mbona jana kibandamaiti zenji maalim seif aliliongelea kwa kupinga vikali na kutolea ufafanuzi vizuri mkuu?
Sijamsikiliza mkuu
Kuna mdau katoa mchango mzuri sana mi nahisi wana makusudi yao kukaa kimya muda bado UKAWA ina watu hatari sana na wenye trick za kali na za ajabu mno mwaka huu CCM wana kazi ya ziada
Ukimya kwa mtu anayedhamiria uropoke ni jibu muafaka sana tena lisilokuwa na utata!!..Kumbuka "Uzushi haukanushwi,kuukanusha ni kuupa nguvu"
mwenyewe wananiuz akina mama ni waoga wakiambiwa kuwa nyie ndo mtaumia basi wanaaminKama hvyo sijui lkn wasilipuuze hili! nasisitiza umma wa watanzania wapo very delicate, anything can change them hasa hasa kitu hatarishi! chadema watch out!
Chadema wanapenda ku dili na ishus kubwa kubwa, ishus ndogo ndogo wanaona uzushi!
Sasa kwa taarifa yenu wenye uelewa wa ishus kubwa kubwa ni wachache sana na wala hawana mzuka wa kupiga kura! Ishus ndogondogo ndio wengi na ndio wapiga kura!
Afisa yeyote wa chadema wakishirikiana na wa ukawa kwa mamlaka ya chama aite press afanye yake, sio lazima maafisa wakuuuuubwa!
Hawa chadema nao sometimes wananiangusha sana! sijui tumechoka au tumelewa sifa!
Video ya lowassa tu ambayo hata sio genuine magamba wakaruka nayo, hili la libya chadema tunaendelea kupiga poyoyo tu! Kama vile tunashindwa kuendana na kasi ya mabadiliko!
Bao la mkono! Computer kwa kila mwalimu! Yote yamekanushwa na mazimwi! Na yote hayo wamesema na jamii ikawasikia, halafu unasema upuuzi haukanushwi? Lazima ufahamu hadhira yenyewe ipoje!
Msemaji wa chama tawala anasema goli la mkono sisi tupo kimya tu! Mgombea urais wao analeta mambo ya libya sisi tupo kimya tu! Aisee inataka moyo sana hii!
Katika siasa kila linalotamkwa lina nia na kusudio lake,ni hekima kwa mlengwa kufahamu haswa lengo la msemaji lilikuwa ni ni lipi?Unaweza ukalishughulikia kimya kimya ama ukalipuuza ama ukatafakari muda wa kulijibu utakao kuwa hauna madhara. Hakika nakuambia jambo lolote utakalolikanusha ama kulizungumza katika media linazua jambo jingine.Ni mara kadhaa umeshasikia mtu anakanusha jambo hadharani halafu linamrudia yeye!!Bila shaka umeona la Dr.Mihogo,ni kama amejipaka ----- wakati alidhani angefanikiwa kusambaratisha UKAWA.Ukilazimisha nitajua wewe si mmoja wetu katika mabadiliko!!