu asiyekuwa na uelewa juu ya mambo.) na niliendelea kuwa mjinga kabla na baada ya mdahalo ( Nakumbuka hapa kulikuwa na burudani ya aina yake- Mbowe nilikukubali sana kamanda) Tukiachilia mbali Seif Sharif Hamad na cheo chake baada ya Makubaliano

Juzi tu, hata siku mwaka mmoja haujaisha CUF ilifahamika kama ‘ CCM B’, wameolewa na CCM etc , ni lini hiyo ndoa ilivunjika ama hiyo herufi B ilifutika? Vipi Kama ilikuwa ni ya kikristo? Kampeni za Mbatia Kawe ilikuwaje kwani? Baadaye si alienda mahakamani ? Na si ndio CCM wamempa pa kujishikiza naye for the mean time? Na huyu si tulikuwa na mashaka naye juzi juzi tu baada ya kupewa ubunge? Na si tulisahau yote baada ya kusanua issue ya Mtaala wa elimu , so does it mean hii tukio moja tu ndio kawa mshkaji eti? Huyu si aliwahi kuwa na jamaa yake enzi zile baadaye ikatokea TLP ambapo Lema alianzia kutokea huko, na ja,maaa mmoja namkubali sana kamanda Alphonce Mawazo pia alianzia huko, Hawa vijana Wawili wakamkimbia Mrema maana alikuwa ni pandikizi na leo hii kazi wanayo ifanya inaonekana, does it mean wewe leo hii unataka MABELE na MBATIA wapige kazi pamoja eti? Je tofati zao za zamani zimeisha eti? Au bado unasimamia ule msemo wa kushusha mioyo ya matumanini ya wapiga kura na kuwafanya waamini kuwa siasa ni mchezo mchafu ‘’ kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu’’ All in all my point is

Kama mimi ningekuwa WEWE ( kama vipi niachie kwa muda tu), baada ya hili la kujiunga nao kwa sasa baadaye lazima NINGEWAPIGA CHINI, na hata moja ya sababu ambazo zingenifanya niungane nao ni hii ya kwamba niwavutie MWANYA kisha INAKULA KWAO, ( Hapa ndio siasa inakuwaga tamu sana), ningecheza na kufunga Kama Maradona katika mechi ya robo fainali ya kombe la dunia kati ya Argentina na England ,22 June 1986 (One of the most famous goal in football history) na hapa lazima ningejipatia ujiko kinoma maana sasa ningeanza kuwatumikia wananchi ile kwa kwenda mbele kisha nawakumbushia kale ka msemo ketu ‘’ kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu’’.YOU SEE

Iko hivi, hawa washkaji UKIZUBAA wanakupiga chini, na kwenye ramani ya siasa ndio inakuwa KWAHERI mimi ninsingekubali ujinga huu, maana CDM ilipofikia kwa sasa, NCCR, CUF hazikuwahi kufikia. Obvious hawa washkaji kuwa na wewe inawezekana ni moja ya strategies za CCM ili baadaye ile kwako. Hata mimi ndio ningekuwa Strategist wa CCM hapa ningecheza hivi na NINGEKUPIGA kirahisi sana ( hapa kuna njia Zaidi yah ii), sema CCM hawezi na pia hawajui maana hii ni mbinu ni advanced sana kwao hivyo sio size yao hao kina lowasa na kinana ni STANDARD LEVEL tu. Nape wala usimhesabu sema tu yuko juu maana hana mpinzani ktk nafasi yake, Mnyika anapwaya hachezi ipasavyo, nadhani ifikie kipindi sasa hii nafasi mpe mtu aliye nje na huru na majukumu ya bunge( I can defend my argument) Nape angekuwa Chadema angekuwa mzuri sana, hii ndio maana ya Siasa za upinzani……jaribu kunielewa….

Lazima tukubali kuwa CCM wana watu ambao ni strategies wazuri sana ( Kinana na lowasa) na wengine wengi, sema tu upepo wa wananchi umewakataa na kuegemea kwetu hivyo hii ni nafasi ya pekee kuhakikisha kombe tunabeba, ambapo pia kwa hari ya kawaida tu hata kama mimi ningekuwa Ni Kikwete ama kiongozi wa CCM kukupa nchi kirahisi rahisi tu hivi katika democrasia ya herufi ndogo ni impossible, ningekupa nchi pale tu nikiona kweli umepambana vya kutosha na sina jinsi kunusuru hari ya usalama but kwa sasa kuna jinsi ya kufanya na Nchi lazima tunabeba hii haina ubishi kamanda.

Kama mimi ningekuwa wewe, hawa washkaji ningeungana nao kwa nia ya kudai TANGANYIKA TU, kisha nawatosa, kama wanataka kuungana na mimi basi wavue jezi za vyama vyao, wavae ya kwangu kasha twende sawa, wakivaa jezi yangu tunaungana tunasakata kabumbu safi sasa. Lakini bila hivyo hawa washkaji wakisha saidia kuleta Tanganyika tu tunawafanya maaduni maana hata sasa hivi ni maadui, ukiwaamini utakuwa mjinga, kama washauri wako wanakuogopa kukuambia ( washauri waoga sio wazuri)

Tukubali tu kuwa hii Katiba ya sasa haitakuwa nzuri pamoja na kuwa tumeungana na hawa jamaa, hapa mwanya ni mmoja tu, tudai TANGANYIKA, Kisha tukipata katiba ya kutusaidia kuchukua Nchi, tunakaa chini ( watu wachache tu) haiitaji watu 500, tunafanya katiba ya maana ‘ YENYE AKILI’ ambayo itakufanya TOMAS JEFFERSON wa TANGANYIAKA ( Hapa vipi nimekushawishi?)

Moja kati ya watu ambao huwa nawakubali sana Albanie Marcossy aliwahi kusema kwamba hii nchi ili mambio yaende lazima kujitoa mhanga. Sasa hebu niruhusu mimi sasa nikushauri namna ya kuwashinda hawa ccm, hawa ni wepesi sana , kama ni jumapili unawashinda ‘’ KABLA YA MISA YA KWANZA’ msemo mzuri sana nimeunukuu toka kwa Ally Bananga
lakini kwanza acha nijadili na wadau wapenda mabadiliko wenzangu

Karibuni....

'' Dont go into Politics Expecting to be the next Alphonce Mawazo''
- Andrew Nkumbi
 
Nime i copi hii post na kuiweka Jukwaa la Siasa, kutoka jukwaa hili, na nimebadilisha Kichwa cha Habari tu, japo maana imebaki ile ile.

Nimefanya hivi maana najua jukwaa hili lina watu wenye busara sana na hivyo naamini sana ktk Mawazo ya wachangiaji wa hapa.

Jukwaa la siasa najua watu wengi kule ni akili ndogo, so nipo huko najua nini kinatokea mpaka sasa lakini nakabiliana nao vyema.
 
Ninaiona hoja yako kwa uzito wake

Morally is wrong to use people as mean to an end, as far as human dignity is concerned na hii iko wazi sana kwa kila mtu na kwa hari ya kawaida wengi Mtazamo wangu kwa hari ya kawaida( hari ya kibinadamu) sio mzuri kuufuata Bali ni wa kukemea, lakini politically ,wazo langu kwa Mbowe kulifuata ni sahihi kabisa( kisiasa). Kama nukuu moja wapo ya Machiaveli inasema " the end justify the mean"

Bandiko langu ni kutahadharisha tu kuwa ground ya Siasa haikutokea ktk kanuni za ki maadiri, Bali sisi ndio tunafanya na tunajitahidi sana kuweka pamoja maadiri na siasa, ni kweli vinaweza kukaa kwa kiasi furani lakini pia vinaweza visikae pamoja kwa kiasi kikubwa.

Mifano ni sera ktk kampeni na Maneno Mazuri ili kushawishi kura za wananchi, hapa tukio la kushawishi wananchi ni sawa na kuwatumia as a mean to an end ambayo ni ushindi , according to Kanti's Moral theory this is wrong. Na haina tofauti na Ushauri wangu kwa Mbowe

Sasa inakuja kitu kimoja kwamba, Kama tunaingia ktk siasa, kuna mipaka ya kuaminiana, na maadiri yana nafasi ndogo sana( si Rahisi kujua), hivyo Kama mwanasiasa unajua jinsi gani huwa una CHEZA na Maneno kupata kura, juwa kabisa hata wenzio huwa wanafanya hivyo sasa SUALA la kutiliana mashaka ( mwanasiasa mahili) hutakiwi kulitupa kapuni, ni lazima uwe tayari kwa lolote kile na uweke mazingira ya kuzuia na pia at any time lazima ujue kuwa hata wenzio wako hivyo hivyo Kama wewe na Kama kila mtu atakuwa ktk hari Kama hiyo, basi hapa kunafungua mwanya wa Timing as to an end, na safari ndefu unaifanya fupi

Concept ni ndogo sana iliyopo, lakini nimezunguka sana kufafanua kutoa mwanya wa mtu kuwa na Thought experiment....
 
Niliposema naliangalia suala hili kwa uzito wake, nilitafakari uliyosema na kujiuliza kama watu walijiridhisha kuwa wanaweza kuishi pamoja. Si jambo baya kutokea kwasababu kuna wakati furaha au shida zinawaunganisha watu.
Kwa siasa kuna jambo wengi hawalijui, nalo ni kutazama mambo kutoka angle zote.

Huenda ndio mwanzo wao mzuri, sina uhakika na huenda ikawa shubiri nyingine.
 
Mr. Andrew Nkumbi thanks for this useful post

However, sorry to say that with kind of 'shake well before use brain'' when excitation surpassing logic no one is ready to think about those.

Thats why you can see people like Nguruvi will say ''it is a new start'' !!! he will never argue, he will never give you logic behind that history, he will never tell you why now?? he will say ''it is okey'

in the next two years, they are the ones who will write long articles why upinzani failed in Tanzania

lets watch
 
Waberoya , kwanza niweke nukuu za niliyoyasema ili kuonyesha kuwa bandiko lako umekuja ukiwa na reservation au prejudice kwa Nguruvi3.

Ninaiona hoja yako kwa uzito wake

Niliposema naliangalia suala hili kwa uzito wake, nilitafakari uliyosema na kujiuliza kama watu walijiridhisha kuwa wanaweza kuishi pamoja.
Si jambo baya kutokea kwasababu kuna wakati furaha au shida zinawaunganisha watu.
Kwa siasa kuna jambo wengi hawalijui, nalo ni kutazama mambo kutoka angle zote.

Huenda ndio mwanzo wao mzuri, sina uhakika na huenda ikawa shubiri nyingine.

Hayo ndiyo niliyoyasema. Nukuu ya kwanza nilimaanisha kuwa hoja za Andrew Nkumbi niliziangalia kwa uzito kutoka kona nyingine kwa maana kuwa sijui kama kulikuwa na tafakuri wakati Mbowe anachukua hatua na kama zipo je zinakidhi haja kama alivyoainisha Nkumbi.

Nukuu ya pili, mwisho nikasema shida naraha huwaunganisha watu nikimaanisha 'marriage by convenience''
Nikaendelea kusema katika siasa kuna mambo ambayo watu hayawangaalii kutoka kona mbai mbali. Hapa pia nilimaanisha kuwa huko nyuma vyama vya upinzani havikuona umuhimu wa kuungana kwa kukosa mitazamo ya kona nyingine.

Nilimaliza kwa kusema, huenda ni mwanzo mzuri, nikisisitiza SINA UHAKIKA, nikaendele kusema inaweza kuwa SHUBIRI.
Nilichomaanisha ni kutokuwa na uhakika na ushirika huo kama utazaa matunda au utageuka kuwa mwiba kama ilivyokuwa huko nyuma. Maneno Sina uhakika na shubiri ni muhimu sana katika nukuu zangu

Waberoya amechukua neno na kulindika kwa kiingereza kaipotosha maneno yangu kabisa.
Sijui kwani amefanya hivyo . Najua kuwa si kila ninchoandika kinawapendeza watu, na Waberoya ni mmoja wapo. Nakuomba usiniwekee maneno, kama ni mjadala tuufanye kwa kuwa wakweli

Nadhani umeamua kutumia maneno ya dharau dhidi yangu si kwa uzi huu ni kutokana na nyuzi na mabandiko mengine yanayokuudhi sana, mengine yakigusa interest zako.

Naomba nikuambie ukweli, mimi huwa siangalii nani kasema nini, sina ushabiki wa vyama wala shibakii Zitto Kabwe au Fahmi Dovutwa. Ninapiga kila ninapoona inafaa kwa mtazamo wangu.

Nipo huru sifungwi na mawazo ya mtu au watu. Sutakuomba radhi kama kuna mahali pengine nilikokuudhi, nitatoa maoni yangu kama mimi bila kuwa na wasi wasi na interest zako pengine.

Sitakuwa na reservation au prejudice kwako, nitakuwambia ninachotaka kusema na si kile unachotaka kusikia.

Ahsante

Nilisoma sijaona ubaya wowote aliofanya Mbowe. Kama mwanasiasa ni lazima achukue nafasi zinazojitokeza. Na nafasi zingine itabidi ashirikiane na kambi zingine za kisiasa kwa manufaa ya taifa, chama au binafsi.
 
Kwa ufupi huu unaoitwa "Ushirikiano" au "Muungano" au "Umoja" wa UKAWA haukufikiriwa kwa ina sana. Kwani inaonekana umetokana hasa na kudai Tanganyika. Sasa suala la kudai Tanganyika ni suala la sera tu kwa vyama; kwa upande wa CCM wao sera yao wameendelea nayo ni ya serikali mbili. Sasa kama itaendelea hivyo (serikali mbili) ushirikiano huu utakuwa unaundwa kwa ajili ya nini kwa sababu ukiangalia sana utaona kuwa CCM iko kwenye offense na uwezekano wa kushinda ni mkubwa sana kwani wakati UKAWA wanalilia Tanganyika CCM wanalilia serikali za Mitaa baadaye mwaka huu na tayari tunajua kuwa uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa utafanyika chini ya Sheria na Katiba ya sasa.

Now... hata kuandika haya siku hizi yanaboa kwa sababu hofu yangu ni kuwa mwamko wa kutaka kuiondoa CCM madarakani ambao ulikuwepo kuelkea uchaguzi wa 2010 unaanza kufifia au kufifishwa kuelekea 2015... kwanini bado sijajua.
 
Hiki ni kilio cha wote wapenda mabadiliko
 
Waberoya , kwanza niweke nukuu za niliyoyasema ili kuonyesha kuwa bandiko lako umekuja ukiwa na reservation au prejudice kwa Nguruvi3.

Hayo ndiyo niliyoyasema. Nukuu ya kwanza nilimaanisha kuwa hoja za Andrew Nkumbi niliziangalia kwa uzito kutoka kona nyingine kwa maana kuwa sijui kama kulikuwa na tafakuri wakati Mbowe anachukua hatua na kama zipo je zinakidhi haja kama alivyoainisha Nkumbi.

Nukuu ya pili, mwisho nikasema shida naraha huwaunganisha watu nikimaanisha 'marriage by convenience''
Nikaendelea kusema katika siasa kuna mambo ambayo watu hayawangaalii kutoka kona mbai mbali. Hapa pia nilimaanisha kuwa huko nyuma vyama vya upinzani havikuona umuhimu wa kuungana kwa kukosa mitazamo ya kona nyingine.

Nilimaliza kwa kusema, huenda ni mwanzo mzuri, nikisisitiza SINA UHAKIKA, nikaendele kusema inaweza kuwa SHUBIRI.
Nilichomaanisha ni kutokuwa na uhakika na ushirika huo kama utazaa matunda au utageuka kuwa mwiba kama ilivyokuwa huko nyuma. Maneno Sina uhakika na shubiri ni muhimu sana katika nukuu zangu

Waberoya amechukua neno na kulindika kwa kiingereza kaipotosha maneno yangu kabisa.
Sijui kwani amefanya hivyo . Najua kuwa si kila ninchoandika kinawapendeza watu, na Waberoya ni mmoja wapo. Nakuomba usiniwekee maneno, kama ni mjadala tuufanye kwa kuwa wakweli

Nadhani umeamua kutumia maneno ya dharau dhidi yangu si kwa uzi huu ni kutokana na nyuzi na mabandiko mengine yanayokuudhi sana, mengine yakigusa interest zako.

Naomba nikuambie ukweli, mimi huwa siangalii nani kasema nini, sina ushabiki wa vyama wala shibakii Zitto Kabwe au Fahmi Dovutwa. Ninapiga kila ninapoona inafaa kwa mtazamo wangu.

Nipo huru sifungwi na mawazo ya mtu au watu. Sutakuomba radhi kama kuna mahali pengine nilikokuudhi, nitatoa maoni yangu kama mimi bila kuwa na wasi wasi na interest zako pengine.

Sitakuwa na reservation au prejudice kwako, nitakuwambia ninachotaka kusema na si kile unachotaka kusikia.

Ahsante

Asante Nguruvi, nimekupata
 
haya ni mahesabu ya kisiasa na si ya kihandisi...
ukikosea unyanyui ndege...

mtazamo wangu nawapa 0.3 ukawa kufika malengo..
 
Kwa ufupi huu unaoitwa "Ushirikiano" au "Muungano" au "Umoja" wa UKAWA haukufikiriwa kwa ina sana. Kwani inaonekana umetokana hasa na kudai Tanganyika. Sasa suala la kudai Tanganyika ni suala la sera tu kwa vyama; kwa upande wa CCM wao sera yao wameendelea nayo ni ya serikali mbili. Sasa kama itaendelea hivyo (serikali mbili) ushirikiano huu utakuwa unaundwa kwa ajili ya nini kwa sababu ukiangalia sana utaona kuwa CCM iko kwenye offense na uwezekano wa kushinda ni mkubwa sana kwani wakati UKAWA wanalilia Tanganyika CCM wanalilia serikali za Mitaa baadaye mwaka huu na tayari tunajua kuwa uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa utafanyika chini ya Sheria na Katiba ya sasa.

Now... hata kuandika haya siku hizi yanaboa kwa sababu hofu yangu ni kuwa mwamko wa kutaka kuiondoa CCM madarakani ambao ulikuwepo kuelkea uchaguzi wa 2010 unaanza kufifia au kufifishwa kuelekea 2015... kwanini bado sijajua.

Mzee Mwanakijiji, kweli kuandika haya Yanaboa nakubaliana kabisa na wewe. Kuna kitu kimoja vyama pinzani vinashindwa kuelewa kuwa hii CCM wanayotaka kuitoa wasidhani kama inaweza kuachina nchi kirahisi kama wanavyoweza kufikiria akili na nguvu ya ziada inahitajika.

Toka mwaka 2010 tunaelekea miaka mitano sasa akili nyingi tumezielekeza kuwaza kuhusu uchaguzi wa 2015, Graph ya mwamko ya mwaka 2015 haitakuwa kama ile ya Mwaka 2010. Suala la kufanya maamuzi yoyote ( hata kama ni madogo) ktk siasa yanahitaji Umakini mkubwa sana si kwa ngazi ya chama tu bali kwa wananchi wote waliokwisha weka matumaini juu ya chama.

Nyayo tunazoacha zisiwe nyayo zinazorudi nyuma, tunahitaji nyayo zenye uelekeo wa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom